Tunaishi nyakati za mwisho. Hivi karibuni, baragumu italia, na hapo tutaungana na mwanamwali atakayetoka mbinguni.
Na pale mpinga Kristo atakapofichuliwa, atatimua mbio akijaribu kufukuzana na muda kutenda uovu wake. Ni siku 1260 zitakuwa zimebaki wakati ule wadhiki kuu aangamie. Bibilia inasema atakapofika, atakuwa na muda mfupi: "Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache" (Ufu. 17:10).
Nyakati hizi ni sawa na zile yapata karibu miaka 2000 pale Kristo aliposema msalabani: IMEKWISHA. Yote yakuwezesha mtu kupokea wokovu yalikuwa yametimizwa, na sasa ilikuwa ni juu yetu sisi wanadamu kukubali au kukataa kupokea wokovu. Muda uliopo wa kueneza injili unaisha. kazi ya kueneza injili karibu inafikia mwisho. Tunaelekea wakati ambapo watumishi wa Mungu watatuzwa, na wale ambao ni wafuasi wa mwovu shetani watahukumiwa na kuadhibiwa.
Lakini je, Kristo alimaanisha nini kabisa alipolia msalabani na kusema Imekwisha!
Kristo alisulubiwa kwa ajili ya dhambi zetu sisi wanadamu (Isa. 53: 5-6). Na hii inatokana na sababu, malipo ya fddhambi ni kiifo (Warumi 6:23) haikuwa tu anapata maumivu na kuumia, ila ilikuwa ni lazima afe kifo kwa ajili yetu. Yeye alikufa badala yetu (substitutionary death). Na pale alipokufa, yeye alitimiza yale Mungu alikuwa amepanga kwa ajili yetu sisi wanadamu. Ni kutokana na kifo chake tumepata wokovu. Kifo cha Kristo kilipangwa na Mungu ili sisi wanadamu tiuweze kupata wokovu. Kama hangekufa, basi tungekuwa viumbe vilivyo hukumiwa na kufa. Hakukuwa na njia ya wokovu.
"Wakati wa mwisho kabisa kabla hajafa, Kristo alisema: Yesu akalia kwa sauti kubwa, akasema Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu" (Lk. 23:46).
Na hapo akalia na kusema Imekwisha! (Yoh.19:30).
Neno alilotumia ni "Tetelestai" katika karne ya kwanza, lilikuwa na maan "malipo yote yametolewa." Katika kiGriki, neno hili lilitumiwa kwenye risiti kuonyesha kwamba, malipo yote yametolewa kwa ukamilifu. Ndiyo maana Kristo alikuwa nayo alipolia pale msalabani; kwamba malipo yote ya kukuwezesha kuokoka yametolewa.
Je, umewahi kufikiria na kuwaza kuhusu jambo hili kwamba Kristo alikununua na kutoa malipo yote kwa kutuimia damu yake mwenyewe? Mtume Paulo anatukumbusha kwamba Kristo alitununua kwa bei ya juu sana iliyo damu yake.
"Maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi mtukuzeni Mungu katika miili yenu" (1 Kor. 6:20).
Naye Petro alisema hivi: "Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwanakondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo" (1 Pet. 1:18-19).
Ushuhuda wa wazee mbinguni katika Ufunuo 5:9 pia watilia mkazo jambo hili kwamba tumeokolewa kupitia damu ya mwanakondoo.
Je, una uhakika kwamba umepokea wokovu? Na kwamba malipo yote ya kukuwezesha kupokea wokovu huu yameshalipwa? je, umetubu dhambi zako, ili upokee msamaha? Neno la Bwana lasema hivi katika Mithali.
"Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema" (Mit. 28:13.)
Na katika Yohana asema hivi katika waraka wake wa kwanza: "Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni muaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote" (1 Yoh. 1:8-9).
Baada ya kupokea wokovu, ni lazima tutembee katika mwanga na kutubu kila dhambi ambayo roho mtakatifu anatufichulia (1Yoh. 2:1-2).
Wakristo amabao walikuwa Wakorintho hawakutilia maanani umuhimu wa baadhi ya mambo haya, na hawakuweza kukuwa vyema:
"Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo Naliwanywesha maziwa, sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, kwa maana hata sasaninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, Je! si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?" (1 Kor. 3:1-3, 16).
Usiingie katika maisha ya wokovu huku ukiendelea kubeba mawazo ya uovu, na dhambi ambazo hujatubu. Hii itasababisha imani yako kufifia. Tubu kila dhambi na utapata wokovu. Kristo ametoa malipo yote.
Katika karne ya kwanza ilikuwa ni kuandika kosa la mtu pamoja na hukumu iliyotolewa kwenye karatasi na kuweka karatasi hii katika mlango wa pale ambapo amefungwa. Baada yeye kumaliza kifungo, karatasi ile ilitolewa na badala yake kuandikwa neno hili Tetelestai Yeye aliyefungwa alipewa karatasi hiyo. Ni wazi kila mtu ni mfungwa washetani (soma Warumi 3:23). Kila mmoja wetu ambaye hajampokea Kristo kama mwokozi wake yuko kifungoni, hukumu ya kifo yamngoja. Mwenye kusimamia jela hii ni shetani mwenyewe. Hakuna anayeweza kuepuka hukumu kali hii pasipo kupitia kwa Mwokozi wetu Yesu Kristo.
Ili kutuokoa sisi wanadamu, Kristo alijitoa kufa msalabani (soma Warumi 6:23). Baada ya kufufuka, yeye yu hai, na wakati huu ana uwezo wa kutuondolea - kila mmoja wetu - mashtaka yanayomkabidhi na hapo kutuepusha hukumu ya kifo. Haya twayasoma katika Wakolosai 2:13-14:
"Na ninyi mlipokuwa mumekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushtaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani."
Sawa na vile nabii Isaya anavyosema katika agano la kale, Mwokozi wetu alikuja duniani ili, “kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa" (Isa. 42:7).
Ujumbe huu, kwamba Kristo alikuja kutuokoa sisi wanadamu wenye dhambi watiliwa mkazo pia katika Isaya 61:1: "Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwatibu waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao."
Je, dhambi zako ambazo zatumiwa na mwovu shetani kama mashtaka – dhambi hizi zimeondolewa?
Kama umemkubali Kristo akuondolee dhambi zako, kama Yeye ni mwokozi wa maisha yako, basi hakuna atakayeweza kukushitaki. Hukumu kwa wenye dhambi imeondolewa kabisa.
Neno hili Tetelestai liliwahi kutumiwa kama kielelezo cha ushindi katika vita. Pale jemadari aliporudi mjini Roma akitoka katika vita, yeye aliwaonyesha wenyeji wafungwa wake wakivita akipaaza akisema: Tetelestai... tetelestai... tetelestai! Kwa hiyo, tamshi hili ni la maana kwamba ushindi umepatikana dhidi ya adui.
Pale msalabani, mwokozi wetu Yesu Kristo pia alitumia neno hili Tetelestai. Kifo cha mwokozi wetu Kristo kilikuwa ni kifo cha ushindi ili kupitia kufa kwake, alimshinda adui. Haya twasoma katika Wakolosai 2:15: "Akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo."
Kristo alipata ushindi, na hasa pale msalabani. Hata hivyo, adui bado yuko duniani. Yeye adui bado anaendeleza uovu wake, na hii ndio sababu tunatiwa moyo katika Warumi 8:37: "Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda."
Tumo vitani, la kutia moyo ni kwamba, tayari tuna uhakika kwamba ushindi ni wetu.
Tujitahidi kutumia vyema muda ambao umebaki. Ni bora kutumia muda huu kutangaza neno la Bwana na kueneza injili katika kila pembe za dunia. Muda unaenda kasi sana, na huenda tukakosa wakati wa kufanya yale tunayohitajika kufanya. Sawa na Mwokozi wetu Kristo, inafaa tuseme hivi:
"Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi" (Yoh. 9:4).
Saa ya hukumu inakaribia; dhiki kuu yakaribia pia, na yako mengi ambayo hatujayafanya kabla baragumu haijalia. Waliopotea wanasatahili kuokolewa. Wakristo wenye imani wafaa kuandaliwa mapema kuwa tayari kwa ajili ya yale yalioko mbele yetu. Wakati wa kurudi mwokozi wetu umekaribia sana. Mpe nafasi Mungu akamilishe kazi yake katika roho yako:
"Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa" (Efe. 5:25-27).
Maranatha – Mungu wetu anakuja!