"Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana haya hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado. Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme, kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali" (Mt. 24:6-7).
Siku za dhiki kuu zitakuwa siku za vita, uvamizi wa wadudu waharibifu, na mikasa ya mazingira ya aina mbali mbali. Matokeo yatakuwa kwamba wanadamu watataabika sana. Mali na vitu vingi ambavyo mwanadamu amejenga vitaharabiwa. Idadi kubwa ya wale wanaoaga dunia miili yao itaachwa ioze bila kuzikwa. Uwezo wa kuwahudumia wagonjwa mahospitalini utadidimia. Haya yote yataleta maradhi na uchafuzi wa mazingira, uchafuzi ulio hatari. Hali ya maisha katika sehemu zenye msongamano itazidi kuwa mbaya. Hii itakuwa chanzo cha shida nyingi. Kiasi kikubwa cha mali asili ambacho tayari kimechafuliwa na miyale iitwayo radioactive kitazidi kuharibika zaidi kwa ajili ya mitetemeko ya ardhi, ukame, na joto la jua linalozidi kiwango.
Kutatokea mitetemeko ya ardhi yenye kusababisha uharibifu mkubwa, hata miji mikubwa itaharibiwa kabisa. Nyuma ya haya yote kuna shetani ambaye anapenda kuharibu vyote vilivyo vizuri ambavyo Mungu ameumba. katika muda mfupi wa saa moja, wakati wa enzi fupi ya giza, shetani na wafuasi wake watamwagwa kote duniani kuendeleza uovu wao. Katika kufanya hivyo, kiwango cha uovu kitafikia kilele, na hii ndio italeta kuangamia kwao. La kusikitisha ni kwamba moto wa jehenam ambao umeandaliwa kumuangamiza muovu na malaika wake, moto huu pia utawaangamiza mamilioni ya watu waliodanganywa.
Vita vikali vya shetani vitatokea katika nusu ya pili ya muda ule wa dhiki. Muda huu utaitwa the great tribulation, au dhiki kuu zaidi. Pale mwanzo wa miaka tatu na nusu ya dhiki, muovu atanyimwa ruhusa na kufungiwa njia ya kufikia kiti cha enzi cha ufalme ambapo amekuwa akishtaki waKristo usiku namchana. Twasoma haya katika Ufunuo 12:10. Yeye atashikwa pale kutupwa kutoka mbinguni. Katika muda ule mdogo unaobaki, atatumia uwezo wake wote kuleta kiasi kikubwa sana cha hasara. Mtume Yohana ameandika hivi kuhusu jambo hili:
"Nikasikia sauti kuu mbinguni ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku... Kwa hivyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu" (Ufu. 12:10, 12).
Wakati huu, mpinga Kristo atamuacha farasi mweupe na sasa kuchukua yule mwekundu. Hapo ataanza kuleta fujo, na uharibifu duniani. Na pale miezi 42 ya Ufunuo 13:5-7 itakamilika, uharibifu wa muovu utakuwa umeenea kote duniani. Huku mambo yakiwa yameharibika kabisa, muovu na mwuaji huyu atajitokeza na kukusanya roho zao waliokufa kusudi azipeleke jehenam. Akiwa shetani, na mpinga Kristo atafurahia sana vifo vya watu hawa.
Wakati wa kujadili dhiki kuu, wengi huzungumzia juu ya vita vikuu vitakavyotokea. Katika Ufunuo 6:8 twasoma kwamba vita vya mpinga Kristo, pamoja na maradhi (pestilences) na njaa, vyote vitasababisha vifo vya karibu robo ya watu duniani. Kulingana na hesabu ya hivi sasa, hawa ni watu karibu bilioni moja na nusu ambao wamewahi kufa duniani. Kiasi hiki ni kikubwa sana ambacho kimewahi kutokea. Idadi kubwa ya wale waliowahi kukufa ni millioni 52 ambao walikufa wakati wa vita vikuu vya pili duniani.
Uvamizi wa warusi katika taifa la Israeli ulitabiriwa na Ezekiel miaka 2600 iliopita. Ufafanuzi zaidi umetolewa kuhusu vile Urusi itaungana na Iran, Libya, Ethiopia, Uturuki (Turkey), Ujerumani na nchi mbali mbali zenye nguvu kupigana na taifa la israeli. Sababu kuu ya vita itakuwa ni kuamsha upya sera ya siasa ya kikomunisti, na ile ya Nazi. Vikundi hivi vyote hupinga wayahudi pamoja na wakristo. Katika Ezekieli 38 na 39, yako maelezo kuhusu jinsi vile uwezo wa mfalme wa mbali kaskazini utavunjwa kwenye milima ya Israeli. Ikikumbukwa kwamba Marekani ni nchi rafiki ya Israeli, uvamizi wa muungano wa warusi, waarabu na wajerumani katika taifa la wayahudi waweza kusababisha vita vikuu vya dunia.
Katika Ufunuo 9:13-19 yako maelezo yanayohusu jinsi vile wakuu wa mataifa ya mashariki ya mbali yaani uChina na marafiki wake watakavyoandaa majeshi yao na kuyaweka tayari kwa ajili ya vita wakati wa dhiki kuu. Jeshi la watu 200 million wa asili ya kiAsia watavuka mto Frati na kuingia mashariki ya kati na magharibi na kuwaua watu wengi sana. Katika Ufu. 9:15 twasoma kwamba, nao watawaua theluthi moja (a third) ya idadi ya wale walioko duniani. Uaji huu na uvamizi utaendelea mpaka mwisho wa dhiki kuu wakati ule wa vita vikuu vya Har-Magedoni. Katika Ufunuo 16:12, ambapo kuna utaratibu wa matukio ya mwisho kabla ya vita vya Har-Magedoni kutajwa, kuna usemi kuhusu safari ya kutisha kuelekea mashariki ya kati. Twasoma:
"Na huyo wa sita akamimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua" (Ufu. 16:12).
Ziko ishara mbali mbali kwamba silaha za nuclear huenda zikatumiwa katika vita katika Ufunuo. Mtume Yohana hakuwa na majina ya kitaalam ya kisasa juu ya silaha za karne hii, hata hivyo anagusia mengi yanayohusu vile silaha hatari zitatumiwa. Anasema:
"Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyotangamana na damu, vikatupwa juu ya nchi; theluthi ya nchi ikateteketea, na theluthi ya miti ikateketea, na majani mabichi yote yakateketea. Malaika wa pili akapiga baragumu, na kitu, mfano wa mlima mkubwa uwakao moto, kikatupwa katika bahari; theluthi ya bahari ikawa damu. Wakafa theluthi ya viumbe vilivyomo baharini, vyenye uhai; theluthi ya merikebu zikaharibiwa" (Ufu. 8:7-9).
Baada ya haya, yeye anataja jinsi vile theluthi moja ya maji duniani yatatiwa sumu. Anaonya kwamba watakayoyanywa maji haya watakufa. Hali hii huenda ikasababishwa na miyale kutoka kwamchanga wa maadini yaliyo na uwezo wa kutoa nguvu za umeme yaani radioactive dust. Mchanga huu au uchafu kutoka kwa maadini haya utaanguka kwenye maji. Kulingana na Ufunuo 8:12, Jua, mwezi na nyota havitaonekana. Sababu ya hali hii kutokea ni kwamba kuna uchafuzi mkuu wa mazingira.
Watalaam wa sayansi wanasema kwamba ikiwa vita vya dunia vitaanza, na zana za nuclear zitumiwe, karibu watu bilioni moja wataaga dunia. Wengine bilioni moja wataaga dunia baadaye. Miyale yenye joto jingi kutoka kwa jua itasambaa kote duniani, na hii itawasha moto vitu vyote ambavyo vyaweza kushika moto kwa urahisi. Moto huo utawasha gesi nyingi hatari na kujaza kila sehemu ya dunia na gesi hatari ya carbon monoxide, na hata cyanide.
Baada ya vita ambapo zana za nuclear zitatumiwa, matokeo yatakuwa ya kutisha.Baada ya moto ule wa pale mwanzo, sehemu ya juu ya dunia itapoa kwa haraka. Joto litapunguka hata kwa zaidi ya kipimo cha kupima joto kiwango cha digrii 55, na hapo dunia itakuwa imezingirwa na theluji na maji yaliyogandamana. Hii itaharibu dunia yote hasa majani na mimea. Sehemu za kuweka maji zitaharibiwa. Seehemu ya ya kaskazini duniani itajaa uchafu wa aina aina, ni kwa ajili sehemu hii ndiyo itakuwa imekumbwa sana na milipuko. Jua litafunikwa kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja Mawingu makubwa yataelekea sehemu ya kusini, na hii itafanya dunia ionekane kana kwamba ni wakati wa jioni na jua limepotea kwenda machweyo.
Ufunuo 6:12 inazungumzia wakati huu hivi: "...jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu."
Hali hii itaendelea kuwako mpaka pale Kristo atakaporudi, na hata kuzidi. Na pale mpinga Kristo atakapokuwa amemaliza kazi ya kuharibu ulimwengu, yeye ataweka majeshi yake tayari nchini Israeli. Na hapa majeshi haya yatajiandaa kupigana vita viwili vikuu vya mwisho (Ufu. 16:14-16).
Vita vya kwanza vitakuwa dhidi ya wayahudi, na vya pili dhidi ya Kristo mwenyewe. Mpinga Kristo anajua kwamba Kristo atarudi mara ya pili na jeshi lake kuu la malaika wa mbinguni, na atangoja kurudi kwake pale mlima wa mzeituni. Katika kukabiliana kwao, mpinga Kristo ataleta kujiangamiza mwenyewe, pamoja na kuangamia kwa wafuasi wake wote ambao ni wale ambao wamekubali kuwekewa chapa yake. Mtume Yohana anasema hivi katika Ufunuo:
"Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake. Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti; na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao" (Ufu. 19:19-21).
Na katika kitabu cha Zekaria twasoma hivi: "Na hii ndiyo tauni, ambayo Bwana atawapiga watu wote waliofanya vita juu ya Yerusalemu; nyama ya mwili wao itaharibika, wasimamapo juu ya miguu yao, na macho yao yataharibikia ndani ya vichwa vyao, na ndimi zao zitaharibika ndani ya vinywa vyao" (Zek. 14:12).
Ni wazi kwamba uchafuzi ambao utatokana na vita vya zana hatari za nuclear, na matumizi ya zana za kemikali na kadhalika utasababisha uchafuzi wa hewa na magonjwa ya aina mbali mbali, na hata kuweka aina ya sumu angani na uchafuzi wa hatari sana wa mazingira yetu. Miyale ya silaha za nuclear itasababisha vifo vya watu. Na hata pale kiasi cha miyale hii kitapunguka, matokeo na madhara yake yataendelea kujitokeza. Kiwango cha madhara kitategemea wingi wa watu. na jinsi vile wamesongamana katika makao yao kila mahali duniani. Miyale hii inaweza kusababisha aina mbali mbali ya magonjwa. Inaweza kusababisha maradhi ambayo hayana tiba kama cancer ya ngozi ama cancer ambayo hujitokeza kama uvimbe kwenye sehemu fulani katika tumbo. Kwa wa mama, miyale hii yaweza ikasababisha mabadiliko katika sehemu za mbegu za uzazi na matokeo ni kuzaliwa watoto ambao maumbile yao si ya kawaida.
Na katika mazingira, uchafuzi utakuwa wa hali ya juu sana hivi kwamba mali asili kama maji na mimea itajaa miyale hii iliyo hatari baada ya matumizi ya zana hizi za nuclear. Pale mifugo watakapokula nyasi ilio na sumu ya miyale hii, basi nao pia watadhuriwa hivi kwamba maziwa na nyama ya mifugo haitafa tena kuwa kitoweo. Hata mvua itokayo kwenye mawingu itakuwa na kiasi kikubwa sana cha uchafuzi. Pia mawingu yatabeba uchafu na sumu hii kutoka zana za nuclear na kuelekea sehemu za mbali kutoka kwenye uwanja wa vita hivi na kuchafua sehemu kubwa sana ya ardhi. Wanadamu, wanyama, mifugo na hata mimea itadhuriwa sana na kufa.
Hata wanyama waishio katika ziwa na bahari pia watadhuriwa na sana sana ikiwa kutatokea mlipuko katika bahari jinsi vile tunavyosoma katika Ufunuo 8:8, pia mawimbi yatakayotokea na mvua yatasababisha kuzama kwa meli. Ufunuo 16:3-4 yazungumzia jinsi vile maisha ya aina yote yatakavyoangamizwa, na sehemu zenye chemi chemi ya maji safi kuchafuliwa kiasi kwamba hayawezi kutumiwa na wanadamu tena. Hasara itakayotokea, na taabu; vyote vitapita kifani.
Mwanadamu amejiongezea ujuzi pia ana utaalamu wa kumuwezesha kuanzisha maradhi mengi ya ajabu na kutisha. Mataifa kadhaa ya kiarabu hivi sasa yako katika harakati ya kujenga na kutengeneza aina ya silaha ambazo zaweza kueneza maradhi katika miji na sehemu za adui na kusababisha maradhi kama yale ya kuhara damu (dysentery), kuhara (diarrhoea), na maradhi yale ya anthrax na hata homa kali ya matumbo ambayo huenezwa na chawa Typhus. Zana ambazo ziko na uhai katika asili yake (biological weapons) zaweza kutumiwa kueneza maradhi haya yote kwa urahisi kuliko zile za kemikali. Mataifa mengi katika ulimwengu wa tatu yameonyesha kuwa na hamu na zana hizi zinazoeneza magonjwa.
Maradhi ambayo yatachagua wale kudhuru, hawa nao ni wale waliokubali kuwekewa ile chapa ya mpinga kristo. Maradhi kama haya yatajitokeza sana wakati ule wa dhiki kuu. Mtume Yohana ameandika hivi: "Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na jipu baya, bovu, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake" (Ufu. 16:2).
Maradhi kama ya ukimwi yamekuwa ni maradhi ambayo yanawadhuru watu fulani tuu. Pale mbeleni yalijitokeza sana katika kikundi cha wale makahaba waitwao homosexuals. Wakati wa kujitokeza mara ya kwanza, maradhi haya yalikuwa ni kama aina ya ugonjwa ambao mtume Yohana anataja hapa juu.
Wakati huu, bara la Afrika hasa sehemu ya kusini ya jangwa la Sahara inakumbana na tisho kuu la kuangamizwa na maradhi haya hatari ya ukimwi. Katika ukadiriaji fulani inasemekana kwamba ifikapo mwaka wa 2005, kati ya watu 50% na 70% watakuwa tayari wameambukizwa viini vinavyoleta maradhi haya ya ukimwi katika bara hili la Afrika, idadi ya wanaume walio na viini vya maradhi ni karibu sawa na ile ya wanawake walio na viini vyenyewe. Katika Ulaya na Marekani, maradhi haya yamejitokeza sana kati ya wale ambao ni walawiti (Homosexuals) na wale wanaotumia madawa ya kulevya. Makahaba wengi pia wana maradhi haya.
Mungu anatuonya juu ya uovu kama huu wa ulawiti (homosexuality) na ukahaba. Huenda hii ikawa ndio sababu tiba kamili haijaweza kutengenezwa hata ingawa utafiti wa kisayansi umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu. Mungu anawaonya wanaotenda uovu kwa njia hii na maneno haya: "Au hamjui ya kwamba wadhalimu hawataurithi ufalme ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi" (I Kor. 6:9-10).
Uzinzi, ulawiti na uovu wa aina aina umeorodheshwa hapa. Biblia inaonya kwamba wale wanaotenda uovu huu lazima wataumia katika miili yao kama malipo ya uovu wao. Katika warumi twasoma hivi:
"Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa amtumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke ya asili wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata anafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao" (Rum. 1:26-27).
Katika nyakati za mwisho, sawa na siku zile za Nuhu na Lutu, wako wale watakaojiunga na watenda uovu na hata kujiweka mikononi mwake mpinga Kristo ili wapate pesa. Wakiwa katika hali hii ya uovu, wao watakataa kutubu dhambi zao na kujibadili. Wakati wa dhiki kuu, bado watakataa kutubu kabisa. Maradhi na uchungu uletwao na uvimbe wa aina aina utawasumbua lakini bado watakataa kutubu. Wataendelea kutenda uovu zaidi kupitia vinywa vyao.
"Wanadamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, nao wakalitukana jina la Mungu aliiye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu" (Ufu. 16:9).
Na katika Ufunuo 9, yako maelezo mengi yanayohusu taabu na dhiki itakayowakumba wale watakaonusurika mikasa mbali mbali. tunasoma hivi:
"Na wanadamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo matatu hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizo weza kuona wala kusikia wala kuenenda. Wala hawakuutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala usherati wao, wala wivi wao" (Ufu. 9:20-21).
Mtu yeyote ambaye amechagua kumfuata shetani, nakutenda yale yanayomfurahisha shetani huwa anafuata yale shetani anamtaka afanye tu. Yeye kawaida hukataa ukweli, na hajui yuko njiani kuelekea jehenam.
Kuna dalili kwamba matukio ya kutisha na hasa mikasa sawa na ile inayotajwa katika Biblia inakaribia kutokea. Wataalamu wa mambo ya sayansi wanasema kwamba joto duniani linazidi kupanda. Joto hili litabadili hali ya anga duniani. Hii imetokana na ongezeko la gesi aina ya carbon katika anga. tayari sehemu fulani ya anga inayoitwa ozone imeharibika kabisa. Sehemu hii huwa kinga dhidi ya madhara yanayoweza kutokana na miyale hatari kama ile ya ultra violet kutoka kwa jua. Kuna uwezekano kwamba theluji iliyoko katika sehemu ya kaskazini (polar region) inaweza ikayeyushwa kwa ajili ya joto jingi duniani. Hii yaweza ikasababisha kuongezeka kwa kiasi cha maji katika bahari, na kuleta mafuriko kwenye sehemu za nyanda za chini.
Uchafuzi wa mazingira yetu umekuwa ukiendelea. na kuna aina fulani za gesi ambazo hulea mvua iliyo na kemikali, nayo imeharibu misitu sehemu nyingi duniani. Zaidi ya hayo, mali asili imekuwa ikiharibiwa na uchafu kutoka viwandani na kwingineko, hasa mafuta yanapomwagika kwenye bahari na kadhalika. Pia, pale hali ya anga inapobadilika, mimea hudhuriwa. Hivi sasa, idadi ya watu duniani ikiwa zaidi ya bilioni 6, kuna tisho la njaa. Ni kwa ajili ya vitisho hivi kuliitishwa mkutano wa kimataifa nchini Brazili mwezi Juni mwaka wa 1992 kujadili na kuchunguza kwa makini hali ya mazingira yetu.
Mkasa mmoja ambao hutajwa sana nyakati za mwisho ni ule wa mtetemeko wa ardhi. Kwa vile hivi sasa watu wengi huishi pamoja na karibu karibu hasa kwenye miji zetu, mkasa kama huu waweza kusababisha maafa makubwa. Kuhusu jambo hili Kristo mwenyewe amesema hivi:
"Tena, kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya ya mataifa wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake; watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika. Hapo ndipo watakapomuona mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi" (Lk. 21:25-27).
Kando na tisho la mitetemeko ya ardhi, ziko ishara za vitisho ambazo zitaonekana kutoka mbingu za mbali kuadhiri dunia. Sayari na nyota mbali mbali (Meteors na asteroids) zitaharibu sehemu nyingi duniani. Pale mambo yatakapoharibika kabisa, Kristo atajitokeza na huu ndio wakati wake kurudi mara ya pili. Watenda uovu watatishika kabisa na kujaribu kutoroka kutoka machoni mwake. Yohana anaeleza zaidi katika Ufunuo:
"Nami nikaona, alipoifungua muhuri wa sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepeo mwingi. Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemedari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, wakiiambia milima na miamba, tuangukieni, tusitirini, mbele ya kiti chake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya mwana kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuj; naye ni nani awezaye kusimama?" ( Ufu. 6:12-17).
Ufunuo 16 pia yaeleza zaidi kuhusu jambo hili:
"Na huyo wa saba akamimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa. Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na teteemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa tetemeko hilo. Na mji ule mkuu ukagawanyika na mafungu matatu; na miji yamataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo wa ghadhabu ya hasira yake. Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekena tena. Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno" (Ufu. 16:17-21).
Makuhani wengi wa Agano la kale pia nao wametaja na kuandika mengi sawa na hayo kuhusu siku za mwisho. Kwa upande mmoja, wengi watatatizwa na joto jingi pamoja na ukosefu wa chakula. Kutakuwa na makelele ya kutisha pamoja na mitetemeko ya ardhi. Watenda dhambi ambao hawataki kujibadili watatupwa chini na kuangamizwa na uovu wao. Miili yao italiwa na ndege na wanyama. Nabii Isaya anasema hivi:
"Tazama siku ya Bwana inakuja, siku kali ya hasira na ghadhabu, ili iifanye kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake. Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze. Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini yao walio wakali; nitafanya wanadamu kuadimikia kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya ofiri. Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake, kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana wa majeshi, na kwa sababu ya siku ya hasira yake kali" (Isa. 13:9-13).
Kuna tahadhari ilio sawa na hii pia katika maandishi ya nabii Isaya ambapo tena twasoma hivi:
"Tazama, Bwana ameifanya dunia kuwa tupu, aifanya ukiwa, aipindua, na kuwatawanya wakaao ndani yake. Na itakuwa kama ilivyo hali ya watu, ndivyo itakavyokuwa ghali ya kuhani; kama ilivyo hali ya mtumwa, ndivyo itakavyokuwa hali ya Bwana wake; kama ililvyo hali ya mjakazi, ndivyo itakavyokuwa hali ya bibi yake; kama ilivyo hali yake anunuaye,ndivyo itakavyokuwa hali yake auzaye; kama ilivyo hali yake akopeshaye, ndivyo itakavyokuwa hali ya akopaye; kama ilivyo hali ya atwaaye faida, ndivyo itakavyokuwa hali yake ampaaye faida. Dunia hii itafanywa tupu kabisa, na kuharibiwa kabisa; maana Bwana amenena neno hilo. Dunia inaomboleza, inazimia; ulimwengu unadhoofika, unazimia; watu wakuu wa dunia wanadhoofika. Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele. Ndio sababu laana imeila dunia hii, na hao wanaoikaa wamedhoofika. Tena dunia imetiwa unajisi kwa wat wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele. Ndiyo sababu laana imeila dunia, na hao wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia, ndiyo sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea, watu waliosalia wakawa wachache tu" (Isa. 24:1-6).
Yale mwokozi wetu Kristo aliyoyasema kuhusu siku za mwisho yanakaribiana sana na haya nabii Isaya ambaye alisema: "Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo na dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu na hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. Na kama siku zisingalifupizwa, asingeokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo" (Mat. 24:21-22).
Wakristo wanaonywa na kutakiwa kutilia maanani maonyo haya katika maandishi matakatifu. Kama Nuhu wa Agano la kale, wakristo wanahitajika kujiandaa vilivyo. Kando na kujiandaa, wanahitajika kuwaeleza wenzao walio karibu na hata mbali kuhusu hukumu ya siku za mwisho. Lutu alipatikana kuwa mtu aliyefaa kuepushwa balaa iliyotokea Sodoma na Gomora. Hii ilimfanya Mungu amuokoe. Na kama Lutu hangelitilia maanani maonyo aliyopewa, basi, yeye naye angeangamia.
Ingawa sisi wanadamu siyo viumbe ambavyo ni vya kumkera Mungu, yafaa tuwe macho, na tujiandae vilivyo ili tuwe watu wanaostahili kusimama mbele yake wakati wa hukumu. Maandishi matakatifu yasema hivi:
"Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo; kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima. Basi kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika hayo yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu" (Lk. 21:34-36).
Je, umejiandaa vya kutosha kuepuka hukumu ya Mungu? Wakati wana waisraeli walipotoka utumwani, Misri, wao walijificha chini ya damu ya mwana kondoo. Je wewe umefanya hivyo?