4. Mpinga Kristo

Matukio yote ambayo  yametajwa katika Ufunuo 6-9 yatatokea katika muda wa miaka saba. Muda huu wote ambao ni sawa na siku saba katika wiki moja ni  wakati unaoitwa muda wa dhiki kuu. Muda huu wa miaka saba umegawanywa katika sehemu mbili; kila moja ni ya miaka  tatu  na nusu.

Katika sehemu ya kwanza, yaani miaka tatu na nusu ya kwanza, kutakuwa na juhudi kubwa ya kuleta amani nayo shughuli hii itaongozwa na  mpinga Kristo mwenyewe. Atajitokeza na kujigamba kwamba ni yeye kiongozi wa pekee duniani kote. Na pale juhudi yake ya kuleta amani itakapokosa kufaulu, basi atajitokeza kuwa mtu anayetaka kuleta amani kwa kutumia nguvu.

Wakati wa miaka tatu na nusu hivi ya mwisho  wa dhiki kuu, yeye atatawala kimabavu na kuwatesa watu. Mamia ya mamilioni ya watu watauliwa kiasi kwamba wale watakaokufa kitavunja rekodi.

Wakati wa sehemu ya miaka tatu na nusu hii ya mwisho ndio wakati unaoitwa dhiki kuu kamili (the great tribulation.) Hata wako wengine ambao husema miaka saba yote kuwa ni miaka ya dhiki kuu. Lakini inafaa tuelewe hapa kwamba ni wakati ule wa miaka ya mwisho ndipo watu wataumizwa kabisa. Miaka ile ya mwanzo itakuwa ni wakati wa udanganyifu na kuwahadaa watu kuhusu mambo ya imani na kadhalika. Ni katika miaka tatu na nusu ya mwisho ndipo kutatokea uharibifu usio na kifani: uharibifu utakaoanzishwa na kuendelezwa na huyu mpinga Kristo.

Waendeshaji Farasi Wanne

FARASI MWEUPE

Mpinga Kristo, kama mpenda amani, kiongozi wa dunia na pia Masihi.

FARASI MWEKUNDU

Mpinga Kristo, kama dikteta wa kije­shi, muongo ajiitaye mungu wa dunia.

FARASI MWEUSI

Mpinga Kristo,  imla anayewanyanyasa  wa watu.

FARASI WA RANGI YA KIJIVUJIVU Mpinga Kristo mwuaji na malaika wa kifo.

 

Katika Ufunuo 6:1-8, mpinga Kristo atajitokeza mara ya kwanza kwa njia ya udanganyifu ambapo ataonekana kuwa ni malaika wa mwanga. Baada ya  hadaa hii ya mwanzo, ataanza kujitokeza  kama mkuu na baadaye kuwa mtawala wa kimabavu kabisa.

Pale mwanzoni, atajitokeza kuwa mpenda amani; ambaye  jukumu lake duniani ni kuleta amani na hali ya kuelewana kila mahali (Farasi mweupe). Akitumia ujuzi wa kidiplomasia, yeye atayashawishi mataifa yaanzishe serikali moja duniani. Pia atatumia mbinu hii kuanzisha dini moja ya watu wote. Kisingizio chake ni kwamba anataka watu wasitafautiane kwa vyo vyote. Hata hivyo, hatafanikiwa kutimiza baadhi ya haya anayonuia kuyatimiza. Na hapo ndipo atakapobadilika na kujaribu kutumia nguvu kutimiza haya. Hapa ataanza kutawala kijeshi (Farasi mwekundu).

Baada ya hapo, yeye atapiga hatua na kuanza mbinu za kusimamia uchumi kote duniani. Ataanza kuwapimia watu chakula hasa wakati wa njaa (Farasi mwekundu).

Na baada ya hayo, kile kitakachokuwa kimebaki ni yeye sasa kutembea huku na huko akijaribu kuwanasa wafuasi watakaomfuata hadi jehenam (Farasi mwenye rangi ya  jivu).

Katika matamshi yake ya unabii, Mwokozi wetu Yesu Kristo alitaja matukio ambayo yatatokea wakati wa dhiki kuu (Mt. 24:4-9).

·      Jichunge usije ukadanganywa. Wengi watakuja kwa jina langu wakisema,"Mimi ndimi Kristo" nao watawadanganya wengi (Farasi mweupe).

·      Na mtasikia uvumi kuhusu vita, kwa vile mataifa yatajitokeza kupigana (Farasi mwekundu).

·      Kutakuwa na njaa na magonjwa (Farasi mweusi).

·      Watakushika na kukuletea maafa  na kukuua. (Farasi wa rangi ya kijivujivu).

Kati ya haya tumetaja hapo juu, yako yale ambayo tumekuwa tukiyaona katika baadhi ya mataifa yetu, na hasa kata nchi za kiKomunisti hapo miaka iliopita.

Pale mwanzo  wa utaratibu waserikali ya kikomunisti, watu huelezwa kwa udanganyifu kwamba mtindo fulani wa kisiasa utawaletea mafanikio ya aina. Wao hujichukua kuwa na umoja na undugu wa kipekee katika taifa.

Na baadaye, ukweli hujitokeza pale serikali hizi zinapoanza kuwatesa na kuwagandamiza watu wake. Wakati fulani, wao husema kwamba wanajenga upya taifa, na kwamba ni sharti wabomoe vyote vya awali vilvyokuwako (Farasi mwekundu).

Wakati wa vita, kuna kiasi kikubwa sana cha hasara   na uharibifu wa mali. Uchumi huzorota. Watu hupoteza kazi, na kazi zenyewe huwa ni haba. Chakula huwa ni kichache na watu hufaa na njaa wakati fulani. Na pale chakula kinapopatikana, basi bei yake huwa ni ya juu kabisa (Farasi mweusi).

Na mwisho, yale yaliyoanza na nderemo na vigelegele kwa jina la mabadiliko katika serikali na kadhalika huisha na kilio, na vifo (Farasi wa rangi ya jivu.)

Kwa kweli, duniani yako matukio sawa na haya ambayo yametajwa katika maandishi matakatifu, na hasa katika Ufunuo. Katika 1 Yoh. 2: 18, wako wapinga kristo wa uwezo wa chini ambao tayari wamewahi kujitokeza. “Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wamekwisha kuwapo.”

Kwa hivyo, wako wengi ambao tayari wamemtangulia mpinga Kristo. Na uovu wao utaungana na kuleta madhara makubwa wakati wa dhiki kuu. Kwa hivyo, shida zilizoko kama njaa,  vita kati ya mataifa: haya yote ni matukio ambayo yanatuelekeza katika siku za mwisho, ambazo ni siku za dhiki kuu. Matukio haya yanafaa yatukumbushe kwamba tunaishi nyakati za mwisho; ni nyakati za vita na nguvu za kishetani na za uovu. Hata hivyo, ni jambo la kutiliwa maanani kwamba  bado hatujayaona  maovu sawa na yale tunayoyatazamia wakati wa dhiki kuu. Kuhusu dhiki kuu hii, Kristo anasema hivi:

"Kwa kuwa wakati kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. Na kama siku hizo zingelifupizwa, asingeokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo" (Mt. 24: 21-22).

Na pale farasi wa maafa watakapojitokeza jinsi vile tunavyosoma katika Ufunuo 6, matukio ya ajabu na kutisha yatafuata. Matukio haya yatafichua wazi hatari na hasara ya dhambi na uovu.

Farasi Mweupe

Katika Ufunuo 6:1-2, tunasoma hivi: "Kisha nikaona napo mwanakondoo alipofungua moja ya zile mihuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne  akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda."

Pale mwanzo wa dhiki kuu, Kristo anafungua muhuri wa kwanza akiwa juu mbinguni, na malaika wa amani anajitokeza akiwa amepanda farasi mweupe duniani. Ana nyuta mkononi, na ameficha mishale yake, na hii ni kwa ajili anataka kujitokeza kuwa malkia wa amani. Hataki aonekane kuwa mtu ambaye amejihani kwa ajili ya vita. Yeye anataka aonekane kuwa  mleta amani.

Yeye hakuweza kujitokeza mapema kwa ajili ya nguvu za Mungu ambazo zilikuwako kupitia Kristo kanisani. Na sasa kwa ajili kanisa haliko tena, basi huyu muovu amepata nafasi ya kujitokeza. Mpinga Kristo amepata nafasi fupi ya kuweza kutenda uovu wake duniani. Na hii ni kabla Mungu wetu hajajitokeza kumuondolea mbali na kumuelekeza kwenye moto wa milele.

Ni wazi kwamba tukiangalia yale ambayo tayari tumesoma, aliye juu ya farasi mweupe si mwingine ila ni mpinga Kristo mwenyewe. Ni kosa kusema kwamba yule aliyebebwa na farasi mweupe katika Ufunuo 6 ni Kristo kwa sababu katika Ufunuo 19 twasoma kuhusu Kristo akiwa kwenye farasi mweupe. Hakuna hakikisho kuhusu jambo hili. Vitu ambavyo huchukuliwa kuwa mfano (symbols) haviwezi kuchukuliwa kuwa vya maana halisi.

Kwa hivyo ni lazima tuvichukue ama tupate maana yake kutoka kwa maandishi yale au kutoka kwa sehemu tunayosoma (context). Hii ndiyo sababu katika sehemu fulani, tunachukua Kristo kuwa ni yule simba wa Yuda (Ufu.5:5) na pia katika sehemu tofauti, shetani anachukuliwa kuwa kama  simba angurumaye akitafuta mtu ammeze (1 Pet. 5:8).

Katika Ufunuo 6, Yesu ameketi kwenye kiti cha enzi, anafungua kitabu ambacho kimefungwa na mihuri saba, na katika kitabu hiki, orodha ya jinsi hukumu itatolewa kwa wote wanaotenda dhambi imeandikwa.

Lengo kuu hapa ni kufichua muovu shetani na hila zake zote, pamoja na wale ambao  wanamuunga mkono, na abaada ya hapo wahukumiwe na nguvu zao kote duniani ziondolewe kabisa. Wakati kila muhuri unapofunguliwa, farasi wanne wale wa kwanza wanafunguliwa, na kupewa ruhusa kudanganya na kuua watu. Uovu na hasara yao yaonekana wazi pale tunaposoma katika Ufunuo 6:8:

"Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni mauti, na kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi."

Hata hivyo, inafaa tutilie mkazo hapa kwamba huyu mpinga Kristo atajitokeza na kusudi la kutaka aonekane kama anayetaka mema, anataka kuwe na amani, umoja na undugu kati ya watu na mataifa.  Watu wataungana na kuanzisha mashirika makubwa katika dini, biashara na kadhalika. Umoja kama huu waweza tu kujitokeza pale migawanyiko itakapondolewa kabisa kati ya watu. Itabidi pajitokeze kanisa lililo na wafuasi kote duniani.

Katika Ufunuo 17:13 twasoma kwamba wafuasi  wote wa mpinga Kristo kisiasa watakuwa watu wa kuelewana vyema kabisa. Wao wataacha nyadhiifa zao wakiwa na kusudi la kumpandisha cheo mpinga Kristo. Mataifa yote duniani yatakuwa kama taifa moja. Hata yawezekana mipaka ya kimataifa itaondolewa kabisa. Hali ya kutoelewana kati ya mataifa itatupiliwa mbali kabisa.

Hata katika dini, kutakuwa na muungano wa makanisa, na labda yawe na jina kama Enzi Mpya. Kiongozi wa taifa moja kuu duniani pia atajiweka taji la kuwa kiongozi wa kidini pia. Atakuwa kiongozi kama vile Mitreya Budha, Krishna, Imam Mahdi and Hata kama Kristo. Yeye atakuwa pia Masihi wa Wayahudi. Dini hizi zitakubaliwa kuendeleza shughuli zao kwa muda wa miaka tatu na nusu ya hapo mwanzo. Kibali hiki kitatolewa chini ya sharti kwamba dini hizi hazitasita sita kuwa kama dini moja na kushirikiana kwa mambo mbali mbali.

Kristo ametuonya kuhusu hatari hii. Katika Mathayo 24:4-5, twasoma hivi: "Angalieni, mtu asiwadanganye, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi."

Na kwa vile umoja unaoletwa na mpinga Kristo huyu utatofautiana kabisa na mafunzo yaliyoko kwenye maandishi matakatifu, na hasa katika Matendo 17:26 na Yohana 14: 6,  wako wale ambao watajitokeza na kumpinga huyu Mpinga Kristo haya yote. Basi hapo ndipo unyama utajitokeza kabisa. Mpinga Kristo sasa atatupilia mbali ule udangayifu wake na hapo ataanza kuwanyanyasa na kuwaletea taabu nyingi wakristo na wote wale  wenye imani halisi.

Farasi Mwekundu

Katika Ufunuo 6:4  twaambiwa hivi: "Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa."

Viongozi wengi wa kisiasa wanaposhindwa kuendelea kuwa na wafuasi wengi, wao hubadili mienendo yao na huanza kutumia nguvu za kimabavu kujiendeleza. Mpinga Kristo atakuwa sawa na viongozi hawa: atatumia mbinu kama hizi zao viongozi wetu wa kisiasa na kadhalika.

Mambo yatakapobadilika, atajitokeza wazi kuwa mtawala asiyewajali watu wake, na hapo ataanza kutumia nguvu kuwatawala na kuwanyanyasa wale walio chini yake.

Yeye atajipandisha cheo kutoka Masihi wa dunia kuwa mungu. Haya twayasoma katika Wathesalonike wa pili 2:4. Yeye atawalazimisha watu kumchukua kuwa kama mungu, haya twayasoma katika Ufunuo 13: 5-6. Hata hivyo, taifa la Israeli litamkataa kata kata huyu mpinga Kristo. Na taifa hili litamkataa pale atakapochafua hekalu ya wayahudi ilioko Yerusalemu. Atafanya hivyo kwa njia ya kuchukua mchoro wake na kuuweka katika hekalu hii. Haya twayasoma katika Mathayo 24:15. Na pale waisraeli watakapomkataa, yeye atazusha vita  akiwa na lengo la kuwaangamiza wayahudi hawa sawa na jinsi vile Adolf Hitler alivyofanya wakati wa vita vikuu vya pili duniani.

Katika kitabu cha Danieli tunasoma hivi: "Na wenye silaha watasimama upande wake, nao watapatia unajisi  mahali patakatifu, ndio ngome, nao wataondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, nao watalisimamisha chukizo la uharibifu" (Dan. 11:31).

Akiwa kiongozi wa kijeshi, wengi watamuona kuwa shujaa na kumsifu sana  huyu mpinga kristo. Wengi watatamani kuwa kama yeye; na twasoma hivi katika Ufunuo 13:4: "Akamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama  uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?"

Yeye atapata ushindi katika vita vingi katika mataifa mengi duniani, na nguvu zake na utawala utaenea kila mahali (soma Ufunuo 13:7).

Farasi Mweusi

"Na alipoifungua muhuri wa tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake" (Ufu. 6:5).

Vita huleta hasara isiyo na kifani. Pesa huwa haba, mapato ya kitaifa hupunguka, maendeleo ya kiuchumi husimama, na hata njaa huweza kutokea.

Ili kuthibiti hali ya mambo, mpinga Kristo ataanzisha mabadiliko makali ya kiuchumi. Kwa kupitia matumizi ya  mitambo ya komputa, mpinga Kristo ataanzisha mbinu ambayo itamuwezesha kusimamia  moja kwa moja uchumi katika kila sehemu duniani. Uwezo wa kila mtu kusimamia pesa zake utaondolewa, na hapa njia mpya ya kutumia na hata kutuma pesa itaanzishwa. Matumizi ya pesa taslimu yataondolewa kabisa.

Na kwa ajili ya vita, uchafuzi wa mazingira na hali mbaya ya hewa, kutatokea ukosefu mkubwa wa chakula. Basi hapa watu wataanza na kupimiwa chakula. Na huku akiwa anawasimamia watu kwa njia hii, mpinga Kristo atatumia nafasi hii kuwanyanyasa watu zaidi. Wale ambao watakuwa wafuasi wake halisi, na ambao atawawekea alama ndio wataepuka baadhi ya matatizo na ugumu wa maisha utakaotokana na mbinu zake Mpinga Kristo. Ni wale tu watakaokuwa na chapa yake mpinga Kristo huyu watakubaliwa kununua vyakula madukani (Ufunuo 13:16-18).

Farasi Wa Rangi Ya Kijivujivu

"Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni mauti, kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi" (Ufu. 6:8).

Kwa vile mpinga Kristo anatoka kwake shetani, sawa na baba yake, yeye atakuwa muuaji. Yeye atafurahia pale vifo vitakapotokea. Atafurahia sana vifo vya mamilioni ya watu ambao ni viumbe vyake mungu. Katika Ufunuo 6:8, twasoma kwamba karibu theluthi moja ya watu duniani watauliwa. Hii ni karibu watu billioni 1.4. Hesabu hii ni  mara ishirini na saba idadi ya watu waliouawa wakati wa vita vikuu vya pili duniani.

Mpinga Kristo

Katika Ufunuo 13:1-2; na Ufunuo 17:9-12, ziko ishara au alama ambazo zaweza kuchukuliwa kuwa vielelezo vya kukuwezesha kumtambua mpinga Kristo. Tunaelezwa kinaga ubaga kwamba mpinga Kristo  ni mnyama mwenye vichwa saba na pembe kumi. Vichwa saba ni   zile falme saba ambazo zimetajwa katika Ufunuo 17:9-10. Katika kitabu cha Mwanzo, Isaya na Danieli, milki hizi zimetajwa.

Nazo ni:

1.   Babeli ya zamani ambayo ilianzishwa na kujengwa na mfalme Nimrodi.

2.   Milki ya Ashuru ambayo ilijumuisha makabila kumi ya Israel ambayo yaliuwa katika ifungo karne ya nane kabla kuzaliwa mwokozi wetu Kristo.

3.   Milki ya Babeli (Neo-Babylonian Empire) ambayo iliishinda  falme ya Yuda katika karne ya sita kabla ya kuzaiwa mwokozi wetu Kristo, na kuwachukua hadi katika utumwa wenyeji wa hapa.

4.   Milki  ya Medo Persian.

5.   Milki ya kiGiriki.

6.   Milki ya kiRumi.

7.   Milki  ambayo  itajitokeza baada ya dhiki kuu.

Katika Ufunuo 17:10, Yohana anasema kwamba wakati huu, mataifa tano tayari yalikuwa yameangamia. Moja lilikuwa lingali lipo, na ya saba lilikuwa bado linakaribia kujitokeza.

Katika mwaka wa 95 wakati kitabu cha ufunuo kilipoandikwa, mataifa tano  yalikuwa hayako; na haya ni kutoka taifa la Babeli hadi lile la kiGiriki. Taifa la Warumi lilikuwa likitawala. Utawala wa mnyama Mpinga Kristo ulikuwa bado unangojewa. Taifa hili ndilo laonyeshwa likiwa mfano wa mnyama aliye na kichwa na pembe kumi.

Mataifa haya yote sita yalikuwa hayakubaliani na kuwako ufalme wa Mungu hapa duniani. Walikuwa na imani katika mambo mengi ya kishetani, na waliamini kwamba viongozi wao ni sawa na Mungu. Na uovu wao huu na uasi utafikia kiwango ambapo unaweza kulinganishwa na uovu wa nyakati za mwanzo wa Babeli ambayo inachukuliwa kuwa mwanzo wa uovu wote na uasi. Twambiwa hivi, katika Ufunuo 17:18:

Na yule mwanamke uliyemuona ni ule mji ule mkubwa, wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi.

Mpinga Kristo anafananishwa sana na mataifa ya zamani hivi kwamba yeye huchukuliwa kuwa mfano wa chui, makucha ya dubu, mdomo wasimba na kichwa chenye pembe kumi (Ufu. 13:2).

Ishara hizi ni sawa na zile ambazo hutumika katika taifa la Babeli (Simba), Katika Medo Persia (Dubu), Ugiriki (Simba), na katika taifa la Warumi (Mnyama aliye na pembe kumi.)

·      Mpinga Kristo atafuata utamaduni wa kiBabeli ambao walimuasi mfalme wao. Atajitangaza na kujiweka wakfu kuwa mungu aliye  zaidi ya miungu wote. Yeye atahakikisha kwamba sanamu inatengenezwa iliyo mfano wake, na watu wataichukua kuwa kitu cha kusali. Wale watakaokataa kufanya hivyo, watachukuliwa na kutupwa kwenye moto. Yeye pia ataanzisha vita na taifa la wayahudi akiwa na lengo la kuwaangamiza wayahudi wote.

·      Sawa na taifa la Medo Persian, yeye atanyanyasa mataifa yote, na kutupilia mbali uhuru wao, na kuyatwaa kuwa sehemu katika taifa lake kuu. Yeye atatawala kimabavu, bila kuwajali watu wake; na ataweka  kanuni na  sheria kali. Kati ya sheria hizi ni kutoka Medes na Uajemi. Yeye pia ataamuru wayahudi waangamizwe.

·      Taifa la kiGiriki lilichukuliwa kuwa mfano  wa chui na Danieli; chui aliye na mabawa manne. Taifa hili lilikuwa na jeshi lenye uwezo wa kusafiri kwa haraka. Mpinga Kristo atatumia mbinu hizi katika jeshi lake. Atakuwa na uwezo wa kuwatuma wanajeshi wake kwenda mbali kwa muda mfupi. Katika taifa hili la zama kabisa, kulikuwa na roho ya kutowapenda wayahudi Mfalme wa waGiriki Antiochus Epiphanes alikuwa mfame aliyewachukia sana wayahudi. Mpinga Kristo naye atakuwa na chuki kama hii.

·      Mnyama wa nne ana pembe kumi na meno ya chuma; uso wake  ni wa kutisha na haupendezi kamwe. Hii ni ishara ya ukali, na roho chafu ambayo warumi waliuwa nayo. Wakati warumi walipo vamia Wapalestina, na kunyakuliwa kwa mji wa Yerusalemu, mamia ya wayahudi waliuawa, wengine wakanyongwa kwenye miti. Wale waliopona, walichukuliwa kuwa wakimbizi. Mpinga Kristo ataendeleza uovu wa aina hii.

Pembe kumi zile ni ishara ya muungano wa kisiasa utakaoanzishwa na mpinga Kristo. Pale mwanzo wa dhiki kuu, mataifa kumi katika bahari ya Mediteranean yataungana chini ya uongozi wake mpinga Kristo.Katika Ufunuo 17:12-13, tunasoma hivi:

"Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamalaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama. Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao."

Na katika Danieli 7:8, tunasoma hivi: "Nikaziangalia sana pembe zake, na  tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang'olewa  kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu."

Mpinga Kristo atathibiti  tawala tatu za kifalme chini yake, na hapa ni tawala nane zitakuwa zimebaki.

Katika Danieli 11:36-45, mpinga Kristo anaitwa Mfalme wa Kaskazini. Katika agano la kale, Mfalme wa Ashuru alikuwa na jina hili, mfalme wa kazkazini. Ashuru ilikuwa sehemu kubwa iliopakana na  Israeli upande wa kazkazini na kazkazini magharibi. Taifa hili lilijumuisha Syria, Lebanon, Iraq na sehemu fulani ndogo katika mataifa jirani. Katika Isaya 10:20-27; mpinga Kristo aliitwa tena Ashuru. Na katika Mika 5:5-7, kuna uthibitisho hapa kwamba mpinga Kristo atakuwa muyahudi wa kutoka Ashuru.

Matukio ya hivi majuzi, sana sana ujenzi mpya wa Babeli katika  taifa la Iraq ya leo huenda  ukawa ndio mwanzo wa kujitokeza kwa mfalme kama huyu. Hata hivyo, ni sharti awe muyahudi ili wayahudi waweze kukubali kuwa yeye ni  Masihi.

Zaidi ya yote, ishara kuu ya mpinga Kristo ni ule uhusiano wa karibu alio nao na makundi ya kidini, na hasa jinsi vile anajitahidi ili atambuliwe kuwa kiongozi wa wote. Uongozi wa kidini na kisiasa uko katika mikono yake. Na hapa anataka aonekane kama yeye ndiye atakayewaepusha wanadamu kutoka dhiki kuu.

Na pale atakapotenda maajabu, basi ulimwengu wote utakuwa tayari kumfuata jinsi vile tunavyosoma katika Ufunuo 13:3: "Nikaona kichwa chake ni kama kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstajabia mnyama yule."

Wafuasi wake wote watapinga wazo kwamba huenda huyu Mpinga Kristo ni Masihi wa uongo.

Nguvu Za Mpinga Kristo

Pale itakapofikia katikati ya muda ule wa dhiki kuu, mpinga Kristo atajibadili kwa njia ya kustajabisha kabisa. Yeye atajitahidi katika hila za kuwalazimisha watu kuwa wafuasi wa dini yake ya kishetani. Kuna wakati ambapo atajeruhiwa, na baada ya hayo yeye atajiponya kwa njia ya miujiza kabisa. Na baada ya hapa, hakutakuwa na haja yake yeye  kujificha na kutoonekana wazi na hila zake. Atajitokeza kuwa dikteta mkuu ambaye ana tamaa ya ukubwa isiyo na kifani. Kutakuwa na mauaji, na mambo mengi ya kutisha.

Mpinga Kristo huyu atakuwa mkuu wa kisiasa, kidini na hata kiuchumi. Lengo lake katika kung’ang’ania uongozi wa haya yote ni kwamba atakuwa anataka aweze kuwaweka watu katika hali ya utumwa.

Na nguvu zake hasa ni za kijeshi. Atatumia  jeshi na silaha kuthibiti utawala wake. Hakuna atakayeweza kufikia uwezo wake, kwani twasoma hivi katika Ufunuo13:7, “Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.”

Na katika mambo ya dini, yeye atajipandisha ngazi,: kutoka Masihi, na kuwa sasa mungu. Katika Wathesalonike wa pili 2:4, tumeelezwa kwamba atajipandisha cheo cha juu kuliko vyote katika makundi yote ya kidini, na  katika makao makuu ya kidini hekaluni, ni yeye atakayeketi kwenye kiti cha enzi. Wakati huu, yeye atapiga marufuku kabisa kila kikundi cha kidini. Sehemu za maombi zitachomwa (Ufu. 17: 16). Nayo maombi ya wayahudi hekaluni yatasimamishwa na baadaye kupigwa marufuku (Dan. 9:27).

Lile litakalobaki ni watu kumuabudu huyu mpinga Kristo na kumchukua kuwa kama Mungu. Wale watakaokataa kumuabudu wauawa (Ufu.13:15). Wakati huu, kutakuwa hata na manabii ambayo watakuwa waalimu wa mafunzo ya huyu mpinga Kristo, na imani hii ya mpinga Kristo itaenea kote duniani.

Na kando na haya ambayo yatajitokeza katika imani, kutakuwa na mabadiliko ambapo mpinga Kristo sasa ataanzisha njia mpya za  uchumi. Uchumi huu sasa utakuwa ule ambao hamna  matumizi ya pesa. Sasa badala ya matumizi ya pesa, watu watawekewa chapa ambazo kwa kutumia mitambo ya komputa, chapa hizi zaweza kutumiwa katika ununuzi na uuzaji wa aina aina. Maelezo kamili yanapatikana katika Ufunuo 13:16-18 na hapa tunasoma hivi:

"Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa masikini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote, asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita sitini na sita."

Uchumi Pasipo Matumizi ya Pesa Taslimu

Maendeleo ya kisasa na ufundi wa leo unamwezesha mwanadamu kufanya baadhi ya yale ambayo yametajwa katika Ufunuo. Hivi sasa ni rahisi kuanzisha njia  fulani ambapo matumizi ya pesa hayahitajiki kamwe katika shughuli mbali mbali za kila siku.

Inastahili kutiliwa mkazo hapa kwamba, mpinga Kristo hataweza  kuthibiti uwezo wake duniani ikiwa hatakuwa na nguvu za kiuchumi. Lazima uchumi wote uwe mikononi mwake ndipo ataweza kutawala vyema. Kwa hivyo, mbinu yake moja kubwa lazima iwe ile ya kutaka kusimamia uchumi.

Kwa muda sasa, matumizi ya vyombo kama vile Credit Cards badala ya pesa taslimu yameenea sana. Na maendeleo ambapo matumizi ya pesa yanapunguzwa yamekuwa yakipiga hatua siku baada ya siku. Kwa mfano mnamo tarehe 17/5/92, gazeti la SUNDAY STAR lilichapisha habari hii:

NGUVU KWENYE NGOZI

Chombo Maalum kilichoko kwenye ngozi

Kurahisisha Maisha

Chombo Cha Kuwekwa Kwenye ngozi

“Naye akafanya kuwekwa kwa alama maalum kwenye mkono wa kulia au kwenye kichwa” (Ufu.13:16).

Maandishi haya yamewafanya wengi waanze kuchunguza uwezekano wa kuweza kuwasimamia wanadamu kwa njia sawa na ile ambayo mwana sana mwandishi wa riwaya Orwell aliweza kuzungumzia katika baadhi ya utunzi wake. Wakati huu, kila mmoja wetu anahitajika kuwa na hesabu na nambari za aina aina kama vile nambari ya kitambulisho (ID), nambari ya malipo ya ushuru wa serikali (Pin Number)na kadhalika.

Na kwa sababu ya kuwa na nambari nyingi hivi, wazo moja ambalo lajitokeza ni hili: Mbona kila mtu asiwe na namba moja tuu? Na isitoshe, mbona namba kama hii isiwekwe kwenye nyuso kama na wino?

Na wazo lililo bora zaidi ni kutoka kwake Johan Bornman ambaye anasema, badala ya haya yote, mbona mtambo mdogo kabisa wa komputa uitwao chip usiwekwe chini ya ngozi sehemu ya uso, na mtambo huu uwe na nambari zote zinazohitajika?

Faida ya kuwekewa mtambo chini ya ngozi

Ujuzi bora zaidi ya wote ni ule wa kutumia chombo ambacho kinaitwa smart cards. Chombo hiki ambacho kwa kweli ni aina ya kadi maalum ina mtambo mdogo kabisa ukubwa wake sawa na kichwa cha sindano ina mtambo ule uitwao chip ulio na uwezo wa kuweka na kukumbuka mambo mengi kabisa.

Mtambo huu una uwezo wa kufanya mengi kama vile kuchunguza alama aza vidole (fingerprints), ila nambari ya kazi inayotumiwa kutoza ushuru (PIN), na hata aina ya sauti (voice prints) Pia ina uwezo wa kugawa habari mbali mbali katika faili. Pia mtambo huu unaweza kuweka habari kuhusu kazi za biashara zinazohusu pesa, historia ya magonjwa ya mtu, hata historia ya matibabu aya meno ambayo mtu amepokea maishani. Pia mtambo huu mdogo kabisa unaweka habari kuhusu makao ya mtu, na wale wa ukoo wake. Wengi bila shaka watakubali kwamba huu ni mtambo wa kufaa, kwani sasa hakutakuwa na haja kuweka kadi kadha zenye habari hizi, wala kuwa na kitambulisho, wala faili kubwa kubwa ambazo zina habari kuhusu maradhi ya mtu fulani na kadhalika.

Na isitoshe, wanasayansi hivi sasa wametengeneza aina ya smart card ambayo yaweza kusomeka na kutumiwa pasipo matumizi ya mashine maalum iliyo na mtambo wa sumaku. Mtambo sasa waweza kusomeka tu pale unapotumbukizwa katika mashine iliyo na mitambo ya electronic moja kwa moja.

Ikiwa tutaweza kutoa sehemu ya plastiki inayozingira kadi hii, basi tutabaki na kile chombo kidogo yaani chip nacho chaweza kikaingizwa kwenye ngozi kwa  urahisi. Hata hivyo lile ambalo litawapa wanasayansi wakati mgumu ni uamuzi kuhusu ni wapi kwenye ngozi mtambo huu utawekwa.

Hebu fikiria juu ya faida ya mtambo huu? Hakuna cha kutumia kipande au vitabu mbali mbali. Katika duka kama vile supermarket, kile kinahitajika ni kuweka mkono pale kwenye kibofu hiki na hapo pesa ulizo nazo zinajulikana mara moja. Kitambulisho hakiwezi kulinganishwa na nambari maalum iliowekwa katika sehemu ya uso. Hivi sasa tunatumia nambari nyingi sana, mbona basi tusichague nambari moja na kuiweka sehemu fulani maalum mbali na kadi ya plastiki?"

Mwandishi wa makala haya anafanya kosa moja nalo ni kufanyia mzaha yale yaliyoandikwa katika Biblia kuhusu jinsi vile nambari zitakazopewa watu. Pia kosa la pili ni lile la kutaja nambari  inayozungumziwa katika bibilia ambayo imepigwa kama muhuri katika sehemu ya kulia aya ya uso kwa kutumiwa wino. Kwa kweli, maelezo haya yanayohusu matumizi ya mtambo wa microchips kuwekwa katika sehemu ya ngozi yanathibitisha yale yaliyoandikwa katika kitabu kitakatifu yapata karibu miaka elfu mbili hivi:

"Naye awafanya wote, wadogo kwa  wakubwa, na matajiri kwa masikini, na walio huru kwawatumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la  mnyama yule, au hesabu ya jina lake" (Ufu. 13:16-17).

La kusikitisha ni kwamba tafsiri mbali mbali za biblia hutaja tu nambari ambayo imewekwa sehemu ya kulia ya uso. Tafsiri ya kiingereza iitwayo The Living Bible hata inasema kwamba watu waliowekewa nambari, nambari hii itakuwa kama kitu fulani ambacho kimechomwa kwa ngozi (tattoo) Biblia ya Kiingereza tafsiri ya King James ni sawa kwa vile inaeleza chapa hii itawekwa ndani sehemu ya kulia ya uso. Sio tu juu ya uso (tattoo)

Tungependa kutaja hapa kwamba matumizi ya simu kutuma pesa (electronic transfer) haina lolote lililo maalum na kutia hofu. Ila pale   njia hii ya kutuma pesa itakapoanza kutumiwa na mpinga Kristo, yeye ataitumia kwa njia ya kunyanyasa watu akiwa na lengo la kujitimizia mambo yake mwenyewe. Yeye atawalazimisha watu wale kiapo cha kumtii kabla hawajapata chapa hii maalum. Kiapo hiki kitawataka wamtambue kuwa masiya, na mwishowe kuwa Mungu.

Hili ni jambo ambalo hakuna Mkristo anaweza kukubali kwa vile halilingani na mafunzo ya Biblia. Hatukubaliwi tukiwa wakristo kujiwekea alama wala kuingiza kwenye sehemu za miili yetu aina ya mitambo kama hii ya microchip. Katika Walawi 19:28 Bwana asema:

"Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kw ajili wafu, wala msiandike alama miilini  mwenu; mimi ndimi Bwana."

Kwa hivyo tendo kama hili ni tendo ambalo ni sawa na unajisi wa mwili ambao ni hekalu la Bwana, na hata katika 1 Kor. 3: 16 - 17, jambo hili latiliwa mkazo, na hapa tunakumbushwa kwamba miili yetu  wenye imani ni hekalu ya Bwana na hatufai kuchafua hekalu hii.

Sababu ya amri hii ni kuhakikisha kwamba hatujiingizi na kujiwekea alama za kishetani kwenye miili yetu.

Tabia Ya Mpinga Kristo

Mambo fulani ya muhimu kuhusu tabia ya mpinga Kristo yanatajwa na Mtume Paulo katika barua yake kwa Wathessaloniki. Anasema hivi: "Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana, haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu au kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafasi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu" (2 Thess. 2:3-4).

"Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa hata atakapoondolewa. Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumuangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake" (2 Thess. 2:7-8).

Hii ni hali ile ya kumuacha Mungu nyakati za mwisho na uasi dhidi ya Mungu na ufalme wake hapa duniani. Mtume Paulo anasema hivi katika waraka huu kwa waThessaloniki: "Mtu awaye yote asiwadanganye; maana haiji, usipokuja ule  kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu  wa kuasi, mwana wa uharibifu" (2 Thess. 2:3).

Kwa hivyo basi, tabia moja kuu ya mpinga Kristo ni ile ya uasi. Yeye atakuwa mtu asiyeweza kufanya yale anayotakiwa kufanya. Uasi wa kupita kiwango ndio mwenendo wake. Yeye atadharau kila sheria zilizoko, hata sheria za Mungu. Hata wakristo watataabika akwa ajili ya uasi wake. Kuhusu uasi wa huyu mpinga Kristo tunasoma hivi katika  kitabu cha Danieli:

"Naye atanena maneno kinyume chake aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na  sheria; nao watatiwa mkononi mwake kwa wakati na nyakati  mbili, na nusu wakati" (Dan. 7:25; soma pia Ufu. 13:6-7).

Rushwa na mengine mengi maovu yatakuwa natukio ya kila siku katika enzi yake. Wanaomuunga mkono watatendewa mazuri na kufanyiwa mapendeleo. Haya twayaona katika kitabu cha Danieli pia; ambapo tunasoma:

"Naye ataziteka nyara ngome zenye nguvu kwa msaada wa Mungu mgeni; na yeye atakayemkubali atamuongeza kwa utukufu; naye atawapa kumiliki wengi; naye ataigawa nchi kwa rushwa" (Dan. 11:39).

Hakutakuwa na kipimo cha uovu na uongo wa huyu mtawala dikteta. Hata pia anaitwa mwana wa kifo na mharibifu. (2 Thess 2:3). Rafiki yake mkubwa ambaye watasaidiana naye kutenda uovu ni nabii muongo naye atakuwa mwuaji na atakuwa akitumia nguvu za kishetani  kutenda uovu (Ufu. 13:15).

Ukisoma wa Thesssaloniki 2:7-8, utaona kwamba tayari  hali ile ya kutotii sheria yapatikana duniani. Hata hivyo nguvu hii inapingwa na Wakristo ambao ni taa, na pia chumvi ya dunia.

Hata hivyo, wakati wa mwisho, na kabla waKristo kunyakuliwa (rapture) na mwanzo wa dhiki, wengi waKristo walio na imani hafifu (nominal), yaani wale ambao hawajaokoka watajiunga na hawa waliomo kwenye ufalme wa giza. Twaambiwa hivi katika waraka wa Kwanza wa Paulo mtume  kwa Timotheo: "Basi roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani" ( 1 Tim 4:1).

Kutotii sheria, uasi, usherati na uchoyo ni mambo au matukio yatakayotokana na roho chafu ya uasi, ni roho huyu atajitokeza  kwa kabla ya muasi mkuu.

"Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wakujipenda wenyewe, wenye kuependa fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu, wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake, hao nao ujiepushe nao" (2 Tim. 3:1-5).

Kwa kweli, nyakati hizi ni nyakati za mwisho. Wako wengi ambao wanapotea. Wengi wanaojiita wakristo wanaukubali uovu, wanakubali pia hali ile ya kuwa na imani  hafifu. Wao wanashirikiana na wale waasi, na wasio na imani. Wao wanashirikiana na waovu katika kutenda mauaji na kuacha ukristo, na wanafungua njia kwa ajili ya usherati na, uchezaji kamare na yote ambayo ni ya uovu. Sasa hata siku ya jumapili haiheshimiwi kuwa ni siku ya maombi.

Baadaye muasi mkuu, mvunjaji sheria, mwuaji, muongo anayejiita Mungu atajitokeza. Je? wewe unampinga muovu huyu, au unamfungulia njia ili ajitokeze? Tungependa kuwasihi wakristo kwamba wasichoke wala kufa moyo wakati huu kwa ajili ya shida zilizoko ambazo zaletwa na muovu ila waendelee kupinga uovu. Juu ya dhiki, Yesu Kristo alisema hivi  jinsi vile imeandikwa katika  Mathayo: "Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini atakayevumilia hadi mwisho, ndiye atakayeokoka" (Mt. 24: 12-13).

Uovu usio na kifani, roho ya kutaka kutenda dhambi, na kutotii sheria; haya yote yatajitokeza wakati wa dhiki kuu.

Mwenye dhambi ambaye ataihadaa dunia.

Filosofia Ya Mpinga Kristo

Msingi wa filosofia ya mpinga Kristo ni pesa. Filosofia yake kuu ni ile ambapo pesa ndicho kitu cha muhimu zaidi ya vyote. Utaratibu wake wa kidini, kisiasa na kiuchumi ni ule ambapo  kila kitu kinachukuliwa kama ni kitu  moja yaani monism: Katika Ufunuo 13, ulimwengu huu ambao umegawanyika hivi sasa utaungana na kuwa ulimwengu wa majivuno, pamoja na haya utakuja kuwa  chini ya uongozi wa mpinga Kristo.

Twasoma hivi: "Na ulimwengu wote ulishangazwa na kumfuata mnyama. na wote walioko duniani watamshujudu" (Ufu. 13.3, 8).

Mpinga Kristo atajenga nchi moja kote duniani na atafanya hivyo kupitia kuondoa mipaka ya kimataifa ambayo iko hivi sasa. Kando na kuondoa mipaka, mpinga Kristo atajenga uhusiano wa karibu kupitia makubaliano na makundi mbali mbali. Matokeo ni kwamba  tutakuwa na  kundi moja la watu duniani.

Kutakuwa pia na siasa mpya New World Order itakayosimamiwa na serikali ya kimataifa ambayo itasimamia uchumi wa dunia kutoka makao makuu ya kimataifa. Muungano wa dini mbali mbali yaani Ecumenical Movement utaleta au utakuwa msingi wa Muungano wa dini mbali mbali.

Muungano huu wa dini mbali mbali utashirikiana kwa karibu sana na serikali za kimataifa. Mwenendo huu utawafanya watu wajione kuwa wenyeji halisi wa dunia. Mawazo ya kila mmoja yatabadilishwa kwa kutumia mbinu mbali mbali maalum kama vile Transcendental Meditation, na watu watajiingiza katika mambo haya na kujiona kwamba wanajielewa zaidi na wanajielewa kwa hali ya juu. Wao watajiona kwamba hata mungu yuko ndani yao.

Yule anayeamini na kufanya haya yote, yeye atajiona kuwa yuko katika laini na kile ambacho kinatoa nguvu (cosmic energy), na hii itamuwezesha kunena kwa njia maalum ambayo ni telepathy, extra- sensory perception, astral travel, na self healing.

Wakati ule wa kutabasamu (meditational trance), yule anaye tabasamu atajisikia kuwa katika hali ya utulivu, hata kuona yote yaliyoko kwenye anga (cosmos) kuwa ni kitu kilichounganisha vitu tofauti na kuwa kama kimoja.

Uwezo wake wa kutumia akili (mental) utapanuka, na hapo kuwa mwanzo wake kuona vyote kuwa kama kimoja. Dunia na vyote vya asili kuwa miujiza ya uganga (mystical) na vitakatifu (divine). Mimea, wanyama na wanadamu kwao ni vitu tofauti vinavyohusiana ambavyo viliumbika kupitia njia ya evolution, na kwamba vyote vina utukufu ambao umepita kwa vyote na kuvifanya kuwa kama kitu kimoja.

Katika kiwango cha juu sana cha kuumbika kwa vitu (evolutionary development), walio katika kikundi hiki, uwezo wao kuelewa utazidi sambamba. Yule ambaye ameingizwa katika kuelewa mambo ya nuru za anga (cosmic powers) yeye atakuwa na uwezo  wa kutenda  miujiza, na atajua siri zote za anga. Yeye atakuwa mkuu ajuaye kila aina ya ujuzi (wisdom) na huenda baadaye akafikia kiwango cha Kristo.

Inaaminika kwamba mtu kama huyu ambaye anajua mengi na anaweza kuzifanya anga (cosmic powers) kutenda dunia mpya (Utopia of the New World Order) wakati huu huitwa enzi ya Aquarius. Huyu atakayejitokeza atakuwa mpinga Kristo ambaye ni mnyama (beast) katika Ufunuo.

Kwa vile mpinga Kristo ndiye kiongozi wa mabadiliko ya kimawazo, lazima tuelewe kwamba imani iitwayo New Age mysticism ambayo wakati huu imejitokeza, na kuendelezwa kuwa sawa na imani, sio dini na kusemekana  kuwa njia hii ya kuwaza itafungua mlango ili uwezo wa mwanadamu katika mambo mengi uongezeke. Wazo kama hili ni la kishetani. Nia ya haya yote ni kumuandaa kila mwanadamu ili amuabudu mpinga Kristo na shetani.

Maandishi matakatifu yanasema hivi: "Kwa hivyo wakaanza kuabudu yule joka ambaye alimpa mamlaka na madaraka yule mnyama (Beast), na wakamuabudu mnyama huyu wakisema 'Ni nani kama mnyama huyu?" (Ufu. 13:4).

Onyo lililoko hapa liko wazi: Usijaribu kufanya majaribio ya mambo ya anga na sayari na vile vilivyomo. Kwani vyote ni vya shetani. Vyote ni adui katika vita vya kiroho. Na katika Waraka wa Mtume Paulo kwa Waefeso, yeye anaeleza zaidi: "Kwa vile vita vyetu si juu ya miili yetu na damu, lakini dhidi ya nguvu kuu, na watawala wa giza, na roho chafu katika mbingu" (Efe. 6:12).

Muombe Mungu ili aweze kukusaidia uwe na uwezo wa kujua tofauti ilioko kati ya ufalme wa mbinguni na ule wa shetani.

Shetani na malaika wake wanafanya kila wawezalo kukunyang'anya uwezo wa kutofautisha kati ya zuri na baya, na anafanya hivyo kwa kukuhadaa kwamba kila kitu, vyote vilivyoko ni moja. Mabali na haya,  Mungu kupitia roho Mtakatifu, anataka uwe na uwezo wa kujua wazi yaliyo mazuri, na yale mabaya.

Anataka uweze kujua ni yapi ya taa na ni yapi ya giza, mbinguni na jehenamu, njia nyembamba na kubwa, zuri na baya, ukweli na uongo, dini ya kweli na dini ya uongo.

Tuna utaratibu ambao unafuatwa wa kukuwezesha ambao utakusaidia kutofautisha kati ya wema na uovu. Filosofia ya muovu mpinga Kristo yaweza kueleweka ukilinganishwa na kufananishwa na jinsi vile waKristo wanavyoona yale yale ya dunia, kwa vile mpinga Kristo ana muelekeo wa uongo ambao anataka wafuasi wake wafuate.

JINSI VILE MKRISTO ANAELEWA DUNIA

(Christian world-view:

antithetic)

JINSI VILE MPINGA KRISTO ANAELEWA DUNIA

(Anti-Christian world-view: synthetic)

1. Jinsi kufikiria na kujiamulia mambo tofauti. Njia ya kuwaza ambayo inatilia maanani kwamba lazima kuwe na tofauti katika mambo mbali mbali.

1. Yahusu jinsi kufikiria na kuwaza kwa njia  ambayo haitilii maanani kwamba kuna tofauti katika mambo yote. Na  hapa linatiliwa mkazo ni kwamba vyote amabavyo ni tofauti vyawekwa kuwa pamoja na kuwa kitu kimoja. Philosophia hii huitwa holism.

2. Kutaendelea kuwa na tofauti kati ya mwanga na  giza. Mwanga na giza haviwezi kusikilizana.

2. Pale  mkazo utapoendelea kutiliwa umuhimu wa kuleta vyote pamoja, kuna wakati ambapo vyote vilivyoko kwenye anga (cosmos) vitakuja pamoja na kuwa kama kitu kimoja. Kutoelewana, na mawazo yanayotofautiana yatasemekana kwamba yametokana  na kutokuwa na fahamu bora (ignorance).

3. Mambo ya mashetani hayakubaliwi, majaribio yanayohusu nguvu za uchawi (occult) na pia matumizi ya zile sehemu zisizo za kawaida (extra-sensory perception) havikubailiwi.

3. Maendeleo ya kuendeleza ujuzi wa mambo ya anga (cosmic consciousness), kwenda mbele hatakupita mipaka ya yale yasiyoeleweka yatatiliwa mkazo.

4. Imani katika Mungu mmoja (monotheism) Mungu mwenye utatu anakaa mbinguni. Lazima aonekane na kuabudiwa akiwa katika ni tofauti na mbali na viumbe vyake. Mungu anafanya kazi katika mwanadamu kupitia roho mtakatifu, naye huyu roho mtakatifu ana utu wa kivyake ambaye lazima akaribiwe na kwa utiifu.

4. Imani katika Mungu wengi (pantheism) Mungu ni wa ajabu (mystical), na hajali watu (impersonal), na kila kiumbe ni Mungu. Kwa vile watu ni watakatifu, lazima wajifahamu zaidi (conscioussness), na hivyo kumgundua Mungu aliye ndani yao.

5. Mwanadamu ni kiumbe maalum na cha kipekee cha Mungu. Mwanadamu yuko mbali  na tofauti kabisa na vyote vilivyo duniani. Mwandamau ameamriwa na Mungu Kusimamia na kutawala dunia, na pia kuibadili na kufanya dunia iwe ya kumfaa. Pia ni yeye atatawala viumbe vyote. Ana jukumu la kuimarisha na pia kutunza na kulinda mazingira yake.

5. Mwanadamu ni sehemu moja ya vile vyote vilvyoumbika kwa kufuatia utaratibu ulio asili duniani. Yeye mwanadamu alitokea kwenye sokwe kwa njia ya  ya kubadilika iitwayo evolution. Lazima mwanadamu ajione kuwa sehemu moja ya viumbe asili duniani, na ni sharti asiharibu na aendeleze uhusiano huo kati yake na viumbe duniani.

6. Mwanadamu ana maisha aina moja akiwa hai. Kuna wakati ataaga dunia mara moja, baada ya hapo atahukumiwa, na maisha ya milele au hukumu kufuata.

6. Mwanadamu ana maisha mbali mbali (cycles) yeye hupanda ngazi kutoka maisha aina moja kwenda ngazi ya juu. Kwa njia ya  kurudi kuwa nasi baada yake yeye kufa. Na baada ya kifo,  yeye huanza maisha mapya duniani.

7. Wote wenye uhai duniani wanaweza kuwekwa kwenye vikundi viwili. Kikundi cha kwanza ni kile cha waliookoka ambao wataenda mbinguni, na kile cha wale ambao hawajaokoka ambao wataenda jehenamu (hell). Wale walio katika giza la kiroho wanaalikwa kuingia katika ufalme wa Mungu kupitia njia ya kuzaliwa mara ya pili.

7. Umoja katika familia ya wanadamu lazima uonekane katika imani  na dini. Dini zote lazima zikubali kwamba wana Mungu mmoja. Kwa hivyo hakuna dini moja itakayojiona kuwa bora zaidi kuliko dini tofauti. Vyombo  lazima vianzishwe kuleta umoja huo kati ya dini mbali mbali.

8. Kwa vile kuna imani mbili ambazo zinatafautiana kuhusu ufalme wa baadaye, na kila moja yazungumzia juu ya mfalme atakaekomboa ulimwengu, mflame wa kweli, Kristo na yule mfalme Mpinga kristo, lazima uchaguzi ufanywe, yaani lazima mmoja kati ya hawa wawili achaguliwe.

8. kwa ajili dini zote zimetokana na ujuzi (wisdom) ulio na msingi mmoja - msingi wa sayari na anga (cosmic wisdom), dini zote zinasubiri na kungoja Kristo atakayetoka kwenye msingi huu wa sayari (Cosmic Christ). Naye huyu Kristo ataunganisha dini na imani mbali mbali kuwa kama moja. Dini na  wafuasi wa imani mbali mbali lazima waungane pamoja kujiweka  tayari kwa ajili ya  kuja kwake.

9. Mwanadamu ni muovu, na tayari hana uhai wa kiroho, na hii ni kwa ajili ya kuanguka pale shambani Edeni. Kama mwanadamu yeyote hazaliwi mara ya pili, ataingia ziwa la moto.

9. Mwanadamu ni mwenye wema, na anatenda tu maovu kwa ajili ya mambo fulani katika mazingira yake yanayomlazimisha kufanya hivyo. Hakuna shetani wala Jehenam (Hell) popote duniani (universe).

10. Kupitia maombi, dhambi zako zaweza kuondolewa kupitia kwa Mwokozi wetu yesu kristo. Hapa mapenzi na upendo wa Mungu utaingia katika moyo wako kupitia kazi yake roho matakatifu. Hakuna chochote ambacho kitachukua nafasi  ya maombi. Kutafakari (meditation) ni njia ya maombi iliyo mbaya (counterfeit) ambayo chanzo chake ni Transcendental Meditation.

10.  Kupitia njia ya kutafakari kwa upole (quiet meditation), na kufunga kabisa sehemu za mwili za kupokea mawazao kuingia katika ubongo sehemu ya kulia, mtu anaweza kujenga uwezo wa kuelewa (consciousness). Hapa utaweza kuwa mmoja na Kristo ndani yako, na hapa utapata amani na kuwa na starehe ndani yako.

11. Wakristo wanapoungana pamoja katika maombi, roho mtakatifu anafanya kazi yake  na nguvu zaidi kuwaonyesha watu makosa yao na kuwaokoa.

11. Watu wengi wanapotafakari (meditate) wakati mmoja, basi nguvu maalum hujitokeza (cosmic energy), na nguvu hizi huleta na kuendeleza amani ambayo itaendeleza amani duniani.

12.  Masikilizano (reconcialiation) kati ya mwanadamu  na Mungu hutokea tu pale msalabani, na hutokana na sababu Kristo alikufa pale msalabani kwa ajili na badala ya mwanadamu. Masikilizano kati ya wanadamu yanatokana na wanadamu kusikiliza na kuheshimu haki ya wenzao, kupitia mazungumzo kusuluhisha mizozo na kuheshimu mipaka.

12. Masikilizano kati ya watu mbali mbali au mifumo ya siasa (ideologies) na hata imani inatokana na kuelewana, kutoa mipaka, na umoja. Vikundi vya watu lazima vitupilie mbali hali ya kuwa bila umoja (exclusivity) na kukubali kuendeleza hali ya kuwa pamoja.

13. Yesu Kristo ni mwana wa Mungu aliye hai, na atarudi tena kutoka mbinguni kuchukua mchumba wake kutoka duniani hapa kwenye ufisadi na kumpeleka katika mji mpya Yerusalemu. Baada ya miaka saba, atarudi tena na nguvu na utukufu kuhukumu mataifa na kutawala katika ufalme wake hapa duniani.

13. Mpinga Kristo ni mwana wa  kishetani  (perdition) ambaye atatoka  kwa wale walioanguka. Wafuasi wa dini za uongo watakuwa ndio wachumba wake nao watatawala naye kutoka Babeli. Baada ya miaka saba, utawala wake utamalizwa, na wafuasi wake kuangamizwa atakaporudi mfalme wa wafalme.

 

Mpinga Kristo Anaelekea wapi?

Kuhusu ni wapi mpinga Kristo anaelekea, muongo na mtawala wa kimabavu, Biblia inasema wazi. Mtume Paulo anasema hivi katika Wathesalonika: "Mungu atamumaliza na pumzi kutoka kinywa chake, na kumuangamiza kabisa na mwanga atakaokuja nao" (2 Thess. 2:8).

Mtume Yohana pia anataja tukio hili kuwa moja ya matukio muhimu kabisa wakati wa kurudi kwa Kristo. Anasema hivi katika Ufunuo: "Basi yule mnyama akashikwa mateka, pamoja naye yule nabii wa uongo ambaye alifanya maajabu, maajabu aliyoyatumia kuhadaa dunia. Na sana wale waliokuwa wamewekewa alama ile ya ibilisi shetani, na pia kuabudu picha yake. Hawa wawili watatupwa katika ziwa la moto" (Ufu. 19:20).

Haya pia yanawangoja wale ambao wameungana na mpinga Kristo katika uovu wake, na pia kusujuduu (worship). Kutakuwa na wengi ambao, kwa sababu huyu nabii wa uongo na wale wanaofanya kazi nao katika dunia ya uongo na katika kanisa la dunia ya uongo, na wengi watakuwa wamedanganywa hata kuanza kumuabudu mpinga Kristo.

"Ikiwa mtu awaye yeyote akimsujudu mnyama huyu na hata sanamuyake, na kuipokea katika  kipaji cha uso wake, au katika mkono yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa kikombe cha kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za mwanakondoo. Na moshi wa  maumivu yao hupanda  juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake" (Ufu. 14:9-11).

Hakuna awezaye kupuuza onyo hili, akidhaniya kwamba kwa ajili ya kutaka kufaidika kisiasa, au kuepuka shida ambazo wakati wa dhiki kuu, anaweza akakubali kuwekewa alama na baadaye kuiacha na kuitupilia mbali baadaye.

Wale watakapowekewa chapa hii kwenye vichwa vyao au kwenye mikono yao wanauza roho zao kwake shetani kwa kumkubali huyu mpinga Kristo kuwa mungu wao. Jambo moja ambalo ni wazi kabisa ni kwamba huyu mpinga Kristo hatampa yeyote nafasi ya kukwepa baada yake kukuwekea  chapa hii.

Kuna amri moja tuu ya muhimu kuhusu mpinga Kristo huyu, nayo ni: mtupilie mbali mpinga Kristo, hata ikiwa msimamo wako huu unaweza kukuletea mauti.