Sehemu moja ambayo inatajwa na kutiliwa mkazo sana ni mbinguni , sehemu iliyo kwenye kiti cha enzi cha ufalme. Sehemu nyingi katika ufunuo huanza na maneno haya: "Baada ya hayo…." Maneno haya yana maana kwamba yale yaliyo katika ufunuo ni matukio ambayo yanafuatana kwa utaratibu fulani.
Pale Mtume Yohana anaposema katika Ufunuo 4:1 hivi: "Baada ya hayo...." hii ina maana yale ambayo anataka kugusia yanafuatana na yale ambayo yametangulia kuhusu kanisa duniani. Kwa hivyo tukianza na kifungu cha nne kuendelea, yale ambayo tunataja ni yale yatakuja kutokea baadaye.
Ili aweze kuyaona kwa ukamilifu yale yatakayotokea, Mtume Yohana alichukuliwa hadi mbinguni katika ndoto. Alisikia sauti ilio sawa na baragumu ikisema: "Baada ya hayo, naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami; ikisema, panda hata huku nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo" (Ufu. 4:1).
Wateule wa Mungu nao pia hivi karibuni watasikia sauti kama hii ikiwaita pale Kristo atakapokuja mara ya pili kuwachukua.
"Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi farijianeni kwa maneno hayo" (1 The. 4:16-17).
Tunapotaja mambo yanayohusu unabii, ni lazima maneno haya yaelewekeke vyema kabisa. Kwa mfano neno la kingereza linalotumiwa katika WaThessaloniki ni “caught up” neno hili limetafsiriwa kutoka Kiyunani, na lenyewe ni "harpazo."
Mmoja wa watalaam wa mambo ya tafsiri Bwana K. S. Wuest, anasema maana yake ni “kunyakua,” au “Kuchukua kwa ghafla,” au “Kuchukua kuwa sawa na kitu chako.” Mtaalam huyu anaendelea kusema kwamba neno lenyewe lilitumiwa kama msemo ulio na maana kwamba “kuepusha mtu bala au taabu ya namna fulani.” Neno hili la Kiyunani pia limetumiwa katika Mt. 11:12; 13:19; Yn. 6:15; 10:12, 28:29; Mat. 8:39; 23:10; 2 Kor. 12:2; 4; 1 The. 4:17, Yud. 5:23, na Ufu.12:15.
Njia bora sana ya kuelewa maandishi ya unabii ni kusoma kila sehemu ambapo neno lenyewe limetumiwa, na kuomba Mungu akufungulie ili uweze kuelewa vyema yaliyomo.
Neno hili ambalo tumetaja "harpazo" limetafsiriwa katika maandishi matakatifu kwa njia zifuatazo:
· Nyakua (Mat. 13:19).
· Chukua kwa nguvu (Yoh. 6:15).
· Chukua kwa nguvu kutoka kwenye kikundi (Mdo. 23:10).
· Shikwa na kuchukuliwa ( Mdo. 8:39).
· Shikwa juu (2 Kor.12:2; 1 The. 4:17; Ufu.12:5).
Tafsiri ambayo ina maana “shikwa juu,” na “shikwa na kuchukuliwa,” ambayo imetumiwa hapa katika vitabu vya matendo ya mitume, Wakorintho, Ufunuo na Wathesaloniki vyaeleza wazi maana ya jambo hili lenyewe.
Ishara maalum kwamba kunyakuliwa kutatokea kabla ya dhiki kuu yapatikana katika Luka 21. Twasoma hivi: "Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika hayo yote yatakayotokea, na kusimama mbele ya mwana wa Adamu" (Lk. 21:36).
Utaratibu ambao umefuatwa katika Ufunuo waonyesha wazi kwamba kanisa litatukuzwa kabla muhuri wa kwanza kufunguliwa wakati wa dhiki. Tukiangalia mambo haya na kuyalinganisha na yale yanayoendelea duniani wakati huu, kunyakuliwa kutakuwa njia moja ya kuwawezesha wakristo waepuke dhiki kuu.
Kabla ya tukio hili la wakristo kunyakuliwa, kutakuwa na shida nyingi sana ambazo zitawakumba waKristo, na kufanya wale wenye imani kamili kupitia katika majaribu mengi na shida za aina aina. Wakristo hawa watafanyiwa dhihaka, na kudharauliwa. Wataitwa manabii wa uongo pale watakapokuwa wakiwaonya watu kuhusu hukumu inayowangoja waovu wasio na imani, na hasa wafuasi wa mpinga Kristo. Pia wataitwa waasi pale watakapokataa kujiunga na jumuia ya makanisa itakayojitokeza. Ikiwa wataendelea kuwa na imani, na kutenda yale yanayomfurahisha Mungu kulingana na maagizo yake, yeye (Mungu) atawachukua kupitia njia ya kunyakuliwa kabla ya mpinga Kristo kujitokeza wakati wa mwanzo wa dhiki kuu. Ahadi hii imetolewa katika waThesaloniki:
"Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake. Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa. Hapo ndipo atakapofunuliwa yule muasi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake" (2 The. 2:6-8).
Wale ambao hivi sasa wameanza kufuata utaratibu wa kidini uitwao New Age au enzi mpya kamwe hataweza kuepuka hukumu. Ni dini aina ambazo baadaye zitakuwa mwanzo wa dini moja ya kimataifa itakayoongozwa na mpinga Kristo. Wafuasi wa dini hii hawataepuka dhiki kuu. Katika 1 WaThessaloniki 5:3 twasoma hivi: "Wakati wasemapo, kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa" (1 The. 5:3).
Katika somo hili, ni wazi kwamba wako wale ambao wataepuka dhiki kuu, nao wengine ambao hawajamrudia Mungu hawataweza kuepuka dhiki kuu. Wazo hili lakubaliana kabisa na lile ambalo lapatikana katika Yohana 5:24 kwamba wale walio na imani katika Yesu Kristo hawatahukumiwa ila watapita moja kwa moja kutoka kifo hadi maisha ya milele.
Ingawa kunyakuliwa kwa wenye imani ni jambo lisilo la kawaida kabisa, maandishi matakatifu yana ujumbe kuhusu jinsi ambavyo Mungu alipomwaga duniani hasira yake, na akawaepusha wale walio na imani ya kwelia dhiki iliofuata. Katika Mwanzo 6:13-14, twasoma jinsi vile Mungu alimuokoa Nuhu. Twasoma hivi: Kabla ya hukumu, wale wanane walio na imani waliingia katika safina. Mungu nwenyewe alifunga mlango kabla ya kuwahukumu wenye dhambi (Mwanzo 6:16-23).
Wakati wa Lutu, wenye imani pia waliokolewa. Usiku kabla ya Sodoma na Gomora kuangamizwa, waliamuriwa waondoke Sodoma na kukimbilia milimani. Malaika walitilia mkazo jambo moja kwamba, hawangeangamiza miji hii pamoja na Lutu na familia yake. Miji hii iliangamizwa pale walipoondoka (Mwanzo 19:13-25).
Biblia yasema wazi kwamba kuna uhusiano wa karibu kati ya matukio haya na jinsi ambavyo Mungu atakavyowatendea wenye imani na wale ambao hawana imani siku za mwisho. Katika Luka 17:26-30 twasoma hivi:
"Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu,ndivyo itakavyokuwa siku zake mwana wa Adamu. Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata ile siku Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote. Na kadhalika, ilivyokuwa siku za Lutu, walikuwa wakiila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga; lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma, kulinyesha moto na kiberiti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu" (Lk. 17:26-30; soma pia Mwanzo 6 na 19).
Matukio ya zamani na yale ya siku hizi yanafanana kwa njia hii:
· Wakati wa Nuhu na Lutu tabia ya kuvunja sheria ilikuwa imeenea sana. Watu hawakuheshimu maadili na mila zao, uzinzi ulizidi katika jamii. Pale watatu walipokosa kukubaliana, basi wao walitumia nguvu kutatua ugomvi. Na mambo kama haya ndiyo yatakayotokea siku za mwisho hapa duniani.
· Wakati wa Nuhu na Lutu, imani ya wengi ilikuwa imefifia sana. Wengi walikosa imani ya kiroho, hata mienendo yao ikawa haimbatani na maadili ya kijamii. Ulafi, magendo na ulaji rushwa ulienea sana katika jamii. Hata leo siku za mwisho zitakuwa hivyo.
· Wakati wa Nuhu na Lutu, watu walipenda mali sana kuliko vyote, na maisha yao yakawa yale ambayo hayana heshima hata kidogo. Wengi walitenda dhambi kama vile uzinzi, na kuonana kimwili waume kwa waume; wake kwa wake. Katika siku za mwisho kutakuwa na haya pia.
· Wakati wa Nuhu na Lutu, watu waliwadharau sana na kuwafanyia mzaha waKristo. Watu walidharau sana maonyo ya kinabii yaliyo katika maandishi matakatifu. Waliyachukua haya kuwa upuzi, na kundelea na maisha yao hayo ya uovu. Mambo yatakuwa hivi tena siku za mwisho.
· Wakati wa Nuhu na Lutu, Mungu aliwapa nafasi wenye dhambi watubu. Wao walikataa kutubu sana dhambi zao na hapo wakawa wamejihukumu wenyewe. Ni wao wenyewe walistahili kujilaumu kwa ajili ya yale yaliyowakumba. Ni hivyo yatakavyokuwa siku za mwisho.
· Wakati wa Nuhu na Lutu, Mungu aliwapa nafasi ya kuepuka wale waliokuwa na imani. Utaratibu ulikuwa kwamba, kwanza wapewe onyo wale wanaotenda uovu kuhusu hukumu inayokaribia, na baadaye kuwasaidia walio na imani kuepuka hukumu. Mambo yatakuwa hivyo siku za mwisho.
· Wakati wa Nuhu na Lutu, hakukuwa na njia yeyote ya wale wenye imani hafifu kujikinga. Mke wake Lutu ni mmoja wa wale waliokuwa na imani hafifu. Kwa inje, alikuwa na imani, lakini ndani, hakuwa na imani kamili. Yeye hakuwa amekomaa kiroho. Imani hii hafifu ilikuwa na matokeo kwamba alikufa. Siku za mwisho, itakuwa ni hivyo hivyo.
· Wakati wa Nuhu na Lutu, balaa kuu ilikumba dunia pale tu wenye imani walipoondoka. Vifo na uharibifu ulikuwa ni wa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana katika historia ya dunia. Ndivyo mambo yatakvyokuwa siku za mwisho.
· Wakati na Nuhu na Lutu, wasio na imani hawakujua ni yapi mema yaliokuwa yamewakaribia kwa ajili ya wale wenye imani kati yao. Mungu alikuwa tayari kuwapa msamaha wenyeji wa mji mzima kwa ajili tuu ya wenye imani kumi. Pale wenye imani na waishio katika mwanga walipochukuliwa, basi giza nene la kiroho lilijitokeza na hii ikamkasirisha sana Mungu. Ni hivyo mambo yatakavyokuwa siku za mwisho.
· Wakati wa Nuhu, watu waliwafanyia mzaha walipokuwa wakijenga safina: wasitambue hata gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu. (Mt. 24:39).
Muda mfupi baada ya kunyakuliwa wenye imani, wengi ambao watakuwa na hofu, watajaribu kueleza tukio hili kwa njia mbali mbali. Jambo hili litakuwa la kushangaza zaidi pale itakapogunduliwa kwamba kati ya wale ambao wameachwa ni wakristo walio na imani hafifu, makasisi wenye sifa kubwa, na wasomi maarufu wa mambo ya kidini.
Uongo utakaojitokeza kueleza tukio hili utakuwa wa kiwango ambacho hakijaonekana duniani. hapo mwana mrithi wa ufalme wa amani (prince of peace) aliye na uwezo mkubwa sana wa kubadili mambo duniani atajitokeza. Hapa yeye ataweza kuwashiwishi na kupata wafuasi wengi sana duniani.
Mtume Yohana alikuwa juu mbinguni aliposikia sauti kama tarumbeta ikisema: "Na mara nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa juu mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti; na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ikionekena mithili ya zumaridi. Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu" (Ufu. 4:2-4).
Utukufu aliouona Yohana ulikuwa wa ajabu. Yeye aliweza kuulinganisha na vitu vya thamani kubwa sana kama vile maadini. Maelezo haya yanapatikana katika Ufunuo 21:11. Usafi kamili wa Mungu waweza kuelezwa kwa njia hiyo hiyo. Mawe ya Sardius ni ya rangi nyekundu, na hii ni sawa na damu ya Mwokozi wetu Yesu Kristo. Ile rangi ya kijani kibichi inayozingira kiti cha enzi ni sawa rangi ilio sawa na uzima wa milele ambao tunao kupitia Kristo. Rangi hii ya kijani kibichi ni rangi ya uhai. Nao ule mviringo unazingira kiti cha enzi waelekea maisha ya milele.
Wale wazee 24, na taji katika vichwa vyao, wao ndio kanisa la Kristo. Wanajitambulisha pale Yohana anaposema: Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri yake; kwa kuwa ulichinjwa ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa (Ufunuo 5:9). Wao ndio wakristo walionunuliwa na damu kutoka mataifa yote duniani, na wao watapokea miili mipya wakati wa kuzaliwa mara ya pili. Wote walio mwili wa Kristo watajikusanya mbele ya kiti cha enzi ili kushirikiana na mungu kuhukumu walio duniani wakati ule wa dhiki kuu (1 Kor. 6:2).
Wakuu na wazee (elders) katika Agano Jipya ni watu ambao wameokolewa na Kristo, na ambao wamejitoa kumtumikia. Nayo nambari hii 24 ina maana maalum. Katika 1 Nya. 24 Mfalme Daudi alichagua familia 24 ili zihudumu katika hekalu. Kila familia ilihitajika kuhudumu kwa muda wa wiki mbili kila mwaka kulingana na utaratibu maalum ulioandaliwa. Katika 1 Pet. 2:9, kila mwenye imani anaitwa "ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu.” Mzee ni mtu ambaye ameitwa na akakubali wito wa kumtumikia Bwana.
Je, wewe umekubali wito ulioupokea ukiwa Mkristo? Je, umepokea kipawa cha kiroho cha kukuwezesha kutimiza yale uliyoitiwa?
Wazee wale 24, kila mmoja amevaa taji la dhahabu kichwani, na hii ndio ishara maalum kuonyesha wazi kwamba wamepewa kumhudumia Bwana, na kwamba wamevishwa taji hizi na Mwokozi Kristo mwenyewe (Ufu. 22:12). Kwenda mbele yake bila chochote ulichokitimiza katika kazi yako ya huduma ni sawa na kuficha talanta uliyopewa na kuja mbele ya Bwana bila chochote (soma 1 Kor.3:15; 2 Kor. 5: 10; Gal. 6:9; 1 Yoh. 2:28; Ufu. 22:12). Uzee ni sawa na uchungaji, kwa vile zote huhusu imani na matendo. Matendo yenyewe sio yale ambayo yametokana na ujuzi na nguvu za mtu binafsi, ila ni yale ambayo yametokana na kutimizwa na mtakatifu. Lazima tujihadhari ili tusije tukachukua matendo ya mtu kuwa sawa na wokovu. Katika Waefeso twasoma hivi:
"Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yeyote asije akajisifu" (Efe. 2:8-9).
Hata hivyo, baada ya kupokea wokovu, tunahitajika kuishi maisha ya imani na matendo yanayonekana. “Maana tuu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo." (Efe. 2:10). Ni kwa ajili ya kazi aina hii wazee watapokea taji. Biblia imetaja taji zifuatazo ambazo mkristo anaweza kupokea:
· Taji la kufurahia kazi ya kuwaleta watu katika ufalme wa mbinguni (1 The. 2:19; Flp.4:1).
· Taji la uzima kwa wale wanaokufa kwa ajili ya imani yao (Yud. 1:12; Ufu. 2:10).
· Taji la utukufu kwa wachungaji bora (1 Pet. 5:4).
· Taji kwa ajili ya maisha bora yasiyo na dosari (1 Kor. 9:25).
· Taji la utukufu kwa wale wanaofurahia kuja kwake (2 Tim. 4:8).
Baada ya kuwaokoa wote walio na imani safi walio katika kanisa la kweli, Mungu ataadhibu wote ambao wamemkataa, na hapo kuokoa ulimwengu kutoka minyororo ya uovu wa giza. Ufunuo 5:1-5 ni utangulizi wa matukio ya kuwaokoa wanadamu katika wakati ule wa miaka saba ya dhiki kuu. Jambo hili limetajwa kulingana na jinsi vile waIsrael huzungumzia mambo ya kuokolewa wanadamu siku zamwisho. Mfano wake wapatikana katika kitabu cha Ruthu.
Naomi pamoja na familia yake, yaani bwana na wana wake 2 wa kiume walihamia Moabu kutoka Bethlehemu ili kuepuka janga la njaa. Jinsi hii pia, mwanadamu anajikuta katika jangaa kuu baada ya kuanguka kule Edeni. Na kwa ajili hiyo, haki nyingi za mwanadamu juu ya mali amepokonywa. Hata leo, sisi wanadamu ni wasafiri katika dunia ambapo tunapigana vita na nguvu za giza kuu (Efe.6:10-13).
Wakati alipokuwa mkimbizi, watoto watatu katika familia ya Naomi walikufa, na mmoja akaamua kubaki nyuma. matokeo yakawa ni wawili tu waliweza kufurahisha Mungu na kurudishiwa mali yao.
Kwa kweli ni wengi hufa wakiwa bado wangali safarini wakiwa wenye dhambi. Nao wale ambao wanapokea wokovu, na kuweka imani yao katika Kristo hupata uamsho wa kiroho.
Tukirudi Bethlehemu, Naomi na mke wake walipata shida kubwa sana. Deni lilibakia katika shamba lao lilikuwa kundi kubwa mno. Iliwabidi wamtafute mtu katika ukoo wao ambaye angeweza kulipa deni hilo ili wasinyang’anywe mali hii. Na yule atakayefanya hivyo atalazimika kumchukua Naomi kuwa kama mke wake ili kuendeleza ukoo huu. Boazi ndiye aliyepatikana kuwa na uwezo wa kufanya haya. yeye alilipa deni, na kumchukua Ruthu pamoja na mkwe wake kutoka Moabu. Ruthu na Naomi walifurahia sana yote Boazi alifanya. Yeye aliwaokoa nakufanya jina la ukoo huu liendelezwe ili watu wa inje wasiangamize ukoo huu.
Ni Yesu Kristo ambaye ametuokoa. Ni yeye alichukua mzigo wa dhambi zetu na kuulipia vikamilifu. Na kwa ajili ya mapenzi haya, sisi ni warithi wa ufalme pamoja naye. Kando na hayo, ametuchukua sawa na Ruthu kutoka nchi ya mbali kuwa kama mchumba wake. Ni jambo la kupendeza sana kupita kiasi kwamba Mungu ametuchagua, akalipa deni letu na kutufanya watoto wa Mungu, ili tufurahi milele daima.
Wakuu wale wazee walifurahi sana kusikia kwamba Kristo ni mmoja wao katika ukoo, atawaponya, amelipa deni la dhambi zao, na kwamba ataokoa ulimwengu wote. Na kwa ajili hii, kuambatana na yale yaliyo katika Mwanzo 1:28; watarithi dunia na kutawala na Kristo. Kwa hivyo yale yaliyotokana na uasi ule wa mwanzo hayatawakabili (1 Yoh. 5:19).
Katika taifa la Israeli, ilikuwa ni desturi kuandika kwenye sehemu maalum rekodi za urithi wa mali katika jamii. Baada ya maandishi kuwekwa, ilikuwa kawaida kufunga kabisa karatasi hiyo iliyotumiwa kuweka stakabadhi hizo. Nasi tulio wenye imani, haki yetu kama warithi wa dunia yote imeandikwa kwenye stakabadhi na kufungwa kabisa na mihuri saba. Ni Kristo anayeweza kufungua mihuri hiyo. Ulimwengu wote ni wake, na pia ni yeye ambaye amelipa malipo ya kutuondolea dhambi zetu zilizoletwa na uongo wa mwovu shetani.
Na pale mihuri itakapofunguliwa moja baada ya nyingine, hukumu kali sana itatolewa duniani. Manabii wengi wa Agano la Kale waliitaja mengi kuhusu jambo hili, kwa mfano:
"Tazama, siku ya Bwana Inakuja, siku kali ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi wasikae ndani yake. Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze. Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali" (Isa. 13:9-11).
"Na makundi ya wanyama watalala kati yake, wanyama wote wa mataifa; mwari-nyuni na nungu watakaa juu ya vichwa vya nguzo zake; sauti yaoitasikiwa madirishani; vizingitini mwake mtakuwa ukiwa; kwa maana ameifunua kazi ya mierezi. Huu ndio mji ule wa furaha, Uliokaa pasipo kufikiri, Iliosema moyoni mwake, mimi nipo, Wala hapana mwingine ila mimi. Jinsi ulikuwa ukiwa, mahali pa kulala pa wanyama wa bara! Kila mtu apitaye atazomewa, Na kutikisa mkono wake" (Sef. 2:14-18).
Kazi zote za mwovu shetani zitaharibiwa, na nguvu zake shetani kuharibiwa kabisa mpaka pale ngome zake zote zitakapoangushwa na kuharibiwa. Na pale simba wa Yuda atakapojitokeza akiwa mshindi kwenye uwanja wa vita pale mwisho wa dhiki kuu, mpinga Kristo na yule nabii wa uongo watashikwa mateka na kutupwa kwenye ziwa la moto. Naye shetani atafungwa nakutupwa kwenye shimo lenye urefu usio na kipimo kwa muda wa miaka 1000.
Na huku wakingoja kwa hamu matukio haya, wazee wanangoja kwa makini kuona muhuri wa kwanza ukifunguliwa.