2. Kuenea Kanisa

Barua saba za kutia  moyo na pia kukosoa zimetumwa na Kristo kwa makanisa saba katika Agano Jipya. Wakati barua hizo kutumwa, kulikuwa tayari yako makundi zaidi ya mia moja ya waumini. Lakini saba kati ya makundi haya yalichaguliwa kwa ajili mienendo na matukio yaliyokuwa katika makanisa haya yalikwa karibu ni sawa kote wakati huo. Hatuna sababu maalum iliyofanya makanisa au vikundi vya waumini wote vikose kupokea barua. Kila kikundi cha wakristo, kanisa, au mtu yeyote binafsi anaweza kuchukua ushauri katika barua kuwa umeelekezwa kwake binafsi, na kuutilia maanani.

Katika Ufunuo 2 na 3  twaona kanisa la Kristo kikamilifu kuwa liko katika au limejigawanywa katika vikundi saba. Kwa hivyo kanisa lile la kwanza lilikuwa na vikundi saba. Hivi leo, tukiwa tunakaribia sana siku za mwisho, kanisa bado liko katika vikundi saba.

Na kwa muda wa miaka hii yote ambayo imepita tangu Kristo anzishe kanisa, kumekuwa na aina saba za makanisa. Historia ya kanisa yaweza ikagawanywa katika enzi saba maalum. Hivi sasa tuko katika enzi ya saba. Enzi hii ya saba ni sawa na enzi ile ya kanisa la Laodikea katika Ufunuo. Ingawa yako katika vikundi vya makanisa sita yanayotangulia, idadi kubwa ya kanisa imo katika kikundi hiki cha saba yaani Laodikea.

Katika yale ambayo tunaelekea kuyataja hivi sasa kuna tofauti kubwa sana kati ya kanisa la Kristo, na Wakristo walio katika kanisa. (Church of Christ and Christian Church). Kanisa la Kristo ni kanisa ambalo wanachama wake  ni watu ambao dhambi zao zimeoshwa na damu ya Kristo. Nao wakristo walio katika kanisa hawa ni wale ambao wameingia katika kanisa lolote la Kikristo ambao hawajapokea wokovu. Katika makanisa ya Kikristo, Idadi kubwa ya waumini ni wale ambao wanafanya mambo wanayoyachukua kuwa maadili ya kiKristo lakini ndani kabisa, wao sio wakristo. Ni wakristo kama hao ambao Yohana anawatumia ujumbe kupitia maandishi haya matakatifu. Anawatuka wahusika watubu jinsi vile imeandikwa katika  barua tano.

1. Kanisa la Efeso – Kanisa Ambalo Limeacha Ukristo

Katika mwaka wa 95 AD, wakati Yohana alipopokea ujumbe kwa njia ya maono, kulikuwa na wale ambao walikuwa wameacha Ukristo, na kwenda kinyume cha maadili ya kikristo, kwa kurudia maisha yao ya hapo mbeleni. Vikundi vya wakristo hodari ambao tuliwasikia katika Matendo ya Mitume walikuwa wanarudi nyuma katika imani yao Ukristo wao ulikuwa  sawa na ule ambapo Kristo hayuko msitari wa mbele. Taratibu za kiKristo zilikuwa bado zinafuatwa na Wakristo hawa lakini hawakuwa wakristo halisi ndani yao. Kristo hawezi kukubali utaratibu wowote unaofuatwa ambao hawekwi mbele. Anasema hivi:

"Lakini nina neno moja juu yako, yakuamba umeacha upendo wako wa kwanza. Basi kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini usipofanya hivyo naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako mahali pake usipotubu" (Ufu. 2:4-5).

Mwenyezi Mungu anayaita makanisa yote na kuyataka yatubu. Vitendo vyetu sisi wanadamu tunavyofanya kutimiza  mambo fulani ya kutufaa binafsi havikubaliki mbele ya Mungu. Kanisa bora ni lile ambalo waumini wanamtumikia Bwana wakiongozwa na roho mtakatifu. Kanisa lahimizwa na kushauriwa lirudie yale ambayo ni bora na waliyafanya hapo mbeleni. Ikiwa kanisa halitarudia upendo wake wa pale mbeleni, basi kuna onyo hapa kwamba Bwana atachukua roho wake Mtakatifu na kumuondoa humo kanisani.

Na hapa hali yao waumini itakuwa ni sawa na ile ya watu ambao hawana mwanga. Pasipo roho mtakatifu, kuna giza. Na wakiwa kikundi cha watu wasio na roho mtakatifu, wao watazidi kustawi lakini hawatatumiwa na Kristo katika kazi yake ya utukufu. Kristo sasa atachukua mamlaka yote kutoka kwao na kuwapa wakristo wengine ambao wako tayari kumtumikia kwa roho na kweli.

Je, Ukristo wako ni wa aina gani? Unapomtumikia Kristo, unafanya hivyo kwa sababu gani? Ni kwa ajili umelazimishwa na wenzako au ni kwa ajili ya sababu za kibinafsi? Ama ni kwa ajili roho mtakatifu anakutaka ufanye hivyo? Na pale unapofanya hivyo, unafanya hivyo ili Kristo asifiwe na kuheshimiwa? Acha taa yako ya Ukristo iangaze ili wote walio karibu wavutwe na kuja kwake.

Jambo moja la kutia moyo kuhusu kanisa hili ni kwamba, ingawa kanisa lenyewe limerudi nyuma, wakristo hawajakubali wala kuwakaribisha wale wenye imani potovu. Wamewashutumu wa Nikolai ambao ni wabaya machoni pa Bwana. Wao wanajitakia makuu na wanatenda uovu wa aina aina pamoja na usherati. Wao wanapendelea na kutaka kuanzisha utaratibu wa uongozi kanisani ambao unawapa viongozi madaraka fulani hata wale ambao hawafai kupata uongozi na hata hawastahili  viongozi. Hata jina lao hili “waNikolai” lina maana “kufanya wenzako kuwa wadogo, na wa udharauliwa.”

Hali hii ya kuwagawanya watu wakubwa na wadogo kanisani haifai katika Agano jipya kwani hali hii itazuia kukuwa wa Wakristo. Wadogo hawatapata fursa ya kukuwa, na hii itawafanya wakufe moyo. Na kwa ajili kanisa haliwezi kueneza injili kwa njia inayofaa.

Hali ilivyokuwa katika kanisa la Efeso ni hali ambayo ilienea makanisani mpaka mwaka wa 100. Hali hii inagusia jinsi vile hawa watu walivyokuwa naupendo wa Mungu, na pia jini vile imani yao imepunguka.

2. Kanisa La Smirna – Kanisa La Taabu

Jina hili Smirna lina maana "uchungu." Jina hili limetokana na sababu  kanisa la  Smirna lilikuwa kanisa la taabu na uchungu wakati wa enzi ya utawala wa kimabavu wa Warumi. Kila aina ya unyanyasaji ulitendewa waKristo wa Smirna. WaKristo hawa walitusiwa, na kutozwa faini na ushuru.

Wengi waliachishwa kazi, na mali yao kutwaliwa. Wengi wa WaKristo Smirna walishikwa na kutupwa korokoroni ambapo njaa na magonjwa yaliwasumbua. Wengi waliteswa, na hata wengine kupoteza maisha yao, na ikasemekana wanaenda kinyume cha  mafunzo ya kidini huko Smirna. Hata wakati fulani, wafungwa waliachiliwa kwenye viwanja vya michezo ili simba wawararue na kuwaua. Wakristo wengi kati ya hawa walifurahia na kutoa ushuhuda wao hata wakati huu wa mateso.

Mwokozi wetu anaelewa na kuhuzunika sana wakati wale walio wakristo wa kweli wanapokumbana na mateso kama hayo kwa sababu yeye mwenyewe alipata kuteswa. Katika barua hii, yeye hapa anawaambia wakristo  ni yeye aliyekufa na sasa yuko hai. Anawasihi  wakristo hawa wasimame imara wakati huu wa mateso kwa sababu baadaye watapokea tuzo ambalo ni kufufuka kwao baada ya kifo. Katika Ufunuo 2:10 kuna ufafanuzi zaidi.

"Usiogope mambo yatakayokupata, tazama huyo ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji la uzima" (Ufu. 2:10).

Siku kumi huenda zikawa ni enzi ya watawala kumi wa kirumi. Wa kwanza akiwa Nero mwaka wa 64 hadi Diocletian mwaka wa 305. Tayari muda ule wa taabu ulikuwa umeanza na dhiki na taabu zitaendelea au ziliendelea kwa muda wa karibu karne mbili hivi. Miaka 2 ya mwisho ya utawala wa Diocletian ilikuwa ya umwagikaji damu, na taabu nyingi mno. Diocletian alikuwa ni mtawala wa kimabavu ambaye alijichukua kuwa kama Mungu. Hata watu walipomkaribia, yeye aliwataka wapige magoti, na pia wabusu sehemu yake ya miguu wakisema: "Mungu wangu, Mungu Wangu."

Katika mwaka wa  305, alitoa amri kwamba Wakristo wanyimwe haki zao, na mali yao itwaliwe, na makanisa yote ya Wakristo yafungwe. Mateso yaliyofuata ya likuwa ya umwagaji damuu kiasi ambacho hakijawahi kuonekana Baada aya Diocletian uacha madaraka mwaka wa 305, mateso na kampeini ya kuondoa ukristo iliendelea hadi mwaka wa 312.

3. Kanisa La Pergamo – Kanisa Linalokubali Uovu

Tukio kuu sana katika historia ya kanisa ilitokea mwaka wa 312 AD wakati mfalme Constantine alikomesha kuteswa kwa wakristo baada  yeye kubadili imani na kuwa Mkristo.

Inasemekana kwamba wakati mmoja, alipokuwa safarini kwenda vitani, aliona msalaba angani uliokuwa na maandishi yafuatayo: In Hoc Signo Vinces (Katika Ishara hii utapata Ushindi). Baada ya hapo, inasemakana Constantine alipata ushindi mkubwa vitani, na kwa ajili hiyo, yeye akaamua kuwa Mkristo. Katika amri maalum mwaka wa 313 AD, alitoa amri kwamba ukristo uwe na haki sawa na madhehebu mbali mbali. Hata hivyo, imani yake ya Kikristo ina kasoro kwa sababu hakulaani imani tofauti na pia alipata ubatizo tuu pale  muda  mfupi kabla hajaaga dunia.

Hata hivyo, mabadiliko yaliotokea yalikuwa makubwa mno. Kanisa lilijikuta kuwa na wanachama ambao sasa ni watu mashuhuri, kati yao, mfalme mwenyewe. Wengi waliamua kumfuata mfalme na kuwa wakristo pia. Utaratibu wa kiKristo ulibadilishwa na sheria kushushwa ili idadi kubwa ya watu waweze kuingia kanisani kama wakristo. Mfalme aliwapa wakristo kiasi kikubwa sana cha pesa hasa wale walio walimu wa dini na makasisi. Nao walitumia pesa hizi kujenga makanisa makubwa sana.

Katika mkutano wa Nikea mwaka wa 325 AD, maaskofu walipata ruhusa maalum ya kuwafanya wawe wasimamizi wa kanisa. Na hii iliwafungulia mlango wale walioitwa wa Wanikolai warudi kanisani Efeso. Uwezo au bidii ya wakristo ya kutaka wajisimamie ilipinguka na mwishowe kunyanyaswa. Na baadaye ilikuwa ni lazima kila mkristo afuate maagizo na amri za maaskofu na makasisi. Na kwa njia hii, kanisa likawa  limeingilia neno la Bwana na hata kuingilia kazi ya roho mtakatifu katika maisha ya webye imani.

Na kwa ajili hii, kanisa limeingiwa na hali ya kutokuwa tiifu, na kupungukiwa imani Kupunguka kwa imani kwaweza kuonekana katika jina hili Pergamo ambalo maana yake ni "kuoana." Katika enzi ya huyu Constantine, kanisa “liloana” na Serikali. Na hali hii ya akanisa kuungana na serikali kwa njia hii ni sawa na usherati. Tofauti tuu hapoa ni kwamba usherati huu ni wa kiroho. Tuanasoma katika Yakobo:

"Enyi wazinzi hamjui  ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni  kuwa adui wa Mungu. Basi kila atakaye kuwa rafiki wa  dunia hijifanya kuwa adui wa Mungu" (Yak. 4:4).

Mungu anataja hali hii ya kujiingiza katika mambo ya dunia, na mambo ya dhambi kuwa  sawa na dhambi ya Balaki katika  kitabu cha Hesabu, Agano la Kale. Balaki aliwafanya wana wa Israeli wale nyama iliofanyiwa uchawi, na pia kujiingiza katika usherati katika Hesabu 22 - 24; Balaamu aliombwa, ama aliagizwa na Balaki wa Moabu awalaani wana wa Israeli. Balaamu alikataa kufanya hivyo, akamtaka Balaki atumiye mbinu na kuwasihi wajiingize sherehe za baal. Mbinu hii ilifanikiwa kwani katika Hesabu 25, waIsraeli walikubali mualiko na kuhudhuria sherehe za Baal. Na hapo wakaanza kujiingiza katika usherati na hata kuomba mizimu. Hali hii ilimkasirisha Mungu ambaye alileta maradhi yaliyowaua watu 24,000. Balaki alifurahi sana kwani alikuwa ametimiza lengo lake la kumfanya Mungu akasarike nao. Musa naye anasema  hivi katika Hesabu 31: 15-16:

"Musa akawauliza, Je! mmewaponya wanawake wote hai? Tazama, hawa ndio waliowakosesha wan wa Israeli, kwa shauri la Balaamu, wamfanyie Bwana dhambi katika hilo jambo la Peori, na kwa hivyo pigo lilikuwa katika mkutano wa Bwana."

Hata katika siku zetu leo, shetani amekuwa akitumia mbinu ilio sawa na hii. Muovu, badala yakutumia nguvu siku hizi anatumia ushawishi kuwaelekeza Wakristo kwenye dhambi. Wakristo wengi wamejikuta na wako hivi sasa katika mtego wamenaswa katika dhambi  kutokana na ushawishi. Mateso ya aina aina hayakuweza kuangamiza kanisa katika mataifa ambapo hakukuwa na mateso sawa na yale katika mataifa ya kiKomunisti. Wakristo wengi wanamkasirisha Kristo kwa ajili ya kujiingiza katika uovu ulioko duniani.

Onyo kali kwa Wakristo Pergamo ni kwamba wasijiingize na kuwa marafiki na waovu duniani ni onyo ambalo lazima tulitilie maanani leo hii. Mungu aita Pergamo kuwa penye kiti cha enzi cha shetani (Ufu. 2:13). Mji huu wa Pergamo ulikuwa na maktaba iliokuwa na vitabu 200,000 ambavyo vilikuwa na Filosofia kutoka  Ugiriki.

Imani kwa miungu wengi (pantheism) ilienezwa, na hata mafunzo aina ya metaphysics, ana mafunzo kutoka Plato yalitiliwa mkazo. Wengi waliamini mambo au miujiza yab kishetani. Kulikuwa na makanisa kama lile la Asclepius, ambaye alikuwa Mungu wa uponyaji ambaye alikuwa na uwezo wa kuponya na yeye alikuwa Mungu na umbo la nyoka. Kulikuwa na mfalme ambaye walimuabudu katika mji huu. Wakati ufalme wa Babeli ulipodidimia, mfalme wa Chaldean na wafuasi wake walienda kuishi kama wakimbizi Pergamo. Kwa vile Babylon ilikuwa makao makuu ya dini ambazo si za Kikristo. Kiti cha enzi cha mmoja wa wakuu wa dini hizi kilipelekwa Pergamo na hapa kukawa na makao makuu. Na hapa mtindo ule wa kuwafanya wakuu wa kanisa kuwa wakuu tena serikalini ulitiliwa mkazo.

Kwa hivyo, huu ukawa ni mwanzo wa wakuu serikalini kupewa nafasi ya uongozi kanisani. Pia kulikuwa na mtindo Babeli wa kuabudu Mungu wa jua, na malkia (queen) wa mbingu na mtoto wa kike na ni kupitia msingi huu Madonna alikuja kuheshimiwa sana ana mtoto wake na hata Maria mama wa Mwokozi.

Kwa hivyo kanisa liliingiliwa na kupotoshwa na mienendo  na mila za kibabeli. Wale ambao walip[inga kuingiliwa kwa kanisa kwa njia hii waliteswa na kuuawa. Mfano ni Antipa (Ufu. 2:13), anasifiwa kwa kwa ajili ya kupinga uovu aliouona hata akafa kwa ajili ya msimamo wake huu. Antipa anasifiwa kwa kuwa shahidi shujaa. Jina hili Antipa lina maana "Mpinga Yote." Kwa kweli, Antipa alipinga kila jambo ambalo halikumrithisha.

4. Kanisa La Thiatira – Kanisa Zinifu

Kulingana na Alexander Hislop katika kitabu chake The Two Babylons, makao makuu ya makuhani wa dini za Babeli walihamisha makao yao kutoka Pergamo hadi Roma, na uhamisho huu ulileta makao makuu ya shetani, na mila zake za kidini hadi Roma.

Katika mwaka wa 606 Boniface III alitiwa wakfu kuwa askofu mkuu dunaiani. Huu ulikuwa mwanzo wa enzi ya kikatoliki. Katika enzi ya kati (Middle ages) kanisa lilitawaliwa na kusimamiwa na makuhani, maaskofu na maKadinali na Baba askofu (pope) waliokuwa watu watu wakupenda mamlaka. Kanisa lilikuwa na uwezo uliopita na kuzidi nguvu za Biblia. Hata yale mkuu Pope alipitisha yalichukuliwa kuwa yasiyoweza kutolewa kosa (ex-cathedra.) Kristo sasa alichukuliwa kuwa mbali na wanadamu na Mungu. Watu walilazimishwa sasa kwenda kwa makuhani na makasisi kutubu dhambi zao.

Kwa hivyo kanisa lile la uovu la Babeli liliingiza mila zake katika baadhi ya makanisa makubwa ya siku hizo, na hapa mengi yasiyo ya kiKristo yalijiingiza kanisani. Moja ya hayo ni kumuabudu Maria, ambaye kwa kweli ni sawa na mungu wa Mbinguni aitwaye Semiramis aliyeabudiwa na watu wa Babeli. Maria alitiwa wakfu mwaka wa 38, na ilisemekana kwamba alienda mbinguni. Hata Julai mwaka wa 1987, hadi Agosti 1988, muda huu wote ulichukuliwa kuwa mwaka wa Madona. Yeye anaitwa mama wa Mungu asiye na dhambi, na pia mama wa mbinguni.

Katika barua hii, Mungu anafananisha imani hizi sawa na uovu uliotendwa na Jezebeli kuwashawishi waIsraeli wakamuabudu Baali na kufanya usherati. Katika barua hii, Kristo anakumbusha kanisa hili la Thiatira kwamba yeye ndiye mwana wa Mungu. Na kwamba yeye siye tu mwana wa Yusufu na Maria.

Kwa wale walio na imani ambao watajikuta katika maafa kutokana na uovu wa kanisa wakati wa vita vitakatifu (holy wars) Mungu anamaelezo ya kuwatia moyo:

"Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wowote wasio na mafundisho hayo, wasizijua fumbo za shetani, kama vile wasemavyo, sitaweka sitaweka juu yenu mzigo mwingine. Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja. Na yeye ashindaye na kuyatunza matendo yangu hata mwisho nitampa mamlaka juu ya mataifa, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa baba yangu. Nami nitampa ile nyota ya asubuhi" (Ufu. 2:24 - 28).

Wengi ambao wamekumbana na kifo kwa ajili ya imani yao, wametiwa moyo na maneno hayo kwa muda wa miaka mingi. Wakizidi katika imani yao, basi watastawi na kutawala na Kristo katika wakati ule wa millennial. Katika serikali hii, hakutakuwa na rushwa na hongo, wala uharibifu na kutoelewana. Nyota yenye mwangaza asubuhi ni ishara ya siku ile mpya ambayo itajitokeza duniani kuondoa hiza.

Enzi ya Thiatira iliendelea hadi wakati wa mabadiliko makubwa ya enzi ya kati (Middle Ages) mpaka enzi ya mabadiliko ya kiProtestanti.

5. Kanisa La Sardi – Kanisa Lisilo na Uhai

Ni jambo la kutatanisha kwamba kanisa ambalo ni la wakati wa mabadiliko makubwa ya kidini (Reformation) laweza kuchukuliwa kuwa ni kanisa ambalo halina uhai. Mungu mwenyewe anasema:

"Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenaye yeye aliye na hizo roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa" (Ufu. 3:1).

Wakati huu, ni sehemu ndogo sana ya kanisa ambayo ilikuwa imebadilika (Reformed) kwa ajili ya kufichuliwa wazi baadhi ya imani na itikadi zisizo sawa katika kanisa la kiRumi. Hata hivyo, ingawa kulikuwa na mabadiliko, bado kulikosekana hali kamili ya kuwa na imani  kanisani Sardi. Mabadiliko haya kufikia kila sehemu ya  kanisa. Sababu ilikuwa ni kwamba makanisa ambayo yangeweza kueneza injili kati ya wale wasio na imani yalikuwa bado hayajajitokeza vikamilifu. Bwana anawazomea kwa ajili yao kutojali uovu ulioko.

"Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, na yanayotaka kufa maana sikuona matendo yako yametimilika mbele za Mungu wangu" (Ufu. 3:2).

Kristo anasema au anawaambia hawa walioko Sardi kwamba ni yeye aliye na roho saba za Mungu. Yeye anawaeleza haya kwa ajili ni yeye anayewapa makanisa roho mtakatifu. Ingawa waKristo wa Sardi walianza na msingi bora, walihitaji kujitoa kabisa mbele ya roho mtakatifu ili wapate nguvu na motisha kutimiza kazi waliowekewa katika Agano Jipya.

Historia imethibitisha kwamba katika miaka 200 ya enzi ya mabadiliko, kanisa katika enzi hii lilitimiza kiasi kodogo sana cha kazi ya Uinjilisti likilinganishwa na kanisa katika enzi ya Filadelfia yapata muda wa miaka 20. Sababu iliyoleta hali hii ni kwamba, kanisa hili la Sardi lilikuwa linazingatia  sana umuhimu wa kufuata utaratibu bila kujihusisha zaidi katika kazi jinsi vile roho matakatifu kutoka juu angewawezesha.

Hata hivyo kulikuwa na wale ambao katika enzi hii ya mabadiliko walijikuta katika hatari kubwa kwa ajili ya imani yao, nao walikuwa tayari kusimama mbele ya hadhara hata wakati wa vitisho vya kupita kiasi, nao hawakutupilia mbali imani yao. Hawa nao wamepokea agizo:

"Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili" (Ufu. 3:4).

6. Kanisa la Filadelfia – Kanisa la Kueneza Injili

Jina hili, Filadelfia lina maana "Upendo wa kindugu," na hii ndio ilikuwa sababu kuu ya mkutano na kazi za umishonari kati ya mwaka wa 1750 na 1900. Wakiwa wamejazwa na roho mtakatifu, wakristo walijitokeza na kueneza injili Asia, Afrika, Marekani Kusini, na hata kwenye visiwa vilivyojificha kwenye bahari. Wakiwa bila vyombo vya kufaa, maisha yao yakiwa hatarini kutoka kwa dini za kienyeji, maginjwa na wanyama wa pori hatari, wamishonari walijitoa kueneza injili. Walijifunza lugha mpya ngumu kwa kujitolea. Walitafsiri maandishi matakatifu kwa lugha za kienyeji, wakaanzisha shule na mahospitali wakiwa na vipawa na pesa kiasi kidogo sana. Mali hii ilitoka kwa waKristo wenzao waliojitoa mhanga kuona  kwamba habari njema yaenea kote.

Ingawa kulikuwa na pingamizi hizi, kazi ilienea kwa ajili Mungu alikuwa na watenda kazi. Haya ndiyo Mungu alisema kuhusu wafanyi kazi: "Nayajua matendo yako. Tazama nimekupa mlango uliofunguliwa mbele  yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umekitunza neno langu, wala hukulikana jina langu" (Ufu. 3:8).

Kati ya mashujaa wa imani ambao waliweza kueneza injili ni kina George Whitefield, John Wesley, Charles Finney, D. L. Moody, Hudson Taylor, William Carey, Andrew Murray na wengine wengi.

Mungu anawatia moyo watumishi wake ambao wanafanya kazi katika mazingira ya taabu na kuwataka waendelee kuvumilia: "Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwa taji yako" (Ufu. 3:11; soma pia Ebr. 11:24-26).

Jambo moja ambalo lajitokeza ni kwamba ni kanisa la Filadelfia na lile la Smirna hayakupstikana kosa lile la kukiuka maadili ya Kristo. UKristo halisi katika kanisa la Kristo hujitokeza kupitia waumini kuwa na imani na kujinyima, katika hali ya ugumu zaidi hapa duniani.

7. Kanisa La Laodikea – Kanisa la  Kupenda Mali

Kanisa la karne ya ishirini linafanana na lile la Laodikea. Hili kanisa la Laodikea ni kanisa lenye baridi (Halina moto) Kwa hivyo, hii yaweza kuchukuliwa kuwa ishara kwamba kanisa la karne hii yetu ya ishirini ni kanisa la siku za mwisho. Kuna jambo moja la kutisha kuhusu kanisa siku hizi.

Wakristo wengi wanatosheka na jinsi vile kanisa lilivyo. Wanatosheka na hali ile ya kuonekana inje kuwa wakristo. Au wanatosheka na hali ya kuonekana waKristo inje na hasa kupitia yale wanayoyafanya. Kwa inje wanaonekana kuwa wakristo, lakini ndani yao, mambo ni tofauti. Wao wanaendelea kusali bila kujua kwamba wako katika  hali ya upweke kiroho. Ingawa waumini ni matajiri. Wana mali, na taratibu zao za maombi ni maalum, wao hawaombi na moyo safi. Hawana ukweli katika maombi yao. Mungu huwa hahusishwi na imani kama hizi ambazo binadamu anajitengenezea. Imani ya kuonekana inje, yeye hataki kuhusishwa nayo. Sababu ni hii:

"Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. Kwa kuwa wasema, mimi ni tajiri, nimejitajirisha wala sina haja na kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na masikini, na kipofu, na uchi" (Ufu. 3:16-17; soma pia 1 Tim. 6: 7-12).

Utajiri ulioko kanisani Laodikea sio tu utajiri wa mali, ila ni utajiri wa kiujuzi, na kisiasa ambao unatumiwa kusuluhisha matatizo ya kisiasa. Na kwa ajili ya kujiona kuwa anajiweza, mwanadamu ameacha kumtegemea Mungu, na badala yake ana maringi na kiburi. Hataki kunyenyekea mbele ya Mungu. Jina Laodikea lina maana "Haki Za Binadamu," na hapa ni wazi hili kanisa lazingatia zaidi mambo yanayohusu wanadamu kuliko Mungu. Kanisa limekuwa ni chombo cha kutumiwa na wanadamu kutimiza malengo fulani kumfaa mwanadamu bila kutilia maanani Mungu Binadamu sasa amebadilika na kuwa karibu sawa na Mungu. Yaani yeye ni Mungu na hapa anaanza kuhubiri injili ambayo inatilia mkazo umuhimu wa kupata mali na utajiri, na kutimiza mambo makubwa.

Laodikea ni mfano wa mwanadamu asiye na imani. Yeye anajichukua kuwa anaweza kuelewa mambo yote kwa uwezo wake mwenyewe. Matokeo ni kwamba, yeye anelewa Biblia kwa njia ambayo siyo ile amabayo ni ya kumfanya awe na imani halisi. Matokeo ni kwamba Biblia inaeleweka kijuujuu. Imani na hakikisho kwamba lazima mtu azaliwe mara ya pili ni jambo geni kwake. Mkristo kama huyu anawafunza wenzake wawe na imani sawa na hii. Hali hii imeleta wakristo  wengi kuwa na imani ya juu tu. Makanisa yanayojipima kwa kutumia misingi hii ya kibinadamu hujiona kuwa bora sana.

Kuna hatari hapa kwani hali hii ya kujiona kuwa bora bila kuzaliwa upya ni hali ya wale wasio wake Mungu. Kati ya hawa wanapohisi upungufu, wao hukimbilia ubatizo au meza ya Bwana huandaliwa kujenga zaidi mtu kiroho, sio kumpa imani. Imani huja kupitia maombi na ni zawadi kutoka kwa Mungu moja kwa moja.

Tunasoma katika Ufunuo 20 kwamba ingawa Mungu hajihusishi na imani ilioko Laodikea, na njia yao ya maombi, bado anawatakia mema. Yeye hapendezwi na hali yao mbaya. Anawataka wamrudie na watubu dhambi zao. Ni Kwa sababu hii anasimama mlangoni mwa kanisa karne hii ya ishirini na kubisha hodi: “Nabisha yeye yote atakayenifungulia mlango, nitaingia na kula naye; naye kula nami.”

Idadi kubwa ya makanisa yanafanya mengi ambayo ni ya kidunia, hasa makanisa makubwa. Makanisa haya siku hizi yanatafuta masuluhisho ya shida za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hali hii imeleta kufifia kiroho wengi kanisani. Hali hii itaendelea hadi pale Kristo atakaporudi kuwachukua wale walio wake. Kwa ajili ya kujihusisha na mambo mengi ya kiUlimwengu, kanisa nyakati hizi za mwisho limepoteza na pia halina nguvu itokayo kwa roho mtakatifu. Kwa hivyo, tukio lile la mwenye imani kunyakuliwa litawajia wengi hasa wale wataalamu wa masomo ya dini (theologians) na makasisi ambao hawatarjii. Litakuwa jambo la kuwashtua sana.

Litakuwa tukio la kushangaza ambalo hakuna atakayeweza kulieleza vyema. Wengi watalazimika kurudia Biblia wakitafuta maelezo upya kuhusu matukio hayo. Watakao rudia mafunzo ya Biblia upya watabarikiwa kwani uhusiano wao na mwokozi wetu utakuwa wameimarisha. Wengine nao wataendelea kufuata njia yao na kuwa wafuasi wa yule Mpinga Kristo (Antichrist.)

Je, umetilia maanani yote yaliyokataliwa katika barua saba hizi? Ikiwa ni hivyo, basi, bila shaka unajua ni wapi unahitajika kujibadili.

Upungufu wako kiroho lazima umejitokeza na sasa ni juu yao kutafuta suluhisho. Ikiwa hujakubaliki na kupokea wokovu, na una ubaridi wa kiroho, hadi hivi sasa haujatilia maanani maonyo yaliyo katika barua saba hizi, basi unaelekea kupata shida kuu. Utahukumiwa na giza kuu lakungoja. Wakati wa kanisa kuenea wakaribia kikomo, na sote karibu tutasimama mbele ya kiti chaenzi ili tueleze juu ya imani yetu au jinsi vile ytulivyo wasio na iamani. Litakuwa jambo bora hapa kufuata ushauri wa Isaya: "Mtafuteni Bwana maadamu anapatikana, mwiteni maadamu yu Karibu" (Isa. 55:6).