6. Taifa la Israel Katika Dhiki Kuu

Heshima Yarudi Yerusalemu

Watu wengi hufanya makosa pale ambapo hawaangalii na kuchunguza kwa makini yale yanayosemwa kuhusu taifa la Israeli siku za mwisho. Kwa vile hawajui au hawaelewi ni yapi yametajwa kuhusu taifa hili, wao hupata ugumu kuelewa yale Biblia inasema kuhusu dhiki kuu siku za mwisho. Pia mengi ya unabii yanayohusu kuenea (dispensation) kanisa hayaeleweki na wengi. Na lile la muhimu sana ambalo halitiliwi maanani ni kurudishwa kwa Yerusalemu katika taifa la Israeli kuwa makao makuu au mji mkuu  wa taifa hili.

Na kuhusu kurudi kwake Kristo mara ya pili, katika Ufunuo 1:7 twasoma: "Tazama, yuaja na mawingu; kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina."

Haya tuliyosoma yanasema wazi kwamba lazima waIsraei warudi katika taifa lao ili waweze kuchukua uamuzi fulani maalum kuhusu Kristo aliyesulubiwa, na kukataliwa kwa wale waliokuwa wake wakati  yeye alipokuja mara ya kwanza.

Mji wa Yeruslemu ni mji wa muhimu kabisa kwani hii ndio ishara moja kuu mwokozi wetu yesu Kristo alitupa kuhusu mwisho wa kuenea kanisa wakati huu, na mwanzo wa dhiki kuu. Baada ya kueleza kuharibika kwa mji wa Yerusalemu katika Luka 19:41-44 na 21:5-6, yeye alitaja kutawanyika kwa wayahudi kote duniani, kwamba Yerusalemu itakaliwa kimabavu na kuharibiwa na mataifa yasiyo ya kiyahudi:

"Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili. Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na mataifa, hata majira ya mataifa yatakapotimia" (Lk. 21:23-24).

Mtume Paulo anasema wakati huu wa waIsraeli kutawanyika  ni wakati ambapo roho zao zitazidi kuwa ngumu, na kwao wasio na imani kuwa ni wakati wao kupokea kwa wingi ujumbe wa injili. Ugumu katika roho za wayahudi umefikia kiwango ambapo mpaka wale wasio na imani wamepokea. Hata hivyo wote katika taifa la Israeli watapokea wokovu kwa vile imeandikwa katika  Warumi 11:25-26:

"Kwa maana, ndugu zangu sipendi msijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ngumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa mataifa uwasili. Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, mwokozi atakuja kutoka Sayuni; atamtenga Yakobo na maasia yake."

Luka 21:24 haitaji  tuu wakati ule ambapo Yerusalemu haitakuwa mji ulionyanyaswa, bali inazungumzia wakati ambapo kazi ya kuenea kwa kanisa itakuwa imekwisha. Ni jambo la muhimu kuelewa vyema nakujua ni yapi yanatokea katika mji wa Yerusalemu chini ya wayahudi ili kuweza kufahamu vyema yale yanayotajwa kuhusu nyakati za mwisho (Lk. 12:54-56).

Wakati taifa la Israeli lilipopata mamlaka ya kuwa taifa mwaka wa 1948, taifa hili lilipewa madaraka juu ya sehemu ndogo tuu, ambayo ni sehemu mpya ya Yerusalemu. Hii ilikuwa ishara kwamba nyakati za mwisho zilikuwa zinakaribia. Tukio la muhimu sana lilitokea pale mwaka  wa 1967 pale sehemu ya Yerusalemu ambayo ni mji wa kale ambako kuna Zion na Temple Mount, na hata sehemu ya mashariki ya Yerusalemu kuchukuliwa kwa nguvu kutoka Jordan wakati wa vita vikali  vya siku sita (Six-day War.) Hadi wakati huo, tayari Yerusalemu ilikuwa imejengwa upya, na hii ingefuatwa na Yerusalemu kufanywa kuwa makao makuu ya kisiasa katika taifa hili la Israeli. Ni bora kukumbuka hapa kwamba mara ya mwisho Yerusalemu palikuwa ni mahali ambapo ni mji huru ilikuwa ni pale karne ya sita. Pale wakati Kristo alipokuwa hapa duniani, bendera iliyokuwa ikipepea Yerusalemu ilikuwa ni bendera ya  ufalme wa Kirumi.

Mnamo Agosti 1980, Waziri mkuu wa Israeli Menachim Begin alitangaza wazi kwamba Yerusalemu ndio mji mkuu usioweza kugawanywa wa taifa la Israeli, na hapo akahamisha makao yake makuu kutoka Tel-Aviv hadi hapa Yerusalemu. Miaka miwili baadaye, baraza lake lote la mawaziri lilihamia Yerusalemu. Hapa basi Yerusalemu  ukawa mji mpya ambao ni makao makuu ya kisiasa ya taiafa hili la Israeli.

Lile ambalo lazima litokee hapa ni kufufuka kiimani katika Yerusalemu na kujengwa upya kwa hekalu. Hivi sasa, mji huo bado unakaliwa na wageni ambao wako hapo. Jambo kuu ambalo litatokea katika taifa la Israei ni lile linalohusu jinsi kujitokeza kwa wayahudi maalum 144,000 wakati wa dhiki kuu. Hekalu itajengwa upya. Danieli 9:27 na 11:31 na Mathayo 24:15 na 2 Thessalonika 2:4 na mwisho Ufunuo 11:1-2 hapa twasoma jinsi vile hekalu itajengwa upya. Unabii wa mtume Yohana katika Ufunuo 11 uliandikwa baada ya hekalu iliyotangulia kuharibiwa mwaka wa 70 AD. Kwa hivyo yale mtume Yohana anataja hapa katika Ufunuo lazima yawe ni yale yatakayotokea baadaye.

Waliobaki katika taifa la Israeli  baada ya dhiki kuu watafufuka kiroho pale mwokozi wetu Yesu Kristo atakapojitokeza kwenye mlima wa mizeituni atakaporudi mara ya pili: "Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa mizeituni, unaolekea Yerusalemu upande wa Mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini" (Zek.14:4).

Watu wengi wanangoja siku hii kwa hamu. Wakati mmoja aliyekuwa meya wa Yerusalemu Teddy Kollek alisema kwamba ni yeye aliyekuwa na kazi kubwa sana ya umeya duniani, yaani kuanda mji huo kumpokea masihi.

Kufufuka Kiroho Katika Taifa la Israeli.

Wiki Moja ya  Dhiki

Katika taifa la kiyahudi Israeli, wana mtindo wa kuhesabu ambapo nambari saba inatumika sana. Kwa mfano baada ya siku saba, hii ni wiki moja, baada ya miaka sita, mwaka wa saba ni mwaka maalum, mwaka wa sabato, na baada ya  miaka   saba mara saba, mwaka wa  hamsini (jubilee) huwa ni mwaka  maalum wa sherehe. Soma Walawi 25:1-10. Na kwa vile dhiki kuu na kudumu kwa muda wa  miaka saba, jinsi vile tunasoma katika Dan 9:27, kuna umuhimu wa kutilia maanani sana jinsi vile wayahudi huhesabu siku na miaka yao.

Mwaka wa mwisho kabla ya mwaka maalum wa hamsini unaotangulia kurudi kwa Masihi utakuwa wakati wa majaribu mengi na msisimko wa kiroho katika taifa la wayahudi. Taifa hili bado limefunikwa macho, na mengi yatalikumba  wakati wa miaka ile saba ya dhiki (soma Yer. 30:7; Dan. 9:27; Eze. 22:19-21; Zek.13:8-9). Baada ya muda huu wa taabu na kujibadili, taifa la Wayahudi litaingia kwenye utaratibu maalum wa taifa kuu la wateule ambao wataokoloewa kutoka kwa maafa ya dhiki kuu. Kutakuwa na muamko wa kiroho katika  taifa hili  baada ya miaka hiyo saba.

Ni kutokana na jinsi wayahudi wanahesabu miaka na siku ndipo tunapata uhakika kwamba kweli dhiki kuu itachukua miaka saba. Hata Danieli anataja haya katika Dan. 9:27. Miaka ya mwisho ya dhiki hii itachukua miezi 42 ambayo ni sawa na siku 1260. Kwa hivyo, tunaweza kusema haya:

·      Kutakuwa na watumishi wa Mungu maalum wawili ambao watafanya kazi ya Bwana kwa muda wa siku 1260 wakati wa dhiki kuu (soma Ufu.11:3).

·      Hekalu kuu ya Yerusalemu itaharibiwa na kuchafuliwa kwa muda wa miezi 42 (soma Ufu.11:2).

·      Mwanamke, yaani Wayahudi waisraeli watakimbilia jangwani ambapo watawindwa, lakini hapa watakuwa chini ya utunzi wake Mungu kwa muda wa siku 1260 (soma Ufu.12:6).

·      Mpinga Kristo atakuwa na uwezo na mamlaka makubwa kwa muda wa miezi 42 (Ufu.13:5).

Wateule 144,000

Tukio la muhimu sana wakati wa mwanzo wa dhiki kuu ni ufufuo  kiroho utakaotokea kati ya wayahudi. Ufu. 7:4 yasema wazi kwamba kutakuwa na watenda kazi na  watumishi wa 144,000 kutoka taifa la Israeli ambao watakuwa na muhuri kwenye vichwa vyao: "Na nikasikia nambari ya wale waliokuwa na mihuri: 144,000 ya makabila yote ya Israeli walikuwa na mihuri" (Ufu. 7:4).

Hakuna lile ambalo halieleweki kuhusu haya ambayo tumesoma hapa juu. Ni kosa kusema kwamba ufufuo wa kiroho unaotajwa katika Ufunuo 7:1-8 utaletwa na kanisa au kikundi fulani maalum. Somo hili lagusia taifa la Israeli. Wakati huu, Mungu atakuwa tayari amewaondoa wale walio na imani halisi kutoka hapa duniani. Atawafufua wayahudi 144,000 kati ya wale ambao wamerudishiwa imani yao, au wamerudia Mungu na kupokea wokovu ili wawe mashahidi wake. Ufunuo 7 yakubaliana na maneno ya unabii katika biblia ambapo kuna hakikisho kwamba Mungu hatafufua tu taifa la Israeli na kuwarudisha hapa  duniani, ila  katika siku za baadaye watafufuka kiroho.

"Kwa hiyo waambieni nyumba ya Israeli, Bwana Mungu asema hivi: sitendi hili kwa ajili yenu, Ee nyumba ya Israeli, bali kwa ajili ya jina langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi kati kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndiye Bwana, asema Bwana Mungu, nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao maana nitawatwaa kati ya mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe. Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi, nitawatakaseni uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi  roho mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu. Nami nitatoa moyo wa jiwe iliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu" (Ezek. 36:22-28).

Leo hii kuna wayahudi wengi sana ambao wamepokea ujumbe wa Agano Jipya unaohusu mwokozi wetu Yesu Kristo. Hata hivyo wengi wao  hawataki kuamua mara moja kumtambua kristo kuwa mwokozi na wanafanya hivyo kwa ajili ya hofu kwamba huenda wakateswa na kupata taabu au kwa ajili ya kutojua ni nini kitatokea pale wanapopokea wokovu. Uamuzi utachukuliwa baada ya kunyakuliwa kwa wale walio na imani na wale wayahudi wateule ambao tayari wamemkubali Kristo wamenyakuliwa pamoja na kanisa lote la Kristo. Wale watakaoachwa itawabidii wafikirie kwa makini kuhusu uamuzi wao utakaochelewa.

Kwa ajili ya matukio haya yote, idadi kubwa ya wayahudi kote duniani watanyenyekea na kutubu dhambi zao wakiongozwa na roho mtakatifu na hapo kukubali kwamba Kristo ndiye Masihi. Tunasoma katika Ufunuo 7:3 kwamba Mungu atawachukua wateule wake 144,000 ambao ni watumishi wake waliowekewa muhuri pale mwanzo wa dhiki kuu, na yeye. Wale walioachwa nyuma itawabidi wachunguze upya  msimamo wao.

Mkuu wa Uovu Ajitokeza

Pale waIsraeli wanapobadili nia na kwanza kuwa tayari kupokea wokovu, muovu hatachelewa kuchukua nafasi hii ili kujitoa wazi na kazi yake akiwa  masihi wa uongo. Baada ya kunyakuliwa wale walio na imani, hofu kuu na wasi wasi itakumba taifa lote la Israeli. Hali hii  itazidishwa na vita pale Israeli itakaposhambuliwa na jeshi ambalo ni muungano wa mataifa adui wa jadi. Twasoma haya katika Ezekieli 38 na 39. Kwa njia ya miujiza kabisa, Mungu atajitokeza na kuwaokoa waIsraeli kwa njia ya ajabu. Yeye atawaangamiza maadui wao.

Na hapo hapo pia muyahudi mmoja atajitokeza na kuanza kufanya maajabu. Yeye atapokea shukrani na sifa kimakosa kwani wengi wataamini kwamba yale Mungu amefanya kuokoa taifa la Israeli, yamefanyika kwa ajili  ya uwezo wake.

Atajitokeza na kusema kwamba ni yeye mwokozi wa Wayahudi, na kwamba ni yeye amewaokoa waIsraeli, na kwamba ni kutokana na uwezo wake taifa hili limeepuka bala kuu. Yeye atasema kwamba ndiye Masihi baada ya majadiliano na mikutano viongozi wa taifa watamkubali kuwa ni yeye Masihi. Mwokozi wetu Yesu Kristo anasema hivi kuhusu jambo hili: "Nimekuja kwa jina la Baba, na hamjanipokea, naye yule anayekuja kwa jina lake mwenyewe,  enyi mumemupokea" (Yoh. 5:43).

Huyu muongo ambaye atajaribu kumuiga Masihi na kujaribu kuchukua mahali pake, ndiye yule ambaye anakuja akiwa amepanda farasi mweupe na ni yeye mpinga Kristo. Naye hatakawia kujitengenezea makao yake akiwa kiongozi, na atawapa ruhusa waIsraeli wajengee upya hekalu. Yeye atafanyia mzaha wokovu ule wale Wayahudi 144,000 wamepokea na kusema kwamba msingi wa imani ya hawa 144,000 ni msingi wa uovu ulio kinyume cha mapenzi ya Mungu. Na akiwa kinyume na mapenzi ya Bwana kuhusu ufufuo wa kiroho, yeye ataelekeza yote yaliyo ya kiroho kwenye njia ya zamani (orthodox) ambayo itahusu kujenga upya hekalu na mwanzo mpya wa matumizi ya sherehe  na kafara mbaya.

Kwa ajili ya sababu zilizo wazi hapa, wale wayahudi ambao wamepokea wokovu wa kweli watakosa kusikilizana na hawa ambao msingi wao ni huyu masiya wa uongo ambaye amejitokeza. Hawa wafuasi wa masihi muongo ndio watakuwa wengi. Hata pale atakapojitokeza na kwenda katika mataifa mbali mbali akijifanya kuwa masiya, na hapo kuanzisha  muungano wa kidini, wengi bado kwa ajili ya kutojua wataungana naye na kumfuata, na kushiriki naye katika uovu wake.

Mashahidi Wawili

Wakati huu ambapo kutakuwa na harakati kubwa sana za kuwapotosha waIsraeli, Mungu atawatuma mashahidi wawili ili kueleza taifa la Israeli kwamba ni jambo la muhimu wao kurudi kwake Mungu wa kweli. Tunasoma haya katika Ufunuo 11:3-12. Kuna dalili katika maandishi matakatifu kwamba huenda hawa wawili wakawa Musa na Eliya ambao walionekaa na Kristo katika mlima a jinsi vile tunavyosoma katika Mathayo 17:1-3. Na kuhusu Eliya, katika mistari miwili ya mwisho wa Agano la Kale twasoma hivi:

"Angalieni, nitawapekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya Baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana" (Mal. 4: 5-6).

Malkia wa Amani Abadilika na Kuwa Fidhuli

Pale muda wa dhiki kuu utakapofikia kati kati, makubaliano kati ya waIsraeli na Masihi huyu wa uongo yatavunjika pale yeye atakapojitangaza kwamba ni yeye Mungu katika hekalu. Haya twasoma katika 2 The. 2:4 hivi:

"Yule pingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu."

Akisaidiwa na  yule nabii wa uongo, yeye atajenga na kutengeneza picha yake katika sehemu takatifu zaidi ya yote katika hekalu, na kulazimisha kila mtu kumuabudu. Yeye atatupilia mbali kila aina ya maombi katika hekalu hata ule mtindo maalum wa kuomba ambao zawadi hutolewa kwa Mungu. Danieli anasema hivi :

"Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo atakomesha sadaka na  dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo hata ukoma, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa  juu yake mwenye kuharibu" (Dan. 9:27).

Kwa hivyo, Danieli anasema wazi kwamba huyu mpinga Kristo atatupilia mbali utaratibu wa maombi ulioko na hata ule ambapo dhabihu hutumiwa katika hekalu baada ya miaka tatu na nusu ya utawala wake.

Taifa lililo huzunika la Israeli litakataa kuendelea kumfuata huyu masihi wa uongo. Taifa la Israeli ambalo limekasirishwa na huyu masihi wa uongo litakataa kumtii huyu ambaye sasa atakuwa amejitangaza kuwa Mungu. Na kwa ajili ya kufanya hivyo, wao watamkasirisha huyu masihi wa uongo, naye atataka kukumbana nao na kuwaadhibu. Yeye akiwa kama mungu atakuwa sawa na yule anayebebwa na yule farasi mwekundu. Yeye atajitoa kupigana vita na kuangamiza taifa la Israeli na wote wale ambao si watiifu  kwake na hawafuati mienendo yake. Yeye atawaua mashahidi wawili ambao wamejitokeza na kuonya watu kuhusu uovu wake (twasoma haya katika Ufunuo 11:7). Pia yeye ataamuru wote walio na imani katika Kristo wauawe. Kwa njia ya wazi kabisa, Kristo aliwaonya wayahudi kuhusu taabu itakayoletwa na huyu mpinga Kristo. Tunasoma hivi katika Mathayo:

"Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, imesimama katikl patakatifu (asomaye na afahamu) ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani; naye aliye juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake; wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake. Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo! Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. Na kama siku hizo zisingalifupizwa asingeokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo" (Mt. 24:15-22).

Wakati huu wa dhiki kuu, Wayahudi wengi sana watauawa. Kuhusu jambo hili, Zekaria anasema: "Hata, itakuwa ya kwamba katika nchi yote mafungu mawili yatakataliwa mbali. Nao watakufa, asema Bwana; lakini fungu la tatu litabaki humo" (Zek. 13:8).

Robo tatu itakayobaki itasafishwa na shida zile za dhiki, na pale Kristo atakaporudi, kutakuwa na makubaliano naye jinsi vile tunavyosoma katika Zekaria 13:9: "Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha katika moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwayo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawaasikia; mimi nitasema, watu hawa ndio wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu."

Kukimbilia Jangwani

Katika Ufunuo 12, tunaelezwa jinsi vile waIsraeli watakimbilia jangwani. Hii itatokea pale baada ya hekalu kuchafuliwa, na kutupiliwa mbali kwa makubaliano kati ya  taifa la Israeli na Masihi huyu muongo. Hili ni tukio ambalo litatokea pale katikati ya muda ule wa dhiki kuu.

Katika Ufunuo 12, ugomvi mkuu kati ya waIsraeli na yule mpinga Kristo unazungumziwa kwa njia maalum, na hii itakuwa kati ya Ufalme wa Mungu na ule wa shetani. Yohana  anasema hivi kuhusu vita:

"Na ishara kuu ilionekana mbinguni, mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili. Naye alikuwa na mimba, akilia, hali ana uchungu na kuumwa katika kuzaa. Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake, vilemba saba. Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili, azaapo, amle mtoto wake. Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakyewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na  kwa kiti chake cha enzi. Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na mungu, ili wamlishe huko  muda wa siku elfu na mia mbili sitini" (Ufu. 12:1-6).

Hapa taifa la Israeli lachukuliwa kuwa sawa na  mama aliyeolewa, sio kama mchumba bikira kama vile kanisa la Kristo lilivyo (soma Yer. 31:1-5; Isa. 54:4-8; Hos. 2:15; Mat. 25:1-13; na 2 Kor. 11:2). Huu mwanamke anatajwa pia na kusemekana kuwa atakuwa na nyota kumi na mbili katika kichwa chake, na hii ni alama ya makabila kumi na mbili ya Israeli, pamoja na jua na mwezi ambavyo vimemlenga Yakobo na Raheli kama ni wao watu wa kwanza katika taifa la Israeli. Haya yote yanaweza kulinganishwa na yale yaliyo katika ndoto ya Yusufu katika Mwanzo ambapo tunasoma hivi:

"Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akasema, angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia. Akawambia baba yake na ndugu zake; baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je! mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie hata nchi?" (Mwa. 37:9-10; soma pia Yer. 31:11 na 15 ambapo Yakobo na Raheli wachukuliwa kuwa  kama taifa la Israeli).

Mimba ile ya mama huyu yaweza kuchukuliwa kumaanisha wakati ule wa kuzaliwa Kristo. Yule mnyama ambaye anajiweka tayari kumla mtoto anapozaliwa bila shaka ni muovu shetani mwenyewe. Wakati huu, mfalme muovu ni yule Herode. Ni yeye aliamua kwamba watoto wote wakiume wauliwe ili  mwokozi wetu Yesu Kristo auliwe. Hata hivyo Mungu alikuja na kutenda kazi ya ajabu hapa duniani pale alipofanya kazi yake kuu na kurudi mbinguni  kwake baba yetu aliye juu. Muda wake ule wa kutawala na nguvu kabisa utaanza pale atakaporudi mara ya pili. Twambiwa wazi kwamba wafuasi wake watatwala naye. Haya twayasoma katika Ufunuo 2:26-27. Mpaka pale Kristo atakapokuja tena, muovu shetani anaelekeza nguvu zake zote kujaribu kupinga ufalme wa Mungu, taifa la Israeli na kanisa.

Baada ya kanisa la la kweli kunyakuliwa, yeye sasa ataelekeza nguvu zake kwa taifa la Israeli, kwanza kuhadaa, na baadaye kuangamiza taifa la Israeli ili mpango wa Mungu utimizwe. Ni wakati huu taifa la Israeli litaamriwa kukimbilia jangwani, labda kukimbilia Petra ili kuepuka dhiki kuu. Huko Mungu atawalinda kwa muda wa  siku 1260, ambazo ni kama  miaka tatu na nusu.

Wakristo Wanaokufa kwa ajili ya Imani

Mpinga Kristo atawatesa wakristo wakati huu wa dhiki kuu. Wao wakristo watakuwa hawafuati mambo yake. Hawatatii amri zake ila watendelea kuomba Mungu wa kweli wa taifa la Israeli kupitia Masihi Yesu kristo. Kwa ajili hii, wakristo wana uhusiano wa karibu na mwanamke Israeli (Ufu. 12:17). Katika Warumi 11:15-20. Paulo anasema wakristo kutoka mataifa yasiyo ya kiyahudi wamefanywa kuwa sehemu ya mti wa mzeituni  kwa hivyo, wana uhusiano wa karibu sana nao. Uhusiano huu ndio msingi wa mapenzi tuliyonayo kwa watu wa taifa la Israeli. Ombi letu ni kwamba  wayahudi kutoka taifa la Israeli nao pia watamtambua Kristo kuwa mwokozi na kuingia katika mapatano naye (Heb. 8: 8-13).

Wakristo wa kweli watatambua mara moja kwamba mpinga Kristo ni kiongozi wa uwongo. Wao watamkataa, pia watakataa kanisa lile la dunia atakaloanzisha. Kwao, katika milki hii ya mnyama (the beast), kuna njia moja tuu, nayo ni ile  ya mateso na kufa kwa ajili ya imani.  Kuhusu  hawa watakaokufa kwa ajili ya imani yao, Yohana anasema hivi:

"Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutohukumu, wala kuipatia  haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?" (Ufu. 6:9-10).

Kati ya hawa watakaokufa kwa ajili ya imani, watakuwa wale ambao wamekubali wokovu baada ya huduma kanisani kupitia kazi ya wayahudi 144,000, kutakuwa a wakristo kama hawa wengi. Wao watajitoa kumpinga Kristo, na kuichua uongo wake.

Ikiwa wakati huu utakupata, jua kwamba wokovu wako hautahusika na kumpinga muovu, na kukataa chapa yake, lakii haya yote yatategemea sana kumkubali Kristo. Lazima utubu dhambi zako, mkubali Kristo awe Bwana wa maisha yako, na usafishwe na damu yake. Ni kupitia haya utakuwa umejiandaa vyema kumpinga huyu muovu, hata kama msimamo wako huu wa upinzani waweza kukufanya upoteze maisha yako. Lazima uwe tayari kufa kwa ajili ya imani yako. Sababu ni kwamba waKristo hawatapona dhiki kuu:

"Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado mda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao" (Ufu. 6:11).

Watakapofika mbinguni, hawa waliokufa kwa ajili ya imani yao watapewa mwili wa kufufuka, nao watakuwa na furaha kuu pamoja na Mungu. Hawatakumbuka shida na machozi ya mateso, njaa, na vifo kwa ajili ya imani. Kuhusu  watakaofufuka, Yohana anasema:

"Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila na jamaa, na lugha wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya mwana kondoo wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya  mitende mikononi mwao… Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya mwanakondoo… Kwa maana huyo Mwana kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemi chemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao" (Ufu. 7: 9, 14, 17).

Mkutano katika Mlima wa Mizeituni

Kristo ataonekana mara ya pili hapa duniani jinsi vile imeelezwa katika Ufu. 19, na hii itakuwa pale katika mlima wa mizeituni. Twasoma hivi:

"Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini. Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la milima yangu; kwa maana bonde lile la milima litaenea hata Aseli; naam, mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku za Uzia, mfalme wa Yuda; na Bwana, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye" (Zek. 14:4-5).

Mwokozi wetu Kristo atakuja tena pamoja na watakatifu ambao walikuwa wameungana naye kwa muda wa miaka saba iliotangulia. Sasa anakuja kuleta makubaliano (reconciled) na wale waliobaki taifa la Israeli ambao wakati wa vita vya Har-Magedoni, walikimbilia  usalama katika sehemu zilizo na mawe kwenye mlima wa mizeituni. Mkutano huu utakuwa kwa ajili ya kuwapa wokovu.

"Katika siku hiyo watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, watafunguliwa chemchemi kwa dhambi na kwa unajisi" (Zek. 13:1).

Pale wayahudi ambao wamepona wanapotaja alama za misumari mkononi na kuuliza: "Na mtu atamwambia, Je! jeraha hizi uizo nazo kati ya mkono yako ni nini? naye atajibu, Ni jeraha nilizotiwa katika nyumba ya rafiki zangu" (Zek. 13:6).

Huu utakuwa wakati mgumu kwani wayahudi watajuta kwa ajli ya kutenda dhambi, na pia kwa ajili mababu zao walimkataa masihi wakati yeye kuja mara ya kwanza. Tunasoma hivi katika Zekaria:

"Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamuombolezea, kama vile mtu amuombolezeaye mwanawe wa pekee; nao wataona  uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza. Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya  Haddarimoni katika bonde la Megido" (Zek. 12:10-11).

Kristo ataunganishwa na wale aliosafishwa, wanaokimbia na wenye huzuni, naye atawatia moyo na maneno haya: "Nami nitaleta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwayo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliita jina langu,nami nitawasikia; mimi nitasema, watu hawa ndio wangu; nao watasema, Bwana ndiye Mungu wangu" (Zek. 13:9).