Baada ya kutaja mengi yanayohusu siku za mwisho, ni bora hapa kuweza kutaja mbinu za kukuwezesha kuponya nafsi yako. Lengo letu kuu hapa ni kutaja mbinu za kupigana vita vya kiroho ili wakati wa kurudi kwake Kristo, uwe mmoja wa wale watakaokutana naye baada ya wakati ule wa dhiki kuu .
Wale watakaoepuka dhiki kuu ni wale ambao wamejitayarisha kiiroho (Mk. 13:33-37; Lk. 21:34-36). Pale agizo hili litakapotimia, wengi ambao wanafuata ya dunia hii hawataamini. Huku wakiwa wamejawa na hofu, watapokea hukumu yao. Wengi watajiuliza: “Ni nini kitatokea sasa; na tufanye nini?"
Biblia ina majibu ya maswali kama haya na itawaongoza walio na imani. Ikiwa maagizo kutoka maandishi matakatifu yatafuatwa, basi utaweza hata kupata wokovu wakati ule wa dhiki kuu na kuurithi ufalme wa mbinguni. Hata hivyo halitakuwa jambo rahisi kufuata njia nyembamba hii ya kukuelekeza mbinguni wakati huu wa dhiki kuu. Mbali na kumkubali Kristo kuwa mwokozi, mwenye imani atalazimika kuwa tayari kufanyiwa dhihaka, kudharauliwa, kuwa masikini, na hata kukataliwa na ndugu zake. Mwenye imani mmoja huyu hata huenda akatarajiwa kuwa tayari kufa kwa ajili ya imani yake.
Ingawa wako wale watakaochagua njia ya uzima; wengi , kwa ajili ya vitisho na shida hizi watachagua njia pana ielekeayo kifo. Kutatokea kanisa lenye misingi ya uongo, nalo litawapoteza njia mamilioni ya watu.
Hebu sasa tuangalie matukio siku za dhiki kuu. Matukio haya yatatokea katika muda wa miaka saba. Muda wa kwanza wa miaka mitatu na nusu ni ule wakati wa amani ya uongo (false peace), na hii itafuatana na miaka mitatu na nusu ya dhiki kuu yenyewe.
MIAKA SABA YA DHIKI
(Mwaka Wa Sabini Wa Wiki Katika Hesabu Ya Danieli)
Miaka saba ambapo Mwana mwali hayumo duniani. Wakati alikuwepo, alikuwa kama mwangaza katika giza. Baada ya kuondoka, giza la kiroho.
UTAWALA WA MPINGA KRISTO
Amani ya Uongo (miaka 3˝) |
DHIKI KUU (miaka 3˝) |
Mpinga Kristo afichuka kama mwongo. Uongozi wake duniani katika uchumi, siasa na kidini. |
Mpinga Kristo achafua hekalu, apiga marafuku sherehe kunisani, na kujitangaza kuwa Mungu. Taifa la Israeli lavunja ushirikiano na huyu mpinga Kristo. |
Mfumo mpya wa serikali ambapo kuna serikali ya kimataifa, jeshi la amani, na muungano wa madhehebu. |
Muungano wa madhehebu duniani wavunjiika, badala yake watu wanalazimishwa kumuabudu mpinga Kristo |
Mpinga Kristo afikia makubaliano na taifa la Israeli kwamba yeye ni masihi. Ni yeye wa kuabudiwa. |
Wayahudi na Wakristo wateswa kwa ajili ya kutomchukua Mpinga Kristo kuwa Mungu. Wengi washikwa na kuuawa. |
Hekalu ya tatu yajengwa Yerusalemu karibu na musikiti, na hapa uongo kwamba Mungu mmoja. |
Mpinga Kristo ndiye kiongozi wa kijeshi wa dunia. Anasimamia uchumi duniani ambapo hakuna matumizi ya pesa. Komputa nambari kama 666 zatumiwa. |
Babeli yajengwa upya nayo Iraq ndio makao makuu ya umoja wa mataifa, na ishara ya umoja duniani. Kutatokea maendeleo ya uchumi, na amani isiyo ya ukweli |
Vifo vingi vinavyotokana na vita, na mikasa ya kimaumbile. Wanajeshi waandaliwa kwa ajili ya vita vya Har- Magedoni. |
Saa ya kupaa angani wateule wa Mungu, mwanga wa dunia utapotea. Giza kuu la kiroho litakumba dunia baada ya wale walio na mwanga kutoka kwa Kristo kupaa mawinguni. Hali ya kuogofya itawakumba wengi sana hasa makanisani.
Wale walio na imani zisizo za kiKristo, wale wasio na imani na wengineo watashikwa na hofu, wasijue ni mambo gani hayo yanatokea. Hata hivyo maelezo yasiyoaminika ya ajabu yatatolewa kueleza tukio hili la wenye imani kupaa angani. Uongo wa ajabu utatolewa kuwahadaa wengi kuamini maelezo ya kutoka shetani kuhusu tukio hili la waamini kupaa angani.
Karibu na tukio hili la kupaa angani tukio ambalo latajwa na nabii Ezekieli; kwamba muungano wa jeshi la kiarabu na urusi litashambulia taifa la Israeli (Ezek.38-39). Zana za kinuclear huenda zikatumiwa kushambulia taifa la Israeli. Shambulio hili litazidisha uwezekano wa vita vya dunia kutokea. Mzozo wa kimataifa utazuka. Masoko ya hisa, mengi yao yataporomoka. Majeshi yatawekwa katika hali ya tahadhari Ulaya, mashariki ya kati, Asia na Marekani. Na hapo tukio la ajabu litatokea.
Jeshi ambalo limejianda kupigana na taifa la Israeli litazimwa na Mungu (Ezek.39:1-5). Waisraeli watakubali kwamba ni Mungu amefanya muujiza huo, na watamshukuru Mungu. Lakini kosa watakalofanya ni liloe la kumtambua masihi ambaye hafai.
Mtu aliye na uwezo wa ajabu, wa kutenda miujiza atajitokeza (2 The. 2:9; Ufu.13:11-13). Naye atasema ni kwa ajili yake taifa la Israeli limepata ushindi dhidi ya adui zake. Atasema ametumwa na Mungu kuokoa taifa hili, na kuepusha ulimwengu usikumbwe na vita vikuu na hapo kuokoa wanadamu. Yeye ataunganisha makanisa na nchi mbali mbali na kufanya makubaliano yawezekane ambayo yatamuelekeza kuwa kiongozi wa dunia yote. Watu watamfuata, na kustaajabishwa sana na mipango yake mballi mbali ya kuleta amani duniani. Yeye atawafanya maadui wa jadi wakubaliane.
Kutakuwa na hali ya kuwachukia sana waKristo walio na imani kamili ya kueneza injili (Evangelicals). Viongozi wa madhehebu kama haya wataitwa wafuasi wa ”mpinga Kristo.”
Wakati wa utawala wa mpinga kristo, jambo moja kuu ambalo litajitokeza ni uhusiano wa karibu sana kati ya kanisa na siasa. Mpinga Kristo ataunganisha uongozi wa kisiasa na ule wa kanisa, katika serikali ile ya kimataifa na hapo akiwa mkuu wa serikali, yeye pia atakuwa mkuu wa kanisa. Kiongozi atakayeshirikiana naye ni nabii wa uongo ambaye naye atakuwa kiongozi wa muungano wa madhehebu yote duniani. Atawashawishi wafuasi wa madhehebu mbali mbali wameheshimu yule mnyama (the beast) na kumsali.
Kwa kujisingizia kuwa kiongozi wa kidini, mpinga Kristo atakuwa na uwezo wa kushawishi watu kiasi kikubwa sana; kiasi ambacho hakijaweza kuonekana hapo mbeleni. Yeye Mpinga Kristo atajifanya kuoenekana kuwa ametumwa na Mungu kuleta amani, na uelewano kati ya wanadamu.
Kristo aliwaonya wafuasi wake kuhusu uongo wa namna hii katika Mathayo.
"Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni asiwadanganye, kwa sababu wnegui watakuja kwa jina langu, wakisema mimi ni Kristo; nao watawadanganya wengi" (Mat. 24:4-5, 11).
Tukio lile la wenye imani kunyakuliwa litakapotokea, basi kazi ya kanisa itakuwa imefikia kikomo duniani. Mpaka wakati huu, Yesu mwenyewe atalinda kanisa lake ili lisidhuriwe na vita vya shetani. Haya twasoma katika Mathayo: "Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda" (Mt. 16:18).
Na wakati ule wa dhiki kuu, muovu atawapiga vita wale walio na imani.
"Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa (Ufu. 13:7). Yeye anaweza kuwashinda kimwili, lakini kiroho, hataweza kuwashinda walio na imani ikiwa wataendelea kushikilia imani yao hii" (Ufu. 12:11).
Ni miaka mingi imepita tukisubiri tukio lile la kunyakuliwa angani, na tayari makanisa mengi yamechukua mtindo ule wa kuwa dhaifu, na kufuata mitindo isiyofaa ambayo kwa umbali yaonekana kuwa ni bora. Hata makanisa mengi siku hizi yamejiingiza katika jumuia na mikusanyiko ya dini mbali mbali. Katika baadhi ya jumuiya hizi, umuhimu wa mtu kuzaliwa mara ya pili hautiliwi maanani jinsi maandishi matakatifu yanavyotilia mkazo (Yoh. 3:3).
Wakristo ambao wametupilia mbali imani yao, pamoja na wale ambao watakubali kuzaliwa mara ya pili wakati ule wa dhiki kuu itawabidi wajitoe kutoka makanisa na vikundi kama hivi wakati huo. Sababu ni kwamba kwa vile kiongozi ambaye ni mpinga kristo wakati wa dhiki kuu atakuwa ni yeye anayesimamia serikali, kanisa na hata uchumi. kwa hivyo, yule ambaye atapatikana kanisani atakuwa ni mfuasi wa mpinga Kristo.
Uasi wa ajabu katika mambo ya kiroho utajitokeza, na wengi watakaoasi kwa njia hii watafanya hivyo wakiwa na lengo la kutaka kujitangaza. Makanisa madogo yanayoamini na kueneza injili ya kweli ambayo wengi wa wafuasi wake watakuwa tayari wameshanyakuliwa yatalazimishwa kufungwa pale yatapokosa kukubali kwamba mpinga Kristo ni Masihi. Makanisa yale yatakayokubali kufanya hivyo, nayo pia yatakuwa yamebadilika na kuwa baadhi ya makanisa ya mpinga Kristo.
Itakuwa ni kazi ngumu sana kuponya roho yako wakati wa dhiki kuu. Haitakuwa tuu ni kazi inayohitaji mtu amkatae mpinga Kristo. Ni damu tuu Ya Yesu aliyekufa msalabani itakayowezesha mtu kuponya nafsi yake (soma Efe.1:7; 1 Yoh.1:8-9; 1 Pet. 1:18-19). Itakubidi utubu dhambi zako zote na kuziacha (soma Mit. 28:13). Itakubidi pia ukubali msamaha wake, na uanze upya kujijenga kiroho (soma War.12:2; 2 Wakor. 5:17). Pia itakulazimu ujisikie mwenyewe kwamba umeacha kabisa uovu (soma Yoh. 8:36). Shuhudia mbele ya wenzako kuhusu wokovu uliopokea (War.10:9-10). Shuhudia na kuwaeleza wale unaokutana nao jinsi vile umejitoa kabisa kumfuata Yesu. Itakupasa ujiunge na wandugu walio na imani sawa na kuwatia moyo wavumilie majaribu.
Roho mtakatifu atashuka na kumiminika kati ya Wayahudi: "Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza" (Zek. 12:10).
Pale mwanzo wa dhiki kuu, Wayahudi 144,000 watapokea wokovu. Wakiwa wamejawa na roho mtakatifu, watatangaza wazi wazi kwamba Kristo ni masihi wa taifa la Israeli na dunia yote. Ushuhuda wao huu utawafanya wasikubaliane kabisa na wafuasi wa mpinga Kristo, masiya wa uongo. Na ahapo basi wayahudi hawa ambao wamepokea wokovu watateswa, lakini Mungu mwenyewe atawalinda na kuwadumisha (soma Ufu. 7:1-8).
Wakristo ambao watapokea wokovu wakati huu nao watahitajika kuwa na uhusiano wa karibu sana na wayahudi hawa waliokoka. Itawabidi wawaunge mkono na hata watakapopata vitisho kwa ajili ya msimamo wao. Aliyeokoka wakati huu itakuwa ni laziama kwamba achukue jambo hili la kuwaunga mkono wayahudi waliokoka kuwa ni kama kitendo chake cha mwisho cha kueneza injili ya Kristo duniani. Kila Mkristo wakati huu lazima ajihadhari ili asije akajikuta yumo katika kikundi cha mpinga Kristo (soma 2 Kor. 11:13-15).
Mateso yatakayowakumba wakristo yatakuwa ya aina mbili wakati huu wa dhiki kuu. Katika miaka mitatu na nusu ya dhiki kuu, kutakuwa na amani isiyo halisi na pia umoja. Miaka mitatu na nusu itakayofuata itakuwa ya dhiki kuu kamili. Katika nusu ile ya kwanza, mpinga Kristo akiwa pamoja na wenzake atatawala pamoja na viongozi wa muungano wa madhehebu mbali mbali. Kutakuwa na matumizi ya nguvu, na sio kupita kiasi; na tena nguvu zitatumiwa tuu baada ya mpinga Kristo kujadiliana na kukubaliana na viongozi wenzake walio wa ngazi ya juu. Njia zote zitatumiwa kuwashawishi na hata kuwalazimisha watu watimize matakwa ya mtawala huyu mpinga Kristo.
Matumizi ya vitisho, hongo, kudanganya na propaganda ndizo zitatumiwa kuwafanya watu wawe wafuasi wa mpinga Kristo. Na pale kutakapotokea haja ya kutumia nguvu, basi jeshi la kimataifa litatumiwa kuwaadhibu wale ambao wana asi dhidi ya utaratibu wa mambo. Watakaoadhibiwa wataitwa waasi, na maadui ambao hawataki kuona amani na umoja duniani.
Vita vya maneno vitawalenga wakristo halisi. Wakristo hawa watachukiwa na kila mtu. Hata viongozi wa dini na jumuia zao za kidini wote watawachukia wakristo halisi. Pale mwanzo wa dhiki kuu, wakristo halisi watachukiwa, kukataliwa na kutishwa. Baada ya muda fulani, vitisho vitafikia kiwango ambapo sasa litakalobaki ni kuwaangamiza kabisa. Twasoma hivi katika Injili ya Yohana:
"Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi" (Yoh. 16:2-3).
Wakristo wakati huu wa dhiki lazima wajihadhari wasije wakakubali kurudi nyuma kwa ajili ya taabu hizi. Jiandae kuwa kati ya wale watakaomkataa yule mnyama na kuhubiri injili ya Kristo. Jiweke tayari kufa kwa ajili ya imani yako: "Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho katika jehanum" (Mt. 10:28).
Ili uweze kufaidika kikamilifu kwa ajili ya kuwa mmoja wa wale walio katika ufalme wa Mungu wakati wa dhiki kuu, ni vyema kuwa tayari kufanya mambo fulani kuanzia tuu pale mwanzo wa dhiki kuu. Jikinge kabisa ili usije ukawa yule ambaye anashughulikia tuu yale mahitaji yake binafsi na yale ya familia yake kiuchumi. Inatupasa ufanye yafuatayo:
· Umepewa agizo kwamba ni lazima umkatae kabisa mpinga Kristo na hila zake. Kama Danieli wa Agano la Kale, hufai kupiga magoti mbele ya mfalme wa Babeli wa siku hizi. Waonye wengi kadiri ya uwezo wako kuhusu huyu masihi wa uongo. Ungana na kufanya kazi pamoja na Wakristo wenzako kuwaeleza wenzako hatari za kudanganywa na kukubali yale yalio ya uongo.
· Usifanye lolote mwenyewe kujaribu kumtoa mpinga Kristo. Usijaribu pia kutetea mambo yale ya nchi yako. Wakati wa dhiki kuu ni wakati wa giza na kiongozi ambaye yuko wakati huo ni kiongozi aliye na mamlaka makubwa (soma Ufu. 13:7). Toa onyo kwa watu wasifuate huyu muovu. Waeleze wazi kwamba kuna shida na taabu zitakazowakumba wale wasiomfuata huyu muovu, ila wanamtii na kumfuata Masihi wa kweli, mwokozi wetu Yesu Kristo.
· Usifanye mambo fulani fulani ambayo huenda yakakuelekeza ushikwe na kuwekwa kizuizini pale mwanzo wa dhiki kuu, au hata kuuawa. Jaribu kumkwepa mpinga Kristo, na kukaa mbali sana. Jihadhari ili wasije wakakutimia kupata habari kuhusu wakristo na mahali walipo ikiwa watakuwa mafichoni. Kuna uwezekano kwamba wafuasi wa mpinga Kristo wataweka makachero katika vikundi vya wakristo. Ndivyo asemavyo Danieli wa Agano la Kale: "Basi watakapoanguka, watasaidiwa kwa msaada kidogo; lakini wengi wataambatana nao kwa maneno ya kujipendekeza" (Dan. 11:34). Usitoe siri ovyo, na hakikisha yule unayehusiana naye amepokea wokovu wa kweli, na siyo wokovu bandia tuu. Jihadhari sana na wale wakristo wapya ambao huenda wakawa ni wafuasi wa masihi huyu wa uongo.
· Jinsi ilivyokuwa katika kanisa la mwanzo, wakristo wanapaswa kusaidiana na pesa wakati wa dhiki kuu. Ukiwa Mkristo, ni bora uuze mali yako, isipokuwa tu pale mali hii inaweza kuwa ya msaada kwa jamii ya kiKristo wakati fulani. Kumbuka kwamba katika miaka mitatu na nusu ya mwisho ya dhiki kuu, hautaweza kuuza mali yako tena. Wakati huu, pesa haitakuwa ikitumiwa, na ni wale walio na chapa ya mpinga Kristo wataweza kujiingiza katika shughuli kama hii ya kuuza mali. Pia uza mali yako ambayo si ya muhimu hapo ulipo. Tumia pesa hizo kueneza injili, na kuwapa makao na kuwatimizia mahitaji yao wakristo wemzako ambao wana shida. Wanunulie chakula, nguo, vyombo vya nyumbani mablanketi na kadhalika. Hivi vyote vyafaa kuwekwa mahali fulani palipo siri. Usiache kazi yako katika miaka ile mitatu na nusu ya kwanza ya dhiki kuu. Fanya hivyo tuu ikiwa utalazimishwa.
· Katika Miaka ya kwanza mitatu na nusu ya dhiki kuu, makao maalum ya kueneza injili yafaa yaandaliwe ambapo Biblia zitachapishwa na hata kuwekwa. Biblia toleo la King James Version ndio Biblia inayofaa pekee. Weka nakala za Bibilia na vitabu vyenye mafunzo ya kikristo mahali ambapo hapawezi kufikiwa, kwani kuna uwezekano wafuasi wa mpinga Kristo wanaweza kuamua kuzitwa. Kumbuka kwamba wakati wa dhiki kuu neno la Bwana litakuwa halipatikani tena. "Nao watangatanga toka bahari hata bahari; toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki; watapiga mbio, wakienda huko na huko, kulitafuta neno la Bwana, wasilione" (Amo. 8:12).
Tukio la kustaajabisha sana litatokea baada ya miaka mitatu na nusu ya kwanza ya dhiki kuu. Mpinga Kristo ambaye mfano wake ni mnyama katika kitabu cha Ufunuo atauawa, lakini baada ya siku tatu, atafufuka (Ufu. 13:3). Watu watamuogopa, na kuamini kwamba yeye ni kiongozi aliye na uwezo usio wa kawaida kabisa. Watamchukua kuwa kama Mungu pamoja na Lucifer (Bilisi) ambaye kupitia nguvu zake, amefufuka (Ufu.13:3-4).
Shetani, Mpinga Kristo na nabii wa uongo watatumia nafasi hii kunyakua kutwa dunia yote. Dini ya kishetani ndio itakuwa dehebu linalotambuliwa pekee kote duniani. Wale watakaokataa kuwa wafuasi wa dhehebu hili, watauawa hadharani. Kuhusu maafa haya yatakayotokea, Kristo alisema hivi:
"Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeongoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo" (Mat. 24:21-22).
Ikiwa njia moja ya kumuwezesha kusimamia dunia yote, mpinga Kristo ataanzisha huduma mpya ya kiuchumi duniani. Pesa hazitatumiwa tena. Badala yake, chapa, ambazo kila mtu ana yake ndizo zitakazotumika. Wale watakaopewa nambari katika chapa hizi ni wale walio na uwezo wa kiuchumi. Yule atakayepewa namba atapewa tu baada ya kula kiapo cha uaminifu kwa mpinga Kristo huyu na serikali yake. Kiapo hiki kitathibitisha uaminifu wa yule anayepata chapa yenyewe kwa mnyama anayejifanya kuwa kama Mungu.
Kiapo chenyewe ni cha makubaliano na kifo (Ufu.14:9-11). Na kupitia kiapo chenyewe, watu watakuwa wamejiweka nafsi zao zote, kimwili, kimawazo na hata kiroho mikononi mwa dikteta huyu mpinga Kristo. Usiwe kama Esau katika Agano la kale aliyeuza urithi wake.
Nao wale watakaokataa kupokea chapa hii watateswa sana hivi kwamba ni wakristo walio na imani timamu wataweza kufanya hivyo. Kati ya yale yatakayowakumba ni haya:
· Wale wanaokataa watapoteza uraia wao katika nchi yao, na taifa kuu lililo dunia. Hili ni kosa na wafanyayo hayo wataadhibiwa kulingana na sheria.
· Kukataa kuwekewa chapa kutachukuliwa kuwa sawa na na kumkataa kiongozi imla huyu wa dunia, na hili ni kosa la uhaini. Adhabu yake ni kifo hadharani.
· Kukataa chapa hii ya mpinga Kristo kutakuwa ni sawa na kukataa kujiunga na dhehebu la mpinga Kristo na kumchukua mnyama kuwa Mungu. Hili ni kosa kubwa na hukumu ya kosa kama hili ni kifo.
· Bila chapa hii, mtu hataweza kutumia mitambo ya simu kutuma pesa (electronic funds transfer). Mtu kama huyu hataweza kuuza, wala kununua wala kutuma pesa kwa njia yeyote. Itakuwa ni vigumu kununua hata petroli ya gari. Na pale mtu anapokosa kulipa madeni yake, basi mali yake yote itatwaliwa. Lililo wazi hapa ni kwamba hakuna atakayeweza kustawi ama hata kuishi katika dunia hii ambapo sasa matumizi ya pesa yameondolewa. Kinachotumiwa kama pesa sasa ni chapa ile waliowekewa wafuasi wa mpinga Kristo.
· Watakaokosa kuwa na chapa hii, watapoteza kazi zao, na hawataajiriwa tena kwani itakuwa ni vigumu kuajiriwa bila kuwa na chapa hii ya mpinga Kristo.
· Baada ya kuondolewa matumizi ya pesa, pesa taslimu uliyonayo itakuwa haina kazi ila kutumiwa kununua nambari mpya, ama kuwekwa tu.
Ni wazi kwamba mpinga Kristo ataweza kutumia njia za kiuchumi kuwalazimisha watu wamfuate na kumchukua kuwa kama Mungu kwao. Ni kupitia njia hii wote walioko duniani watabadilishwa na kuwa watumwa wake.
Wale ambao hawatakuwa na chapa yenyewe watakosa kazi. Watakuwa hatarini ya kuuawa kwa ajili ya uhaini. Watatafutwa na askari maalum na kuelekeza sehemu za kunyongwa. Wengi watakufa kwa ajili ya njaa wakiwa njiani kutoroka. Magonjwa, hali mbaya ya anga, kiu na maji chafu – haya yote yatawaathiri wale watakaokataa kupewa chapa ya kiongozi huyu mwovu mpinga Kristo.
Pale mpinga Kristo atakapojitangaza kuwa Mungu, Wayahudi watampinga na kuvunjilia mbali uhusiano kati yake nao, na hii italeta hali ya uadui kati yake na wao, na kumfanya atake kuwamaliza kabisa. Myahudi atakayepona ni yule labda atakayetorokea jangwani labda Petra kusini mwa bahari ya Chumvi (Dead Sea). Na hapa Mungu atawalinda kwa muda wa miaka mitatu na nusu ya dhiki kuu.Mathayo inazungumzia jambo hili katika kifungu cha 24 (Mt. 24:15-21).
Wakristo nao pia wataandamwa kukimbizwa, na kuuawa kwa sababu ya kukataa kumchukua huyu mpinga Kristio kuwa kama Mungu (Ufu. 6:9-11; 13:15). Hata ingawa wanateseka, wakristo lazima wawasaidie wayahudi na kuwaeleza kuhusu kurudi kwake Masihi katika mlima wa mzeituni baada ya miaka tatu na nusu ya utawala wa masihi wa uongo (soma Dan. 12:11-12; Zek. 14:4-5). Mungu alisema haya kuwahusu wayahudi:
"Nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye, nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia zitabarikiwa" (Mwa. 12:3).
Ingawa mpinga Krsisto atakuwa na uwezo mkubwa sana kisiasa, kijeshi, kiuchumi na hata kidini, hataweza kuwafanya wakristo wa kweli wawe wamuinamie. Atawaua wengi, lakini hataweza kuwafanya wampigie magoti kama Mungu ikiwa wataweka imani yao katika Kristo. Ni katika saa hii ya giza kuu Mungu atawapa wanawe uwezo maalum wa kumkabidhi muovu (Ufu.12:11).
Kuna silaha tatu maalum ambazo zimetajwa hapa:
· Silaha ya kwanza ni damu ya mwanakondoo. Ni damu ya Kristo aliyekufa msalabani inayoweza kumuokoa mtu pale anapotubu dhambi zake mbele ya Mungu (soma 1 Pet.1:18-19; 1 Yoh.1:8-9). Damu iliyomwagika msalabani pia ni kinga ya kuzuia usishambuliwe na mwovu. Pale unapokumbana na vitisho katika maisha yako ya kiroho, weka imani yako katika Kristo ambaye kupitia damu yake, yeye ni kinga maalum.
· Silaha ya pili ni neno la ushuhuda. pale unaposhuhudia na kusema wazi kuhusu wokovu wako, basi adui mwovu anapata ugumu kukushawishi. Ushuhuda wako pia uaweza kuwafanya wenzako pia waweke imani yao katika Kristo. Usisite kushuhudia kuhusu Kristo.
· Na silaha ya tatu ambayo imetajwa hapa ni kutokuwa na hofu ya kufa kwa ajili ya imani yako. Vitisho vya vifo ndio silaha kuu atakayokuwa nayo mpinga Kristo. Ushuhuda wako utakuwa wa kuaminika kabisa ikiwa uko tayari kufa kwa ajili ya imani yako. Ikiwa unaogopa kifo, na uko tayari kubadili masimamo wako pale unapotishwa na kifo, basi ushuhuda wako utakuwa hauna nguvu kabisa na si wa kuaminika.
Mpinga Kristo na wafuasi wake wanaelekea kwenye adhabu ya milele. Wanaelekea mbali na Mungu na kwa moto wa milele:
"Kisha nikamwona huyo mnyama na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake. Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti; na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wkashiba kwa nyama zao" (Ufu. 19:19-21; soma pia Ufu. 14:9-11).
Ingawa wakristo wamo hatarini ya kupoteza kile walicho nacho wakati ule wa dhiki kuu, mwishowe watafikia makao yenye utukufu (soma Ufu. 7:9-17; 21:4-5). Je, wewe utakuwa mmoja wao? Bado kuna nafasi!
Na kwa ajili ya ahadi katika maandishi matakatifu, walio na imani wanafaa kujitahidi na kuendelea katika safari hii yenye shida na matatizo mengi. Ikiwa wataendelea kuwa na imani hadi mwisho, basi wataurithi ufalme wa mbinguni, na kutawala na Kristo duniani baadaye. Ndivyo tusomavyo katika Ufunuo:
"Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa sababu ya ushuhuda wa Yesu, kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomusujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu moja" (Ufu. 20:4).