5. Babeli Yafufuka

Tukio ambalo lahusiana kwa karibu sana na dhiki kuu ni lile la kujengwa upya kwa mji wa Babeli kwenye ufuo wa mto Frati. Pakiwa mahali ambapo dini za uongo zilikuwa na makao makuu, ni jambo la kutarajiwa kwamba sharti mji huu ujitokeze tena upya. Mji huu lazima ujitokeze upya kuwa makao maalum ya dini ya uovu ya dunia yote. Babeli hivi leo inapatikana katika taifa la Iraq. Tangu mwaka wa 1978, Babeli imekuwa ikijengwa upya. Sehemu ya kwanza ya mji mpya ilifunguliwa kati ya September 22 na October 22, 1987. Sherehe ya kujengwa upya mji huu imekuwa ikiandaliwa na kufanyika kila  mwaka. Magazeti na vyombo vya habari huzungumzia hil na kulichukuwa kuwa ni  tukio maalum la kitamaduni.

Katika sehemu ya kwanza ya ujenzi wa mji huu wa zamani ni Kasr kuu la mfalme Nebukadreza. Sehemu moja ya Kasr hii ni chumba maalum ambako maandishi yalijitokeza katika ukuta siku ya mwisho ya utawala wa Belshaza. Kati ya vyumba vipya ambavyo vimejengwa ni mlango unaoingia katika hekalu la Ishtar. Hoteli na makao ya watalii yamejengwa katika vitongoji vya mji huu.

Kwa ajili ya kuelewa vyema matukio katika Babeli, lazima tuangalie na tuelewe jinsi vile mji huu ulivyojitokeza, na shughuli za  hapa za kupinga Mungu tangu hapo mbeleni. Katika Mwanzo 10:8-10, Nimrodi alianza kujenga ufalme wake Babeli. Kando na kuwa mji mkuu wa kisiasa, ulikuwa pia mji mkuu wa dini mbaya (pagan religions). Ni kutoka hapa dini hii ilienea kote duniani.

Akiwa mtu anayeamini kwamba binadamu anajiweza, Nimrodi alijitokeza kupinga Mungu. Nimrodi alijichukua kuwa  kando na mfalme, kwamba yeye ni Mungu. Ni yeye pia alijenga mji maalum uliozungukwa (fortified) Shinar. Jina hili  lilikuwa  ni jina la hapo awali la Babeli. Nimrodi alipewa heshima sana akiwa kama Mungu wa nguvu (forces).  Aliitwa mkombozi na mwenye taji, na yeye alichukuliwa kuwa kama Mungu wa jua (Sun god), na kwamba yuko hai. Yaani maana hapa ni kwamba ni yeye anayeleta mwanga na pia uhai. Wafalme wa Babeli na Ashuru walitoa nguvu zao na hata utukufu wao kutoka kwake. Utaratibu huu pia uliigwa na watawala wa kirumi na wengine. Utaratibu huu usio wa imani utajitokeza wakati wa dhiki kuu ambapo mpinga Kristo atajitokeza akajiita Mungu, na kutaka wanadamu wote wamshujudu.

Utaratibu wa Maombi

Tangu hapo mwanzo wake, Babeli imekuwa makao makuu na pia kama alama au ishara (symbol) ya uweza mkubwa duniani unaopinga Mungu. Mtindo na utaratibu huu pia unaapatikana katika jina Babeli ambalo maana yake ni Mlango wa Kuingia kwa Mungu (Gateway to the gods). Baada ya watu kutawanyika na kuwa na lugha mbali mbali, pale katika mnara wa Babeli, jinsi vile tunavyosoma katika kitabu cha Mwanzo 11: Babeli imehusishwa na utengamano, mafarakano na hali ya kutoelewana  kati ya wanadamu. Mlango unaoelekea kwa miungu ulikuwa ni kilele cha hekalu (ziggurat), ambapo makuhani (priests) walipanda juu kuonana na Mungu. Huko walikutana na kuwa kama kitu kimoja na  anga (cosmic) na huko waliweza kusoma nyota na kueleza mambo fulani fulani yanayohusu maisha ya wanadamu wakitumia misingi hii yakusoma nyota.

Mnara wa Babeli ulikuwa ni sehemu moja ya jengo ambalo lilikuwa ni hekalu ya Marduk. Ulikuwa na sehemu nane ambazo zilikuwa zimejengwa moja juu ya nyingine. Katika kilele chake, kulikuwa na hekalu ndogo iliokuwa na viti maalum na meza ya dhahabu. Marduk ndiye alikuwa “mungu” wa mji mkuu. Akiwa “mungu” mkuu, Marduk aliitwa mfalme wa mbingu na dunia. Jina la Mungu yaani God katika  lugha ya Chaldee ni Bel. Na hii ndio sababu Marduk pia huitwa Bel ama Baali katika lugha fulani (soma Yer. 50:2; Isa. 46:1). Ni kutokana na jina hili tuna mnara wa Baali au Bel.

Jina hili Baali ambalo maana yake ni “mungu” (Lord), “mungu mlinzi” au “mwenye vyote” lilitumiwa wakati wa kumtaja mungu tofauti hivi kwamba kulikuwa na Baal-Peori ambaye kama huyu ni Mungu wa mlima Peori. Kwa hivyo, Baali alikuwa Mungu waa Babeli. Aliyemfuata kwa ukuu ni Ishtar ambaye wakati fulani huitwa Astaroth, au ashtoreth au Astarte  yaani mashtorethi. katika wingi, majina haya yotee ya na maana ya “mungu wa kike.” Ni kwa ajili hii Biblia wakati fulani hutaja Baali wengi kama maBaali au Maashtorethi. (Soma Amu. 2:13 na 10: 6).

Ishtar alikuwa na madaraka makubwa sana katika imani za watu wa Babeli na Ashuru. Mahekalu, na sehemu za wazi za maombi zilijengwa kwa ajili yake katika miji mikuu na miji midogo. Yeye pia aliitwa malkia wa Mbinguni (soma Yer. 7:18, 44:19), na pia alichukuliwa kuwa mwana wa kike wa Mungu wa Mwezi (moon god) aitwaye dhambi (Sin)  Alama zake ni mwezi unaokuwa (crescent moon), nyota ya asubuhi (morning star) na nyota ya jioni (star of passionate love.) Akiwa mungu ambaye ni mama, sawa na wa mama wa kawaida, yeye aliweza kuonyesha masikitiko na huzuni, na pia kuwa mwenye huruma. Alielekeza huruma hii kwa watoto wake, na hasa wale walio na taabu. Walio na taabu inayotokana na magonjwa na mikasa mbali mbali. Sherehe za kishetani za kuponya magonjwa zilifanywa kwa kutumia jina lake. Pia ni yeye alikuwa mungu wa kuwasaidia watu kupata watoto na pia  mapenzi.

Tamaa na usherati ilikuwa mila kuu katika shughuli zake zote, na hata  mahekalu yalijengwa kwa ajili ya maombi  kwake. Hekalu lake lilikuwa kama makao makuu ya  usherati. Kwa kumtumikia Ishtar, kina mama wengi walitupilia mbali sana hali yao ya usafi kimwili (chastity), na kuwa makahaba katika hekalu hizi.

Kwao haya hayakuwa makosa ila  njia moja ya kujitoa kumtumikia huyu mungu wao Ishtar. Kwa hivyo, wale waliokuwa makahaba  katika hekalu hizi za Ishtar, wao walizidi kuheshimiwa. Pia Ishtar alikuwa Mungu wa Ashuru wa vita (goddess of war). Yeye aliogopewa sana hivi kwamba maadui wa wa Ashuru walitetemeka pale waliposikia  nyimbo za kumsifu huyu Ishtar.

Katika Babeli ambayo imejengwa upya, mlango wa Ishtar umetengenezwa na watu wanautumia kupita na kuelekea katika chumba cha mfalme katika kasr hili. Ikiwa wafuasi halisi wa Ishtar watajitokeza upya Babeli, maisha yasio na imani (idolatry), usherati na vita vikuu vitajitokeza tena sehemu hiyo duniani. Katika hadithi moja huko Babeli, Ishtar alimuua mpenzi wake Tammuz. Kwa ajili ya kitendo hiki, yeye alishikwa na huzuni na hapo akashuka katika sehemu ya wafu na kumpata huko huyu Tammuz na kumfufua.

Kwa hivyo, Tammuz ni ishara au alama ya kifo na kufufuka. Chombo chenye mfano wa Tammuz hutumika sana katika mila nyingi za wale wasio na imani ana hasa katika mavazi na hata kwenye majengo. Katika hadithi fulani, Tammuz huchukuliwa kuwa mtoto wa kiume wa Semiramis ambaye naye huaminika  kuwa  kiumbe kama mwanadamu ambacho ni malkia wa mbinguni (Queen of heaven).

Katika mwaka wa 381 AD Mariamu alichukuliwa kuwa mama aliye muhimu sana na hii ilikuwa njia moja ya kujaribu kumufanya mungu aliye mbinguni awe kama kiumbe ambacho kina mtoto.

Mungu aliyejulikana sana katika katika Ashuru-Babeli ni Shamash ambaye alikuwa mungu wa jua (Sun god). Yeye alichukia sana giza na dhambi.Waliomuamini  walimchukuwa kuwa ni yeye anayetoa l na kupeana amri zinazo faa. Ni yeye alikuwa mkuu wa makuhani (diviners) wa Babeli. Vikundi vya wale walio na imani na kuomba mungu wa jua vilienea sana katika mataifa mbali mbali na bado vinajitokeza hata wa leo. Alama ya mungu wa jua imejitokeza katika dini iitwayo mormon. Katika kikundi cha watu wenye imani iitwayo New Age Movement, jua na  miyale yake ni alama inayotumiwa sana.

Babeli Yafifia

Utabiri unaohusu kufifia taifa na mji wa Babeli ulitolewa na kutimizwa sawa na jinsi vile ilivyotabiriwa katika maandishi matakatifu. Kwa mfano, tunasoma hivi katika Isaya:

"Na Babeli huo utukufu falme, uzuri wa kiburi cha wakalidayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo Mungu alipoiangamiza. Hautakaliwa na watu tena kabisa, wala watu hawatakAa ndani yake  tangu kizazi hadi kizazi. Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi ayao huko" (Isa. 13:19-20).

Naye Yeremia ana maelezo haya kuhusu kuharibiwa Babeli kwa: "Wala hawatatwaa kwako jiwe moja liwe la pembeni, wala jiwe moja liwe msingi; bali wewe utakuwa ukiwa ukiwa daima asema Bwana" (Yer. 51:26).

Mwandishi Dr. J.A. Seiss mwaka wa 1865 katika Letters on the Apocalypse alisema mji wa Babeli utajengwa upya, ili Mungu aweze kuuharibu jinsi vile alivyoharibu Sodoma na Gomora, na hapo usiweze kuwa na uhai wowote wala mtu yeyote kuweza kuishi hapo tena. Ni wazi kwamba hili litakuwa ni tukio la mwsho wa dunia ambalo kulingana na Isaya 13:6 litatokea wakati wa kuja kwake mwokozi wetu Yesu Kristo (The Day of the Lord), na huenda tukio hili likaambatana ama likatokea wakati mmoja na vita vile vikuu vya Har – Magedoni, pale mwisho wa dhiki kuu.

Mnamo mwaka wa 1918, mwandishi Clarence Larkin katika kitabu chake Dispensational Truth, alisema kwamba Babeli haikuharibiwa kabisa, au hata kukosa kabisa uhai. Kwa hivyo utabiri wa Yeremia kwamba baada ya Babeli kuharibiwa hakuna kitakachobaki wala hata jiwe pekee; nilazima utabiri huu utimizwe. Miji ya kawaida na miji mikuu tayari imejengwa kutoka kwa mabaki ya Babeli. Kabla Babeli haijaanza kujengwa upya  katika mwaka wa  1978, maelfu ya mawe yalitolewa na waIraq ili yatumiwe katika ujenzi huu. Tangu kazi ya kujenga upya ianze rasmi, majengo ya aina aina tayari  yamechibuka katika  sehemu iliyokuwa misingi ya Babeli  ya hapo zamani. Matukio haya yanatilia mkazo sana yaliyomo katika maandishi matakatifu kwamba hivi sasa mji wa Babeli bado haujaanguka.

Babeli  Mbili

Mnara wa Babeli wa kisasa.

Katika Ufunuo 17 na 18, Mtume Yohana anasema wazi kwamba kuna Babeli mbili ambazo zitajitokeza na kujulikana sana kabla Kristo hajarudi mara ya pili. Babeli ya kwanza itakuwa ni ile ya Uchawi, (mystical) na hii ni kwa ajili ya muelekeo wa uovu (evil ideology) ama utaratibu usiofaa wa maombi.

Babeli ya pili nayo itakuwa ni mji wa biashara, starehe za aina aina na usherati. Katika Ufunuo 17 na 18 jambo moja ambalo latiliwa mkazo ni kwamba kutakuwa na Babeli ambayo imejengwa upya na hii itakuwa ishara ya kwamba mwisho wa yote duniani umekaribia (end-time). Na pia Babeli hii ya pili ndiyo itakuwa makao makuu ya dini ya dunia itakayojitokeza.

Babeli ya kwanza inaitwa: Mystery, Babylon the great, the mother of harlots and abominations of the earth.

Katika Ufunuo 17:5 tunasoma hivi: "Na katika kipaji cha uso wake aliuwa na jina limeandikwa, la siri, ‘Babeli mkuu, mama wa makahaba na machukizo ya nchi."

Kwa ajili Babeli ndipo patatokea dini mbaya, na muelekeo wa kuunganisha na kufanya dini zote ziwe kama moja, kinyume na mafunzo ya  Biblia, Babeli hii itaitwa “Babeli isiyoeleweka” (Mystery Babylon). Tayari hali hii inapinga Ukristo, ambao kuambatana na mafunzo ya Biblia, hakuna nafasi ya haya. Pia tayari kuna mipango kuandaa kikundi kitakachounganisha makanisa yote duniani, na shirika hili jipya litaitwa “mama wa makahaba" jinsi vile tumeona hapa katika Ufunuo 17:5. Yale ambayo hayengetarajiwa miaka kadha iliopita hivi sasa yanafanyika kote duniani katika makanisa. Muungano wa dini na makanisa mbali mbali umejitokeza sana kote duniani.

Juhudi za mashirika mbali mbali kuunganisha makanisa kama vile World Conference on Religion and Peace na World Council of Churches yataungana na kanisa katoliki, na dini za kikristo kutoka mashariki kuanzisha muungano maalum wa makanisa. Kuanzishwa kwa bunge maalum la makanisa kule Chicago Marekani mwaka wa 1993, huenda ukawa mwanzo halisi wa muungano maalum huu wa makanisa kote duniani. Muungano huu ukiwa chini ya kiongozi mmoja, hapa kuhani au nabii aweza akajitokeza kuwa kiongozi kwa urahisi sana. Uhuru wa kuabudu ambao katika mataifa ya magharibi ambapo ukristo ilikuwa dini ya  taifa, umezidi kudidimia. Siku hizi  wazo hili la kuwa na dini ya kitaifa limeanza kuachwa na badala yake dini zote zinaonekana kuwa sawa.

Hii imekuwa na matokeo ya kwamba Ukristo umepoteza umaarufu wake ambao unatajwa katika Yohana 14: 6. Wazo lile kwamba dini zote ni sawa na kwamba wote wanaoabudu wanaabudu Mungu mmoja limeenea. Matokeo ni kwamba tunaelekea pale ambapo dini zitaungana pamoja na kuwa kama kitu kimoja.

Dini moja ambayo itatokea pale nyakati za mwisho itajitokeza wakati mmojaakuwa na kufufuka upya dini kuu ya Babeli. Dini hii ya Babeli ilikuwa na  misingi na  utaratibu ufuatao:

·      Kumtukuza kiongozi wa dunia jinsi vile ilivyokuwa wakati wa Nimrodi. Kiongozi huyu atatawala akishirikiana kwa karibu sana na viongozi wa kidini.

·      Kutaanzishwa ukoo wa watu watukufu, kati yao kutakuwa na wakuu wa busara (masters of wisdom).

·      Kuabudu Mungu wa Jua (Sun god).

·      Kumshukuru na kumpenda, na kumuelekezea mapenzi yasiyo na kifani (adoration) malkia wa mbinguni na mtoto wake (Madonna and Child)

·      Kumpenda na kumuelekezea mapenzi yasiyo na kifani Baali wengi katika jumla (pantheon) ya Mungu.

·      Kutafakari na kuwaza kuhusu mbinu za kuponya magonjwa pasipo matumizi ya dawa (holistic) na matumizi ya cosmic consciousness.

·      Matumizi ya uganga, usomaji sayari, usomaji nyota na matumizi ya alama na ishara za kishetani.

Kama sehemu moja ya mabadiliko ya kidini katika Babeli, Mungu ataanza kuchukuliwa kuwa mfano wa kike. Waandishi wengi walio katika kikundi cha New Age Movement hujihusiha na mjadiliano kuhusu planetary mother yaani mama wa sayari ambaye yuko kiroho katika kila anayezaliwa.

Kando na mwili wake, mtoto  ana mwili maalum ambao unafamfanya awe sehemu moja ya anga, kwa hivyo yuko chini ya ulinzi wa mungu wa sayari. Hawa waandishi hugusia mambo fulani kuhusu yule wanayemwita “mama maalum.” Imani ya kuweka uke katika mambo ya dini ilikuwako katika dini mbali mbali na majina kama: Isis, Venus, Ishtar, na Mariamu. Isis ni Mungu wa Misri wa mazingira, Venus ni mungu wa mapenzi, katika mila ya warumi, Ishtar alikuwa mungu , na pia alikuwa malkia wa Babeli wa mbingu ambaye makao yake yanajengwa upya naye Mariamu ni mama wa  wanadamu.

Mke ambaye  amepanda juu ya mnyama katika Ufunuo 17:3 ni alama kamili ya dini itakayotokea katika wakati wa dhiki kuu. Hapa hii ni ishara ile ya muungano utakaotokea kati ya dini na siasa. Mchumba wake mpinga Kristo ni kanisa lile la uongo. Jina lake ni “Babeli ya miujiza” au  “mama wa makahaba.”

Katika Ufunuo 17:9-10 na Ufunuo 18, huyu  mke wa uovu ametawala katika sehemu kuu za mataifa kupitia imani kuu ya viongozi katika serikali.Hatuwezi tukadharau uwezo wa huyu mama kwa vile anaweza kuhadaa ulimwengu wote nakuushawishi kufuata mafunzo ya yule mpinga Kristo. Yeye atawafanya mamilioni ya wafuasi wake wakati dhiki wamfuate yule mpinga Kristo na kuwafanya waamini kwamba yeye ni masiya na kukubali kuwekewa chapa yake. Katika Zakaria 5:5-11, makao yake makuu yatapelekwa hadi Shinar, yaani Babeli wakati muda kiwango nusu cha dhiki kuu kitakuwa kimepita.

Na wakati huu, wadhfa wake kama mtu wa dini utafifia. Mpinga Kristo atajitoa na kujitangaza kuwa Mungu. Hapo kuamuru kwamba ni yeye tu wa kuabudiwa. Kanisa litakalompinga litaachwa na kuharibiwa: "Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto" (Ufu. 17:16).

Mpinga Kristo ataamuru yule mke wake auawe baada yao kuishi pamoja kwa muda wa miaka 3 ½ . Na huo utakuwa mwisho wa Babeli ya miujiza ambayo imetawala wafalme wote duniani. Ni wale wafuasi wa kanisa la dunia la uwongo ndio wataacha  dini zao na kumuabudu mnyama kama na kukubali chapa yake. Wao ndio wataepuka  taabu na kuuliwa na yule mama wa makahaba. Na hawa watakaoepuka shida wakati huu nao watahukumiwa baada ya miaka 3½ pale Kristo atakaporudi.

Makao Makuu ya Kimataifa

Yakiwa makao makuu ya kiuchumi, kisiasa, na burudani ambayo yamejengwa upya Babeli patakuwa mahali pa muhimu kabisa wakati ule wa dhiki kuu. Twasoma haya katika Ufunuo 18.

Twaweza kutarajia kwamba amashirika makubwa aya kimataifa yatakimbilia kutafuta makao makuu katika mji wa Babeli, na kwamba majengo mapya yatajengwa na kumalizwa kwa haraka sana hapa Babeli. Baada ya muda mfupi, mji huu utakuwa na muelekeo wa kimataifa na kuwa makao ya kuwavutia wote kutoka sehemu mbali mbali kukutana. Pia tamaduni mbali mbali kujitokeza ana kuonekana. Maendeeleo mbali mbali zitajitokeza hapa. Ni bora hapa tukumbuke kwamba ni hapa Babeli mataifa mbali mbali yaligawanyika na lugha baada ya kuharibika mnara ule waliokuwa wakijenga. Jaribio litafanywa kuleta mataifa haya pamoja pahali hapa ambapo yalitawanyika karibu miaka 4500 iliopita.

Ni katika sehemu tambarare ya shinar huko Babeli ndipo mkutano wa kwanza wa kimataifa ulifanywa. Haya yapatikana katika Mwanzo 11:4: "Wakasema, Haya, na tujijengee mji na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusiapate kutawanyika usoni pa nchi yote."

Katika nyakati hizi, wito kama huu unaweza kujitokeza kwa njia hii: Na tuungane pamoja, tukajenge mjii mkuu katika ya mashariki na magharibi ili ukawe alama ya umoja wa kimataifa. Hebu tukaanzishe umoja maalum wa dini zote duniani na tujenge imani zetu kiroho ili tufikie utukufu wa juu zaidi. Hebu tuanzishe  matumizi ya aina moja ya pesa, serikali moja na utaratibu wa maisha usio na mgawanyiko wowote. Na ni kupitia haya tutaweza kuungana na kuishi pamoja katika dunia hii bila kutofautiana kuwa mataifa tofauti tofauti yanayogombana na kutosikilizana. Utaratibu wa mawazo ya Babeli hivi sasa unaongezeka san duniani. Mawazo haya yatatimizwa kwa matendo kwa haraka sana. Zekaria anasema kwamba mwanamke anayeitwa muovu (wickedness) atapelekwa Babeli na wake wawili wenzake ambao wana hewa katika mabawa yao. Naye atajengewa nyumba katika Shinari ambayo ni Babeli (Zek. 5:9-11).

Popote pale ambapo bunge la taifa jipya la Babeli la kidini litaanzishwa, uamuzi wa haraka utachukuliwa kuhusu ni wapi makao yake makuu yatakuwa. Ni wazi makao makuu haya yatakuwa ni Babeli.

Ujeuri  wa Kishetani Na Rushwa

Pale karibu na mwisho wa dhiki kuu, uovu katika mji mpya wa Babeli hautakuwa na kipimo. Katika Ufunuo 18, twasoma kwamba dhambi Babeli, sawa na Sodoma na Gomora zitazidi kiwango hata karibu “kufikia mbinguni” (Ufu.18:5). Patakuwa mahali wa usherati na karamu nyingi za uovu (Ufu. 18: 7, 9). Muziki utakuwa sehemu moja ya muhimu katika starehe na usherati katika mji huo Babeli (Ufu.18:22).

Wakati wa kufunguliwa mji wa Babeli mwaka wa 1987, mwezi wa tisa na  pia  mwezi kumi, sherehe hii  ilikuwa na  tamasha za muziki za kimataifa. Ni wazi kwamba muziki ambao ni wa mtindo wa rock; na ambao huleta na kuongeza matumizi ya madawa ya kulevya, ulevi wa pombe, usherati, na uasi, uchawi, usomaji wa nyota na mengine maovu; huu utakuwa ni muziki ambao utanawiri sana Babeli. Si ajabu Biblia inasema muziki aina hii pamoja na vyombo vya sauti ya juu vya muziki vitaharibiwa kabisa pamoja na mji huu wa Babeli. Vyombo vya muziki ambavyo ni vya makelele, vyote vitanyamazishwa, na sauti za waimbaji hawa hazitasikika tena (Ufu. 18:22).

Kuharibiwa Babeli

Mji huu wa Babeli utaharibiwa kabisa pale mwisho wa dhiki kuu. (Ufu. 14:8, 16:17-19, 18:2, 10, 21). Na ni wazi hapa kwamba Babylon haitaangamia kwa hatua. Babeli itangaamizwa ghafla kwa muda wa saa moja. Sawa na Sodoma na Gomora, Babeli itachomwa na moto (Ufu. 18:8-10, 18; Isa. 13:19; Yer. 50:40). Na hapo hapo mtetemeko wa ardhi pamoja na mingurumo ya radi itapasua mbingu, na baadaye Babeli kudidimia katika ziwa la moto, hivi kwamba mji huu hautaweza kujengwa tena wala kuwa mahali pa kuishi (Ufu. 16:17-19; 18:21). Moshi ule utakaotoka pale utatengeneza wingu kubwa sana  juu ya sehemu hii ya Shinari, na hata ambazo ziko katika ghuba la ujaemi (Persian Gulf) zitaweza kuona moshi huo (Ufu. 18:17-18). Wafanyo biahsra na na mabaharia watatokwa na machozi pae mji huu utakapoangamizwa pamoja na mali ilioko, umaridadi na utukufu wake.

Kimbieni Kutoka Babeli

Mungu atoa wito na kuwataka watu wake waondoke Babeli. Katika Ufunuo twaambiwa: "Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema, Tokeni kwake enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake" (Ufu.18:4).

Amri hii siyo ya watu wa Mungu peke yaop ambao watajikuta katika katika mji huu wakati wa dhiki kuu., bali ni wito wa wote ambao hivi sasa wao ni wanachama wa madhehebu ya  kiBabeli, na dini za huko. Usijihusishe na makanisa ambayo hivi sasa shughuli zao ni kujenga minara kama ile ya Babeli. Hali yao ya uovu huenda ikakudhuru wewe pia. Kwa njia ya upole, wamweza wakakakupoteza njia na kukuletea madhara. Huenda wakakupoteza wakati ule wa muhimu ambapo twangoja kwa hamu kurudi kwa mwokozi wetu Yesu Kristo, ambaye ni yeye kiongozi wa kweli wa kanisa. Wengi hivi sasa wadanganywa na manabii wa uongo.

Mji wa Babeli, siasa zake, na misingi yake ya kiuchumi, usherati, na dini ambazo hazieleweki: hizi zote ni mitego ambayo imewekwa na muovu ambaye hawatakii mema watu wa Mungu. Jiondoe katika haya yote ikiwa unataka kuendelea kuwa na imani bora ya kumtii Kristo na kufanya yaliyo mema.

Mwisho wa Babeli umekaribia; siku zake zaweza kuhesabiwa. Jiepushe na yote yanayohusu Babeli. Onyo hili lapatikana vizuri katika Isaya 52:11 ambapo tunaambiwa: "Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya Bwana."